Kauli za Sheikh Mwaipopo; athari zake kwa jamii, ukimya wa polisi na fundisho la Rwanda 1994

Kauli za Sheikh Mwaipopo; athari zake kwa jamii, ukimya wa polisi na fundisho la Rwanda 1994

Mjadala mkali unaoendelea hivi sasa nchini Tanzania unamhusu kiongozi wa dini, Sheikh Said Mwaipopo, ambaye ananyoshewa vidole na wananchi wengi, wanaharakati, na wachambuzi wakiamini anatumika kama chombo cha ukandamizaji dhidi ya sauti mbadala.

Katika siku za hivi karibuni, kiongozi huyu ametoa mfululizo wa kauli ngumu zenye vitisho vya wazi vya kuwadhuru kisaikolojia na kimwili raia wanaokusudia kufanya maandamano ya amani kuelekea tarehe 7 Julai.
Lugha anazotumia, ikiwemo kutishia kwamba waandamanaji "watakatwa vichwa" au "kutahiriwa bila ganzi", pamoja na kutambulisha hadharani kikundi cha vijana cha doria alichokiita "Mbwa Mwitu", zimezua taharuki kubwa na kuacha maswali mengi juu ya mwelekeo wa utawala wa sheria nchini.

Mwenendo huu mkali wa Sheikh Mwaipopo unakuja katika kipindi ambacho chama tawala, CCM, kinaonekana kuzidiwa kete kihoja na kiushawishi kila kona na chama kikuu cha upinzani, CHADEMA, hasa katika kuwasha moto wa ufahamu wa haki za kikatiba na kijamii miongoni mwa wananchi.

Kuimarika kwa CHADEMA kumeongeza shinikizo kubwa kwa mfumo wa utawala, jambo linalofanya mbinu za kisheria na kisiasa za kuzuia harakati zao zionekane kushindwa kufua dafu mbele ya umma uliochoka.
Katika mazingira haya, kauli za vitisho kutoka kwa watu kama Sheikh Mwaipopo zinatafsiriwa kama mkakati wa kukata tamaa wa kutumia nguvu mbadala na hofu ili kuzuia mawimbi ya mageuzi ambayo CHADEMA imefanikiwa kuyajenga miongoni mwa wananchi wanaotaka mabadiliko.

Fumbo kubwa zaidi katika sakata hili liko kwenye ukimya wa ajabu na unaoshangaza wa Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.
Chini ya sheria za jinai za Tanzania, mtu yeyote anayetoa vitisho vya kuua, anayechochea vurugu, au anayeanzisha kikundi chochote cha ulinzi nje ya jeshi rasmi, huwa anakamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa haraka sana.

Ukweli kwamba Sheikh Mwaipopo anaendelea kutoa kauli hizi mbele ya vyombo vya habari na hata kuonesha hadharani kikundi chake cha "Mbwa Mwitu" bila kuguswa na polisi, unatoa taswira kuwa kuna nguvu kubwa ya kiserikali iliyoko nyuma yake ikimlinda na kumtuma.
Mkakati huu unalenga kumtumia yeye kama "skrini" ya kufanya kazi chafu ya kutishia raia, ili serikali isionekane kukiuka haki za binadamu moja kwa moja.

Hali hii inapaswa kutoa angalizo zito kwa taifa kwa kutazama yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994, ambapo mbegu za mauaji ya kimbari zilianza kupandwa kwa namna inayofanana na hii. Kabla ya maafa hayo, viongozi wa kijamii na vyombo vya habari (kama redio ya RTLM) viliruhusiwa na vilitumiwa na mfumo uliokuwa madarakani kutoa lugha za vitisho, dharau, na kuchochea chuki dhidi ya raia wenzao bila kuchukuliwa hatua yoyote na vyombo vya dola.

Ukimya na ulinzi wa serikali kwa wachochezi hao ulihalalisha uundaji wa vikundi vya vijana vilivyojichukulia sheria mkononi (kama Interahamwe), ambavyo hatimaye viliitumbukiza nchi hiyo kwenye maafa makubwa ya kihistoria.

Historia inafundisha kuwa, pale vyombo vya dola vinapochagua upande na kuruhusu watu binafsi kutumia mwamvuli wa dini au ukada wa kisiasa kutishia uhai wa raia wengine, misingi ya amani hupasuka kwa kasi sana. Tanzania haiko salama kama itaendelea kufanya macho juu ya kauli za namna hii. Ni jukumu la vyombo vya sheria kukomesha ubaguzi huu wa kiutendaji na kusimamia sheria kwa usawa kwa kila raia, bila kujali anaitetea serikali au anaipinga, ili kuepusha taifa kuingia kwenye mtego wa machafuko yaliyowahi kugharimu maisha ya mamilioni ya Waafrika huko nyuma.

Pia soma Askofu Mwamakula: Unajua sababu za Sheikh Mwaipopo kutaka 'Kuwatahiri watu bila ganzi'?
View attachment 3618965View attachment 3618966View attachment 3618967View attachment 3618968
Ukiona mbwa juu ya mnazi 🥥 ujue kapandishwa
Serikali ya Samia inawatumia mashehe kuongea watakavyo na hawachukuliwi hatua yoyote
 
Huyo mwaipopo ni mlemavu wa ubavu ni wateke moja la ubavu anajifia kabisa muache awajaze upepo hao uvccm na green guard waje kichwa kichwa temu hii watakula za vichwa na wao
Afu ushaona wapi mtu anaitwa sheikh mwaipopo
Tatizo nyuma ya pazia wana backup yenye uwezo wa kuwapa chochote
 
Nilipo waambia hapa JF kuwa mauaji ya October yaliratibiwa kidini watu waliniona mpumbavu ...kikundi cha Raia feki kinacho shika serikali kwa sasa kinatumia uislamu kama moja wapo ya silaha zake..
Ulikuwa sahihi sana na huyu alikuwa sehemu yao
 
huyu jamaa kakosea sana kuwatambulisha hao wahuni huku wamevalia kislam.unataka kutuambia vijana hao ni waislam?
Aliyewaweka anaweza kuwa na jibu sahihi sio mimi
 
Behind the scene.

Huyu shehe hajitambui anaweza kujikuta katika wakati mbaya asioutarajia. Hebu vuta picha kuwa ametumika ili kuwatisha watu tu na hana uwezo wa kufanya aliyoyasema.

Alafu ikatokea watu (kikundi) kisichohusiana na yeye kikaanza kutekeleza kwa vitendo hayo aliyoyaesema. Je atakuwa na mlango wa kutokea?
Alafu huo ujasiri wa kuita wandishi na kuonyesha vijana hao kautoa wapi kama sio kwa mamlaka kubwa zaidi ya polisi walinda usalama wa raia na mali zao?
Kingine cha kusikitisha ni hao vijana waliokwenda kuuza sura zao kwa watanganyika kuwa wao wana uwezo wa kukata vichwa na kutahiri bila ganzi Je wanajitambua kweli? Au wameahidiwa nini mpaka watoke adharani kuonyesha uovu wao?

Mhh!!? Ngoja niishie hapa maana maswali ni mengi humu kichwani. Labda anayewaza kujibu mawazo yangu anisaidie.
 
Mi naamini anajua anachokifanya
 
Mkuu Mimi binafsi kinachouma ni kweli ndio Akili hizi za IDARA ZA USALAMA zipo hivyo?
Hii NCHI ya kijikundi cha watu.

Sisi tunaotafuta riziki juani athari zake tumeanza kuziona.

Halafu wamekaa kimya ..ni UPUUZI WA HALI YA JUU sikiwahi fikiria kama kuna watu UPSTAIR huko ni weupe to such extent.

Kama kuna mtu yupo nyuma ya hao na wote wanaoandaliwa basi AKILI HANA/HAWANA.
 
View attachment 3618970Tumesema hivi, ninao vijana hatari. Nina vijana hatari mno, yaani usiguse usijaribu, ni vijana hatari mno. Hawana cha kupoteza hawa vijana. Yaani hawana cha kupoteza, ni vijana hatari mno. Na ndio maana nikawafananisha sawa na mbwa mwitu, ni mbwa mwitu. Mbwa mwitu anakimbia kilomita ishirini bila kuchoka, ndio hawa vijana walioko nyuma yangu. Kilomita ishirini bila kuchoka. Yaani usiguse. Wana uwezo wa kutembea juu ya kamba kilomita moja mpaka mbili, juu ya kamba"
Akamatwe huyu ni gaidi na pengine ndiye anayehusika na upoteaji wa watanzania.
 
Behind the scene.

Huyu shehe hajitambui anaweza kujikuta katika wakati mbaya asioutarajia. Hebu vuta picha kuwa ametumika ili kuwatisha watu tu na hana uwezo wa kufanya aliyoyasema.

Alafu ikatokea watu (kikundi) kisichohusiana na yeye kikaanza kutekeleza kwa vitendo hayo aliyoyaesema. Je atakuwa na mlango wa kutokea?
Alafu huo ujasiri wa kuita wandishi na kuonyesha vijana hao kautoa wapi kama sio kwa mamlaka kubwa zaidi ya polisi walinda usalama wa raia na mali zao?
Kingine cha kusikitisha ni hao vijana waliokwenda kuuza sura zao kwa watanganyika kuwa wao wana uwezo wa kukata vichwa na kutahiri bila ganzi Je wanajitambua kweli? Au wameahidiwa nini mpaka watoke adharani kuonyesha uovu wao?

Mhh!!? Ngoja niishie hapa maana maswali ni mengi humu kichwani. Labda anayewaza kujibu mawazo yangu anisaidie.
Behind the scene.

Huyu shehe hajitambui anaweza kujikuta katika wakati mbaya asioutarajia. Hebu vuta picha kuwa ametumika ili kuwatisha watu tu na hana uwezo wa kufanya aliyoyasema.

Alafu ikatokea watu (kikundi) kisichohusiana na yeye kikaanza kutekeleza kwa vitendo hayo aliyoyaesema. Je atakuwa na mlango wa kutokea?
Alafu huo ujasiri wa kuita wandishi na kuonyesha vijana hao kautoa wapi kama sio kwa mamlaka kubwa zaidi ya polisi walinda usalama wa raia na mali zao?
Kingine cha kusikitisha ni hao vijana waliokwenda kuuza sura zao kwa watanganyika kuwa wao wana uwezo wa kukata vichwa na kutahiri bila ganzi Je wanajitambua kweli? Au wameahidiwa nini mpaka watoke adharani kuonyesha uovu wao?

Mhh!!? Ngoja niishie hapa maana maswali ni mengi humu kichwani. Labda anayewaza kujibu mawazo yangu anisaidie.
Hana hicho kikundi bali amehakikishiwa kipo na ni kutoka uvsisiemu.. Wanamjaza upepo avuruge.. Mambo yakiharibika watamtoa kafara kivyovyote vile. RIP Shehe majini
 
Back
Top Bottom