Kausha damu zote zifungiwе, benki zibaki kuwa taasisi pekee za kutoa mikopo

Kausha damu zote zifungiwе, benki zibaki kuwa taasisi pekee za kutoa mikopo

Muwafundishe watoto Mathematics hata kwa viboko. Watu ni wajinga mno kwenye kupiga hesabu za riba. Kausha damu wana ujanja wa kuwaambia watu kuwa riba ni 5% tu kumbe hiyo 5% ni asilimia ya hela yote uliyokopa na ukipiga hesabu kwa miezi 6 labda utarudisha 30% ya pesa yote. Mtu akija kushtuka tayari imekula kwake. Watu wapige hesabu za riba ili kuangalia kama biashara yake itarudisha mkopo bila kuyumba.

Pia chukua mkopo kipindi hauhitaji. Usichukue mkopo wakati mambo yako ni magumu. Ukichukua mkopo wakati biashara inafanya vizuri utakuwa na utulivu mkubwa wa akili kupiga hesabu zako vizuri na kurudisha bila presha. Pia mkopo ni wa kukuza biashara na tumia kwenye biashara tu. Usitumie hela ya mkopo kufanyia jambo lingine lolote nje ya biashara. Hata kama ni kumlipia mtoto ada.

Wapuuze Motivational speakers wanaosema daima maisha ni ku-take risks. Calculate all the risks. Usijiendee tu kukopa bila kuangalia hatari zinazoweza kujitokeza na plan B za kufanya endapo mambo yakaenda sivyo.
Unakopa unafanya sherehe ya birthday!
 
Back
Top Bottom