Kauziwa rice cooker Tsh. 300,000 na Waturuki, kaikuta inauzwa Tsh. 140,000 Mlimani City. Anawaza amalizie hela yao ama?

kuna mahali niliwaona wanagawa vyombo kama njugu

kigezo ni uwape namba za simu wanakupigia ikiita basi wanakukabidhi vyombo ,japo ni vya daraja la chini ila nilitazama ule utaratibu wao wa ugawaji wa vyombo ni rahisi sana kurushwa

NB: ilikua ni mkoani
 
Sasa si na riba juuu hapo yani mtu akuuzie kitu unalipa kidogo kidogo miezi 4 bado unalalamika kama ulikuwa na uhitaji ungeenda mwenyewe kuitafuta huko mlimani city kabla.
Kabisa boss, kukaa na pesa ya mtu miezi 4 ndio imezaa hiyo riba kubwa.
 
Walikuja kazini na vyombo vyao wanauza ghali balaa. Kuna mmoja nikamsanua kuwa hayo masufuria unayotaka kuuziwa laki5 yanauzwa laki na tisini, akahisi namuonea wivu. Akayanunua then after a week ndio anaujua ukweli. Aliumiiiiaaa ila ndio ikawa ashapigwa.
 
Sasa huo si mkopo mkuu, 140,000 kwa 300,000 ni halali ila tu hakikisha unamaliza deni lao ndani ya mwaka mmoja au zaidi ili wote mnufaike,kwani ukiwa mkali ni waoga sana wa polisi,wewe wakikuzengua waambie mwende mahakamani,tambua hao watu ni wakwepa kodi,hivyo hawawezi kukubali polisi au mahakamani hawana pa kukupeleka hao.

Mimi ndani mwangu nina vitu vyao vingi,juzi wameniuzia oveni kwa sh 420,000 wakati dukani ina 200,000,nimekaa nayo miezi mitatu bila kulipia,mwezi huu ndo nimewalipa,ninampango wa kumaliza kulipa deni mwaka kesho mwezi wa 12 ilikhali tulielewana mwezi wa kumi na mbili mwaka huu.
Daah...hao Jamaa bhana!!
Kuna Jamaa aliwazingua nadhani ni wahindi hakuwalipa, pesa yote alibakiza Kama 150k kwenye bidhaa ya 500k so wakamtishia kwenda kuichukua, ama wampeleke polis!
Akawaambia waende polisi tu, watakutana mahakamani kwanza hawakumpa risisiti ya efd, plus mikwara kibao sijui iliishia wapi!!!
Kiufupi hao mawhite wanawapiga watu sana maofisini, majumbani n.k
 
Hivi kwanini wabongo wengi hawapendi kujiongeza kabla..

Yaani mtu mali ya mkopo anataka auziwe kwa bei ile ile tu.

Unauziwa simu ya laki 2 kwa laki 4 kwa malipo ya mwaka mzima halafu unalalamika!!.
Kwanini usiende kununua huko kwa laki 2!!
 
Ukishaambiwa mkopo jua bei itakuwa juu zaidi. Unapaswa kuuliza cash ni kiasi gani ili upime gharama ya ww kuchukua kwa mkopo.
Hao Jamaa naskia hawakubali cash!
Ukitaka kuwapa cash wanakataa, kwamba wanataka ukae na bidhaa angalao mwezi mmoja ndio hapo wanapumguza kidogo!
 
Niliuziwaga presha kuka Laki tatu. Nikazama mtandaoni kumbe linauzwa laki na selasini. Niliumia sana.
Screenshot_20231231-172526_WhatsApp.jpg
 
Mbaya zaidi hawakutajii walipo. Nilipanga niende kuwabwagia hapo dukani. Kama mbwai mbwai.
 
Wamama wanapigwa sana na hao jamaa kila sehem wametapakaa kama wachina na madubu
 
Sasa huo si mkopo mkuu, 140,000 kwa 300,000 ni halali ila tu hakikisha unamaliza deni lao ndani ya mwaka mmoja au zaidi ili wote mnufaike,kwani ukiwa mkali ni waoga sana wa polisi,wewe wakikuzengua waambie mwende mahakamani,tambua hao watu ni wakwepa kodi,hivyo hawawezi kukubali polisi au mahakamani hawana pa kukupeleka hao.

Mimi ndani mwangu nina vitu vyao vingi,juzi wameniuzia oveni kwa sh 420,000 wakati dukani ina 200,000,nimekaa nayo miezi mitatu bila kulipia,mwezi huu ndo nimewalipa,ninampango wa kumaliza kulipa deni mwaka kesho mwezi wa 12 ilikhali tulielewana mwezi wa kumi na mbili mwaka huu.

Slogan yangu siku zote ni:mambo ya kihuni humalizwa kihuni
Yote hayo ya nini ?..

Lipa deni la watu.
 
Walimu mna shida sana, kila kitu mnakopa
 
wahuni sana hawa washamuziaga mdada flani plate 2 za gasi kwa 300k ambapo madukani unapata kwa 100k
 
Back
Top Bottom