Heshima sana wanajamvi.
Imekuwa kawaida na utaratibu kila mwanachama au kiongozi wa CHADEMA anayeondoka kupewa majina mabaya ana tamaa,mamluki,wamenunuliwa,team Mbowe na nk.
Viongozi na wanachama wa kawaida wanaondoka wengi wametoa sababu mbali mbali nyingine zina mashiko na nyingine hazina mashiko.
NRNE imeleta mkanganyiko mkubwa ambao pengine kama Viongozi wa sasa wa CHADEMA wangeweza kuuelezea kwa ufasaha zaidi na namna bora ya kuzuia uchaguzi.
Namna bora ya kuzuia uchaguzi ni kushiriki uchaguzi.
Hii mipango ya Lissu ya kulala barabarani itashindwa vibaya sana kwasababu zifuatazo.
Mosi uchaguzi unatatajiwa kuhitimishwa mwezi October 2025.Mchakato wa uchaguzi unatarajiwa kuanza mwezi July mara baada ya bunge kuvunjwa.
Pili Kipindi cha kampeni nadhani ni siku tisini (90 days) vyama vilivyo sign kanuni za uchaguzi ndivyo vitakavyo ruhusiwa kufanya kampeni.
Tatu usipokuwa na WAGOMBEA Madiwani,Wabunge & Rais kipindi cha kampeni nani atazuia uchaguzi.WAGOMBEA ni watu muhimu wa kuongoza mashambuzi ya NO REFORM NO ELECTION.
Lissu na KAMATI KUU wanakosa mbinu bora na muhimu za kuzuia uchaguzi kwasababu wanafikiri wana akili kuliko WATANGANYIKA wote.
Kwa hakika Lissu anakwenda kukimaliza chama kwasababu ya kukosa maarifa na mikakati madhubuti na mahiri.
Tabia ya kuwabeza wale wote wanakikimbia chama na kuwapachika majina ya ajabu ajabu mtakuja kujuta mwezi November 2025.
Ruksa mapovu.
Ngongo Std 4B.