Kava nzuri hunyonya mstuko, heri kutumia simu bila kava kuliko kava gumu linalobana sana, simu inapodondoka mshtuko unanyonywa na simu badala ya cover

Kava nzuri hunyonya mstuko, heri kutumia simu bila kava kuliko kava gumu linalobana sana, simu inapodondoka mshtuko unanyonywa na simu badala ya cover

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Si kila kava ni kwajili ya ulinzi wa simu, Kuna kava ambazo zipo kwajili ya mvuto, ikiwa unanunua kasha kwa lengo la mvuto chagua yoyote itayokuvutia lakini kwa lengo la ulinzi hasa kwetu wenye uchumi wa kawaida tunaopenda kutunza simu, yatupasa kujikita na hadhi ya ulinzi wa kasha.

Kava nzuri ya simu hupunguza athari au nguvu inayotokana na mshtuko, mtikisiko, au mgongano.

Chukulia mfano wa viatu, ukivaa kiatu kinachokubana sana halafu ujikwae au uvae kiatu cha chuma / plastic ngumu halafu ujikwae, ni mwili wako ndio utanyonya hicho kishindo na kupelekea maumivu, ukivaa raba flexible ukijikwaa mstuko unanyonywa kwenye kiatu.

Ndivyo ilivyo hata kwa simu, Ni vizuri zaidi utumie kava ambayo ina material laini mfano iwe material ya mpira, lether ama ya mkanda, sponchi, n.k. kutumia kava ngumu kama ya chuma, mbao, plastiki gumu, n.k. mara nyingi simu ikidondoka inazidisha hatari ya simu kuharibika kwasababu kishindo / mshtuko hunyonywa kwenye simu badala ya kava.
 
Cover yangu imetengenezwa kwa golden fibre na titanium alloys. Very expensive!!
 
Mkuu umeongelea kava kama kava au mimi ndio sijaelewa kitu hapa!
vuta picha umevaa kiatu kimekubana halafu ni cha chuma, ukijikwaa vidole ndivyo vitavyonyonya kishindo na kupelekea maumivu tofauti na raba
 
Se86811019cef4809b2f54c4b89b0a8030.jpeg
S01ee98c6afc54bfca26b71e25ec7cc03d.jpeg
Screenshot_20250103-202533.png
 
Back
Top Bottom