Kausha damu zote zifungiwе, benki zibaki kuwa taasisi pekee za kutoa mikopo

Kausha damu zote zifungiwе, benki zibaki kuwa taasisi pekee za kutoa mikopo

upupu255

Senior Member
Joined
Sep 4, 2024
Posts
119
Reaction score
144
Wadau za wikiendi!

Wakati napita facebook huko nikakutana na post ya huyu jamaa akanikumbusha maumivu ya hii mikopo maarufu kausha damu namna ambavyo ilidhoofisha afya ya dada yangu, akihangaika kulipa mikopo ya aina hii.
WhatsApp Image 2024-09-14 at 14.00.32.jpeg
Stori gani unaikumbuka ukisikia kausha damu?
 
Muwafundishe watoto Mathematics hata kwa viboko. Watu ni wajinga mno kwenye kupiga hesabu za riba. Kausha damu wana ujanja wa kuwaambia watu kuwa riba ni 5% tu kumbe hiyo 5% ni asilimia ya hela yote uliyokopa na ukipiga hesabu kwa miezi 6 labda utarudisha 30% ya pesa yote. Mtu akija kushtuka tayari imekula kwake. Watu wapige hesabu za riba ili kuangalia kama biashara yake itarudisha mkopo bila kuyumba.

Pia chukua mkopo kipindi hauhitaji. Usichukue mkopo wakati mambo yako ni magumu. Ukichukua mkopo wakati biashara inafanya vizuri utakuwa na utulivu mkubwa wa akili kupiga hesabu zako vizuri na kurudisha bila presha. Pia mkopo ni wa kukuza biashara na tumia kwenye biashara tu. Usitumie hela ya mkopo kufanyia jambo lingine lolote nje ya biashara. Hata kama ni kumlipia mtoto ada.

Wapuuze Motivational speakers wanaosema daima maisha ni ku-take risks. Calculate all the risks. Usijiendee tu kukopa bila kuangalia hatari zinazoweza kujitokeza na plan B za kufanya endapo mambo yakaenda sivyo.
 
Hivi wanalazimisha kukopa

Ova
Enzi nikiwa na miaka 23 nilikopa kwa hawa loan sharks wa mjini kama Tsh 250k nikachelewa kwa siku moja tu kurudisha wakataifisha TV niliyoweka dhamana. Ile TV iliniuma sana ilikuwa Sony flat screen 24" mpya enzi hizo ndo zinaanza kuvuma. Akajitokeza dada yangu fulani wa mtaani akadai bora ningemuuzia yeye ile TV alikuwa anaitamani.
 
Enzi nikiwa na miaka 23 nilikopa kwa hawa loan sharks wa mjini kama Tsh 250k nikachelewa kwa siku moja tu kurudisha wakataifisha TV niliyoweka dhamana. Ile TV iliniuma sana ilikuwa Sony flat screen 24" mpya enzi hizo ndo zinaanza kuvuma. Akajitokeza dada yangu fulani wa mtaani akadai bora ningemuuzia yeye ile TV alikuwa anaitamani.
Aise mikopo yao hawa haifai
Benki zingelegeza masharti ya mikopo angalau watu wakimbilie huko

Ova
 
Unadhani nyingi zipo kisheria au zinakata kata corner; nyingi hazikidhi matakwa ya Huduma za Kifedha kulingana kama ni Bank, Micofiance, Saccos au Vicoba.., ila ndio hivyo loan sharks wanapata hio opportunity kutokana na desparation ya watu...

Pili benki inataka collateral na wananchi wengi sio credit worthy hivyo benki hawawezi kuwasogelea hata kidogo..., Kwahio cha muhimu ni kuhakikisha wananchi wengi wanapata ujira yaani angalau tuwe na middle income wengi ambao kipato chao kinakidhi mahitaji yao..., otherwise kesho itazidi kuwa mbaya kuliko leo

All in all usisikilize porojo za serikali madeni sio jambo jema iwe serikali au machinga kitaa....
 
Back
Top Bottom