Kazi gani ya nyumbani huipendi kabisa kuifanya?

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,455
Reaction score
5,134
Nyumbani kuna kazi nyingi sana zinazotumia muda mwingi na haziishi zinajirudia rudia kama kupika, kusafisha nyumba, kuosha vyombo nk.

Kati ya kazi hizo mie sipendi kabisa kufuta vyombo na kupanga kabatini nafanya kwa sababu nalazimika ila kungekuwa na mtu wa kuwa anapanga mie naosha tu namaliza anafuta na kupanga ingekuwa poa sana, naichukia sana hii kazi.

Wewe hupendi kufanya kazi gani hapo nyumbani kwako.
 
Huwa nina kawaida ya kumsaidia bibienu kupika hasa weekend. Kuna msosi, huwa anaupenda sana nikimpikia

Baada ya hapo, Zoezi la kuosha vyombo, ndiyo jambo limenishinda kufanya

Nipo tayari kusingizia naumwa lakini sio kumsaidia kuosha vyombo πŸ™Œ
 

Sipendi Kufua πŸ˜–πŸ˜΅ ishukuriwe teknolojia ya mashine, ila bado kutoa tu hizo nguo na kuziweka kabatini sipendi πŸ™ˆ

 
Kupiga pasi kama hakuna mtu wa kufanya hivyo bora nivae nguo imejikunja,
Kuosha vyombo na kusafisha choo, nashukuru sana nina mtu muelewa na sio mvivu
 
Hili ni janga la dunia bila shaka mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…