Marie Antoinette
JF-Expert Member
- Jan 28, 2019
- 426
- 412
SEHEMU ya I
"Inshu ya Banyamulenge, ni kisingizio tu! Ni kitu ambacho hakipo. Iliisha mwaka 2002". Anasema Nyamwasa.
Baada ya vifo vya wanajeshi wa Afrika kusini kufia vitani nchini DRC, mpaka sasa inaripotiwa wanajeshi 14 ndo waliopoteza maisha.
Hili jambo lilizuwa maswali mengi, wengine wakiituhumu serikali ya Afrika kusini, kuwataka wanajeshi hao wapigane na M23, huku wakiwa hawana mafunzo ya kutosha na vifaa vya kukabiliana na waasi wa M23.
News Room Afrika, chombo cha habari cha nchini Afrika kusini, kilimualika Kayumba Nyamwasa kuweza kuwajuza wasikilizaji mengi yanayohusiana na mgogoro huo.
Kayumba Nyamwasa, aliyekuwa mkuu wa majeshi nchini Rwanda, badae akawa Balozi wa Rwanda nchini India, ambaye kwa sasa anaishi nchini Afrika kusini,Kayumba pia aliwahi kuwa mkuu wa kitengo cha upelelezi chini Rwanda, kabla hajatofautiana na raisi Paul Kagame. Cheo chake ni Lutenanti General.
Akiulizwa na mwanahabari,kuhusu hali ya wakimbizi wa mwaka 1959 nchini Rwanda, iliyomsababishia(Kayumba) kuzaliwa nje ya nchi yake, aliulizwa, ni kipi anaona kinaweza kusaidia kuleta amani katika ukanda wa DRC,RWanda na Burundi.
Kayumba: Nadhani, njia sahihi na ya kipekee kufikia muafaka wa jambo hili la mashariki mwa DRC, ni mazungumzo tu. Lakini, si kwa Congo tu, pia kwa ukanda wote. Ukiangalia tatizo la Congo, ambapo Rwanda imekuwa ikishiriki huo mgogoro kwa zaidi ya miaka 30. Kuanzia mwaka 1996, Rwanda ilikuwa vitani nchini Congo.
Kwenye utawala wa Mobutu, utawala wa Desire Kabila, utawala wa Joseph Kabila, na sasa kwenye utawala wa Tshisekedi.
Tuliwahi pia kuwa na mahusiano mabaya sana na nchi ya Uganda: kuna vita baina ya Rwanda na Uganda huko Kisangani(Nchini DRC. Vinaweza kuongelewa hapo badae kama hiyo threat itakuwa na umhimu), kufungwa kwa mipaka, na mambo mengine kama hayo. Mahusiano yetu na Tanzania, pia kuna kipindi hayakuwa mazuri.
Mwaka 2013, Rais Kikwete na Rais Kagame walipotofautiana. Upande wa Burundi, kuanzia 2015, Rwanda na burundi hawaangaliani kwa jicho la amani. Kwa sasa hivi tunaongelea vita nchini Congo. Lakini pia,kuna uwezekano kukatokea jambo lolote pia huko Burundi. Hata jana, raisi wa Burundi, alitangaza kwamba amejiandaa vita na Rwanda.
Ngoja tuongelee watusti huko Congo kuhatalishiwa maisha. Hilo jambo ni kweli.
Watu huongelea mauaji ya kimbali nchini Rwanda, dhidi ya watutsi. Ni kweli yalitokea.
Lakini, kama unataka kutatua tatizo la ukanda, huwezi kukomboa watusti, kwa kuanzisha vita kwa watu wengine, kutafuta suruhu la watutsi, haimaanishi unatafuta suruhu la kuzuia genocide.
Tukiangalia DRC, tunaongelea watutsi zaidi ya laki 5, waliokimbilia Rwanda.
Je, ni mamilioni mangapi ya makabila mengine(Balega, Bahunde, Bahutu in Congo,Banande, hawa wote wamekuwa wakikimbia miaka yote hiyo 30.
Leo hii ukisema unaenda kuanzisha vita dhidi ya FDLR, hivi vita vinaenda kuwaondoa watu katika makazi yao. Kwangu, hilo siyo suruhisho.
Suruhisho ni kwamba, kwa serikali ya Congo, inatakiwa ikae meza ya mazungumzo na M23. Rwanda pia, inatakiwa iongee na wapinzani wake. Kwa sababu Rwanda inao wengi. Huu ukanda tu,iwe Afrika kusini, iwe Malawi, Zimbabwe,Mozambique wakimbizi karibia wote ni wanyarwanda. Lakini,serikali ya Rwanda, inalichukulia kama hakuna lolote lililotokea. Ongezea na wengine wote waliokimbia nchi, na kwenda ugaibuni. Ni kwamba wanahofia usalama wao. Sasa, kama hao ndo wanaoifadhili FDLR, kwa nini waifadhili?
Leo hii, hata ukiondoa tatizo la M23, wakimbizi wa Rwanda wataendelea kuwepo. Watakuwa kila kona.
Inaendelea................................................................