Kauli za Mkuu wa Mkoa wa Dar, Amos Makalla, zinakiuka Haki za msingi za Binadamu

Kipindi Cha Jiwe Hauwezi kumsikia ndani ya week Moja huyu kamuuwa mke wake ,huyu kamuuwa mpenzi wake ,huyu kambaka mtoto ,majambazi yamvamia wakala .Watu walijua Kuna mwamba anatawala ,upole usipitilize Watu wanakushika kwenye macho ,acha tujionee
 
Angeongezea au Mochwari qmmmk kuna coworker wamevamia kwake juzi night wamembaka housegirl sasa yeye hatujui maana alisema yy hawajamfanya kitu ila wameiba vitu na kuwajeruhi.
 
Ningekuwa police au Mimi ndio IGP ukikamatwa wewe panya road Unafanya uharifu unamezeshwa Uji WA cement halafu unatupwa basi.


Unaua wenzako halafu wewe ukiuawa mnaleta mambo ya haki za binadam.


Mpuuzi weww
 
Wewe ni mpuuzi , kama Una mwanao panya road jiandae kuokota mzoga.
 
Mama yako na familia yako ndio Wana Jukumu la kukurekebisha tusipeane majukumu.

Ukishindwa kumrekebisha mwanao jiandae kurekebishiwa na jamii. Huku atapigwa Shaba au kuchomwa Moto
 
Na panya rodi wanalinda haki za binadamu.
 
Mkuu 'Mystery', HESHIMA MKUU, kwa sababu huwa nafurahia sana mada zako hapa jukwaani; ila sijaona umuhimu wa hii hapa, isipokuwa kama una mfupa tu wa kusaga na huyo mkuu wa mkoa.

Sitetei uvunjifu wa haki za mtu yeyote, kama nisivyopendezwa na uvunjifu wa sheria na hawa wahuni, tena watoto wadogo tu, huko mitaani.

Hawa wanatakiwa kila wakikamatwa wacharazwe viboko na kurushwa vichura hadi akkili ziwaingie kichwani.

Ni upuuzi usio na kimo kujaribu kutetea kwa njia yoyote matendo ya kishenzi yanayofanywa na hawa watoto.

Ndiyo, polisi wana mchango mkubwa sana katika kuacha hali iwe mbovu kiasi ilivyo sasa. Hivi vitendo siyo vya ghafla tu, huanza taratibu, tena kwa uoga mkubwa, wanapoona udhaifu wa jamii na polisi, wanazidi kuwa na ujasiri mkubwa kuendeleza vitendo hivui viovu na kuanza 'recruitment' ya watoto wengi zaidi.

Si lazima wauliwe, lakini mtoto yeyote anayejiingiza kwenye vitendo hivi ni lazima afahamu mbele ya safari kwamba hawezi kutoka salama. Huo ndio ujumbe muhimu unaotakiwa kusisitizwa.

Ni lazima wajuwe mbele ya safari, kwamba katika kutenda wanayotenda, inawezekana kabisa kutokuwepo na fursa ya kufikishwa mbele za sheria (mahakamani), kwa sababu matendo wanayofanya wao wenyewe hayawapi nafasi wanaowatendea nafasi ya kujitetea.

Sioni sababu ya lawama kwa mkuu wa mkoa kusema aliyoyasema; labda kama yapo ambayo siyajui.
 
Ni kweli mkuu,wewe umeona kama Mimi maana Jana alitamka kauli Kali Sana Wakati angepunguza jazba na kumezea Ili washughulike kimya kimya..

Ila kusema mtoto wako akipotea kamtafute Polisi au hospital manake ametia amri ya kupiga watu risasi,inaweza kumletea kuwa uhalifu dhidi ya ubinadamu..
 
Mama yako na familia yako ndio Wana Jukumu la kukurekebisha tusipeane majukumu.

Ukishindwa kumrekebisha mwanao jiandae kurekebishiwa na jamii. Huku atapigwa Shaba au kuchomwa Moto
Lunatic
 
Unajua magenge ya mafia ya Colombia yalianzaje? Liko wapi kosa la RC kutoa angalizo kwa wazazi? # Hebu tuiache serikali ifanye kazi zake. Inajua na kuzingatia haki za binadamu .🙏🙏🙏
 
Ila madogo acha washikishwe adabu, maana ndo tunaitwa wanaume wa Dar, yaani hatujiwezi kwa lolote mpaka tunatishwa na hivi vitoto viteja.
hofu kupitia hilo polisi wasio waaminifu waweza gonga watu wasio na hatia kauli jumuishi sio zurisana
 
Wapuuzi kama nyie ndo hamfai...
Mbona wanapouliwa wasio na hatia hamsemi kitu
 
Mkuu wa mkoa Hana sababu ya kuomba msamaha, Hivi unajuwa uchungu wa ndugu waliopoteza ndugu yao kwa kuuwawa na hao panya Road?? Ungepatwa na msiba ule ungekuja na kupata nguvu ya kuandika hayo uliyoandika hapa? Una maslahi gani na hao vibaka wanaotesa wananchi bila hatia? Kwanini usiandike makala ya kuwasihi wazazi juu ya kuchunga mienendo ya watoto wao? Kwanini usiandike makala ya kuwaasa hao vibaka kuacha tabia hiyo? Unajuwa maumivu ya kukatwa na mapanga wewe?

Tuondolee uanaharakati wako hapa wakati watu wanaumia. Kwani wewe ulitaka asema wazazi wakawaangalie wapi watoto wao? Ulitaka asema wakawaangalie hotelini? Au kanisani? Au ulitaka aseme wakawaangalie shuleni? Acha serikali ifanye kazi yake ya kulinda raia wake, Kama mwanao Ni mhusika mwambie aache Mara moja vinginevyo utamkuta huko ulikoelekezwa, ndio nyie mnakuwa mnatetea mambo yanayokwenda hata kinyume na utamaduni wetu kwa madai ya uanaharakati na haki za binadamu
 
Hali ya uchumi ni ngumu sana.

Hao panya road wameona uhalifu ndio suluhisho la kujipatia kipato.

Wakipora wanasaidia na familia zao.

Hili tatizo lina mizizi mirefu sana.

Halitamalizwa kwa kauli tu.
Uchumi Kama mgumu mbona wewe siyo jambazi au kibaka? Nani kakwambia Hilo ndio suluhisho, kwa hiyo uchumi ukiwa mgumu utawaambia wanao wakawe panya Road?
 
Hakuna ujinga Kama huo hao wakibainika lazima wapewe haki yao maana wametesa raia vya kutosha, Kama wewe unamwanao huko Basi utamkuta ulikoambiwa
Ndiyo maana nikasema hao Polisi wanapashwa kufanya Kazi kwa kufuata Weledi.

Kupokea maelekezo toka juu, ambayo wanajua yanakiuka sheria, itakuja kula kwao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…