Kauli za sasa za Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kuhusu CORONA zimeshaanza Kuzua 'taharuki' nchini, hivyo ama adhibitiwe au ajiuzuru upesi

Jamaa huyu hapa anatuombea,so ninyi pigeni kazi serikali isikose hela
Your browser is not able to display this video.
 
kila mara nasema corona INAJIONYESHA YENYEWE..
Hata usipopima watu kama wapo wanaoumwa wataonekana..
JE wapo hao wanaonekana?.
WANA DALILI KUWA WANA CORONA?.
Korona haijifichi mzee.

"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"

Kwa hiyo waliowekeza kwenye vipimo na kuwatenga walioathilika hawajui kua unaonekana?!
Kwa taarifa yako kuna wengine wengi ni asymptomatic wanaeneza na mtu kawaida anaanza kuugua baada ya wiki mbili au zaidi
 
Hatua zipi serikali imechukua mkuu? Kutembeza bakuli au kutuambia tukachape kazi?
 
Kuchelewa kuwazuia Wachina na au kuwaweka karantini siku 14 kabla hawajaanza umachinga wao hapa Tz yaweza kutugharimu maisha ya WATZ wengi.

Wamefikia wangapi hadi jioni hii?

Kuna waliotangulia mbele za haki?
Tumeshaambiwa mmoja mkuu.
 
kila mara nasema corona INAJIONYESHA YENYEWE..
Hata usipopima watu kama wapo wanaoumwa wataonekana..
JE wapo hao wanaonekana?.
WANA DALILI KUWA WANA CORONA?.
Korona haijifichi mzee.

"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"
We kenge soma hii attachment alafu uache kutetea ujinga
 

Attachments

  • IMG-20200409-WA0030.jpg
    50 KB · Views: 1
Mbona kauli ya Ummy ya kistaarabu nchi za ulaya wanaambiwa kuna watu mtapoteza ndugu na marafiki kabla ya wakati wao huo ndio ukweli ambao muwe tayari kuupokea.

Hakuna kurembua macho kwenye vita ya Corona watu wanatakiwa kupewa ukweli ili waongeze umakini wa kujilinda simple as that.
 
Tatizo watanzania tunapenda kuremba maneno, hata kama ni kibaya wanataka ukiongelee kwa uzuri, tujifunze kusema ukweli, nyeusi siku zote itabaki kuwa nyeusi na haiwezi kuwa nyeupe. Hivyo alivyosema ndio ukweli ulivyo, hata hiyo Italy na USA walipitia stage kama hizo tunazopitia sisi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu namna alivyoiwasilisha kwa wengi ni kama amewatisha na imezua taharuki pia Kwao. Na hii ni kwa mtazamo wangu ambao simlazimishi Mtu mwingine akubaliane nao japo anatakiwa Kuuheshimu kama nami pia ninavyoheshimu Mitazamo yao.
Bro asilimia kubwa ya watu wanaoishi mijini wanajua corona ni nini na namna gani ya kuepuka maambukizi ya corona, unataka asemaje sasa? Huo ndio ukweli na kitakachofuatia ni lock down hizo propaganda za kina Bashite zisitupumbaze

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwenyezi Mungu tunasulu sisi waja wako .


Sent from my iPhone using JamiiForums
 

Wangefanya curfew siku za weekend, yaani ijumaa Hadi jumapili hakuna kutoka nje... Kwa majaribio.
Alisikika raia mmoja wa Kongo akiongea.
 
Umejaribu kuongea kuhusu uwasilishaji wa taarifa na namna unavyoweza kuleta madhara makubwa kisaikolojia Ni vizuri.

Lkn mimi sidhani kwa upande mwingine inaweza leta taharuki kiasi hicho ambacho umejaribu kuaminisha umma. Watanzania kwa asilimia kubwa kwa utafiti nilioufanya katika kipindi hiki ambacho Dunia na Taifa letu linapitia katika wakati mgumu wavkuoambana na COVID-19, Wamekuwa wakifuatilia kwa ukaribu mkubwa Sana yanayoendelea katika nchi nyingi duniani na namna wanavyohangaika na janga Hili.Haijalishi serikali kupitia wizara ya afya itanawasilishaje ujumbe kuhusu Hali ya corona lkn watanzania wanaelewa Hali iliuopo duniani.

Chamsingi tulipo sahivi sio jukumu la serikali tu kujaribu kujenga saikolojia ya watu kuhusu Tahadhari kubwa ya corona, initiatives zianzie katka family level ili Serikali iwe kazi rahisi Sana kuhusu Hilo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cha muhimu ili Serikali iweze kuzuia maambukizi mapya na ugonjwa wa corona kufika sehemu ambazo bado hazijapata hata mgonjwa mmoja, ingegawa mask (barakoa) hasa kwa mikoa yenye magonjwa wa corona na kutoa amri kila mtu avae pindi anapokhwa nje ya nyumba yake au kwenye shughuli zake binafsi na kuzuia safari za kuvuka mkoa (mabasi na gari binafsi) isipokuwa maloli tuu ya mizigo ili kuendeleza shughuli za kiuchumi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…