Sehemu ya II
Anaongea Kayumba : Huwezi ukasema kwamba, kwa sababu nimemaliza tatizo la M23, baaaasi. Kazi imeisha. La hasha. Tatizo bado litakuwa FDLR. Je, suruhisho ni lipi? Liquidate, eliminate. Maana yake ni nini!!! Ni kuwaua tu.
Unawezaje kuuwa raia wa taifa? Tukirudi kwenye swala la jenoside, nilikuwepo. Na mimi nilisaidia kuhakikisha mauaji hayo yanakomeshwa. Na mimi, ni mtutsi; hii ishu naiongelea kama mtu ninaeielewa. Toka kipindi hicho mpaka leo, Rwanda haijawahi kukaa na kuzungumza na hao watu walioshindwa.
Mwanahabari: tukiwa bado hapo kwenye swala la FDLR. KAtika mapigano ya Sake,waziri wetu wa ulinzi na mkuu wa majeshi, walisema kulikuwa na majibizano ya makombola kati ya DRC na Rwanda,ambapo DRC ilirusha makombola nchini Rwanda, na Rwanda ikajibu mapigo. Je, na wewe maoni yako, ni kwamba FDLR, ipo nchini Congo, na inaungwa mkono na raisi Tshisekedi?
KAYUMBA: Siwezi kusema kwamba Rwanda haitakiwi kujishughulisha na FDLR. Taifa lolote lenye makundi ya waasi wanaotumia silaha za moto, nchi hiyo lazina iwajibike. Lakini, unamaliza mzozo vipi? Ni kukaa na watu hao na kutafuta suruhisho. Labda niongezee kitu: Tulikuwa na uchaguzi Rwanda. Raisi, akajipatia kula asilimia 99.9; na umekuwa madarakani kwa muda wa miaka 30. Hata Mandela, nadhani kama angekuwa hai, sidhani kama hizo asilimia angepata kwa kuchaguliwa. Hii, inakupa picha halisi kwa nini watu hawa wanakuwa wapinzani wa serikali ya Rwanda.
Nikisema tatizo la wakimbizi, usifikilie tu watu wa FDLR waliopo nchini Congo. Kuna haya mataifa mengine niliyokutajia, ikiwemo Malawi, Mozambique, Zimbabwe, Zambia, Ulaya, kila kona. Halafu pia, kuna hawa manusura wa mauaji ya 1994 dhidi ya watutsi. Wapo kama mimi, niliepigania uwepo wa serikali iliyopo madarakani leo hii. Sasa basi, haya yote usipoyaangalia, ukasema tu unaenda kuongelea swala la M23, ni sawa na hujafanya chochote, unatatua tatizo nusu tu.
Shida nyingine, ni kwamba unatatuaje tatizo la ukanda! Kati ya Rwanda na mataifa mengine!!! Kama Burundi inasema yaliyopo kwa sasa, kama unafunga mipaka na Uganda. Kinachotokea ni nini! Labda, vita vinaenda kuhama kutoka DRC kuelekea Burundi. Na hapa tunapoongea, M23 karibia inaingia na Bukavu. Ikishafika Bukavu, ina maana tupo Kivu kusini, na mwambao wa Rusizi. Ukishakuwa katika mwambao huo, ndipo M23 itaungana na RED-TABARA. Kinachotokea, kilichopo Kivu kasikazini, ndo kitakachokuwa Kivu kusini.
Hapa ni wazi kwamba tatizo ni uongozi. Tunapoongelea nia ya kisiasa, tusimuangalie tu Tshisekedi. Kwa nini tusione na nia ya kisiasa ya raisi Kagame! Vyote ni sawa tu. Usihisi kwamba matatizo yaliyopo Congo, yanatofautiana na yaliyopo Rwanda. Ukija kuangalia, utagundua kwamba idadi ya wakimbizi wa DRC,haitofautiani na idadi ya wakimbizi wa Rwanda. Au pengine wa Rwanda wakawazidi idadi wa DRC.
Mwanahabari: Ni wiki sasa, jeshi la South Africa, limepoteza wanajeshi 14 huko Sake, katika vita na M23. Kwa mtazamo wako, ni nini kimeipa nguvu M23, kuweza kuwa na silaha za kisasa, na kuhimili kwa mta mrefu vita, na kupigana kwa wakati mmoja zaidi ya eneo moja?
KAYUMBA: Hili jambo lipe uhalisia wake: Mwaka 2020 na 2023, raisi Tshisekedi, aliingia makubaliano na raisi Museveni wa Uganda, wa kupeleka jeshi lake nchini Congo, na ujenzi wa barabara kutoka Uganda kwenda DRC ukafanyika.
Alikubaliana pia na Burundi,kupeleka jeshi lake Kivu kaskazini. Rwanda, haikupewa chance hiyo. Rwanda, ilikasirika. Na Raisi Kagame akasema, sijaalikwa nchini DRC, mi ntakwenda bila kualikwa. na aliposema tutaenda huko bila kualikwa, ndipo M23 ilipoanza mambo yake.
Hii kauli kwamba DRC haijawa na uungwana, ni uongo mtupu. Nakupa mfano: Kwenye uongozi wa Kabila, Rwanda iliruhusiwa kuingia nchini DRC kuitafuta FDLR.
Kuna kipindi ilifanyika oparesheni ijulikanayo kama umoja wetu. Watu wengi sana waliuliwa, wengine wakaimbia makazi yao. Mashirika ya kitaifa yalilalamika sana.
Mwaka 2019, raisi Tshisekedi, aliruhusu uongozi wa Rwanda kwenda DRC na kuuwa viongozi wa FDLR. Na waliwaua.
Hivi kweli, Rwanda inahitaji iruhusiwe mara ngapi kwenda Congo!
Zingatia: kuna kipindi, mkuu wa jeshi la Congo alikuwa mnyarwanda. Miaka! Walifanya nini? Leo hii eti wanataka kuingia Congo! Ngoja nikwambie kitu. FDLR ni kweli ipo. Na madai yake, yana mashiko. Kuwatakia uhuru kabila la watutsi, ni halali. Lakini, inakuwaje utafute amani ya kabila moja, makabila mengine uyaangamize?
Mwanahabari: Kwa haya yanayoendelea, unadhani ni nani anastahili kuwajibishwa matatizo haya yamayoleta mpaka vifo? Pia, umoja wa mataifa, umekuwa ukidai kwamba M23 inaungwa mkonono na serikali ya Rwanda. Je, kuna chochote unachoelewa kuhu hili?
KAYUMBA: Ahhhh, najua sana. Siyo kundi la kwanza tulilounga mkono. Ni kitu kilicho wazi. Hata sielewi kwa nini watu wanafichaficha. Unaona, Rwanda ndo iliweka kikomo kwenye utawala wa Mobutu. Mwaka 1996, tulipofuata wakimbizi na kuwarudisha kwao. Na hilo ndo lilikuwa lengo kubwa. Lakini, baada ya kukamilisha, tulitakiwa tubadili namna ya kuongoza nchi. Rwanda ilitakiwa kuongea na DRC kuhusu namna ya kuishi kwa amani na utulivu. Jambo la pili, ni upotoshaji. Kwamba M23 ni wanyamlenge. Issue ya Banyamulenge ilishaisha kitambo sana. Miaka ya 2002. Tena naweza kusema mwaka 1998, General James Kabarebe alipoondoka Kinshasa (Ndo alikuwa mkuu wa jeshi la DRC).
Kipindi cha utawala wa Kabila, Azarias Ruberwa, alikuwa makamu wa raisi. Ni mnyamulenge. Nyarugabo, alikuwa naibu spika, General Marick, arikuwa naibu kamanda wa jeshi, Bisengimana, ndo alikuwa mkuu wa Polisi. Ni wengi. Mpaka leo, kuna wanyamulenge wengi wenye vyeo kwenye ngazi za usalama. Na Generali Masunzu, hivi karibuni aliepewa kuwa mkuu wa jeshi wa kanda, ni mnyamulenge. HAta mawaziri, wapo wanyamurenge. Waziri wa miundombinu, ni mnyamulenge. Kwa hiyo, huku South Afrika, wakiongelea wanyamulenge, ni upotoshaji tu. Si kweli.
Issue ya wanyamulenge na M23, ni vitu viwili tofauti. Sema tu watu hawaelewi.
Itaendelea...................................................................................