Makanyaga nadhani hili suala hulifahamu vizuri.
Kwanza ujue tu, eneo lote la magomeni kota na zile nyumba zote za kota za zamani pale zilikuwa ni mali ya serikali kwa 100%. Hakuna mtu aliwahi kumilikishwa nyumba au eneo pale. Hivyo mtu yoyote akiondolewa pale hawezi kudai chochote popote pale.
Pili, kilichotokea ni kuwa, serikali iliamua kubadilisha matumizi ya eneo lile kwa kubomoa nyumba za zamani ili kujenga nyumba mpya za kisasa ili kuziuza au kupangisha. Sasa wale wapangaji wa zamani wakahaidiwa (kisiasa, kiungwana na kiutu) na serikali kuwa, mara mradi wa ujenzi utakapo kamilika basi watapewa nafasi ya kupangishwa au kuuziwa. Sasa wakati wa kuuziwa ndio huu, wapangaji wanataka ama wapewe bure au wauziwe kwa bei sawa na bure!
Serikali imesema jambo hilo hapana na haliwezekani.