SoC04 Kazi iendelee kwa kufanya kazi masaa ishirini na nne katika siku saba za wiki kwa kuukuza uchumi wa kila Mtanzania

Tanzania Tuitakayo competition threads

Mamshungulii

Senior Member
Joined
May 3, 2023
Posts
175
Reaction score
88
Yamkini tukiweza kuruhusu na kufungua sehemu nyingi za kiuchumi kufanya kazi usiku na mchana tutaongeza wigo kubwa la kuwapatia nafasi wasiokuwa na ajira kupata ajira.

Tukiachilia hivi karibuni baadhi ya mabasi yaliyoachiwa kufanya kazi ya usafirishaji wa abiria usiku na baadhi ya makampuni kuruhusiwa kufanya kazi kwa masaa 24. Tanzania sidhani kama imewahi kuwa na sera inayozungumzia ufanyaji wa kazi kwa masaa 24.

Ikitokea kuruhusiwa uwepo wa sera ya Uchumi huu wa ufanyaji kazi kwa masaa ishirini na nne tutajipatia motisha ya kodi,nguvu nafuu na ya kuaminika, nishati ya kutosha na msaada wa kifedha kwa biashara ambazo zitafanya kazi kwa masaa 24.

Kwa tutumia hii sera ,serikali ikishirikiana na taasisi binafsi kuanzisha viwanda vya kutosha na biashara ambazo zinaweza kufanya kazi kwa masaa 24.Huu Uchumi wa masaa 24 kimsingi ,unaweza kujikita na USINDIKAJI WA KILIMO,viwanda vya dawa,viwanda vya uzalishaji ,ujenzi ,viwanda vya uchimbaji,makampuni ya usafi wa mazingira na usimamizi wwa taka,makampuni ya burudani na starehe,shughuli za kidigitali,mchakato wa ufanyaji biashara kimtandao,huduma za kifedha,maduka ya jumla na rejareja, na huduma za usafirishaji.

Pia sehemu za asasi za kijamii ambazo zina wateja wengi wanaopaswa kupatiwa huduma na zenyewe zinapaswa kutumia sera hiyo kama vile bandari zote,ofisi za pasipoti na ofisi zile ambazo zitakuwa na ulazima kwa hekima na matakwa ya wananchi zitumie Uchumi wa masaa 24.

Uchumi wa masaa 24 utapaswa kutekelezwa kwa kuzingatia michepuo na afua zingine za kimaendeleo za nchi kama vile elimu na mafunzo ,huduma za kiafya, kilimo, upatikanaji wa nyumba nafuu kwa wafanya kazi na wananchi wasiojiweza,upatikanaji wa usafiri mzuri wa umma ,utoaji wa haki kwa ufanisi na kwa wakati,hayo ni baadhi tu ya matamanio ya andiko hili kuupeleka Uchumi wa Tanzania katika hatua ya juu zaidi ya kidunia .

Uchumi huu wa masaa 24 utajikita pia katika kukuza ujasiriamai na uvumbuzi hasahasa kwa vijana.Serikali ikipendezwa itaendelea kutoa ushirikiano kwa vijana kwa kuwapatia mitaji na rasilimali kwa wajasiriamali viijana kusudi waweze kuanzisha na kukuza biashara zao,hii ni pamoja na kuwapatia fedha,ujuzi,mafunzo na ukaribu katika kuwapatia soko la ndani na nje la bidhaa zao na badala yake kusaidia nchi kupunguza kwa kiasi kikubwa uingizwaji wa bidhaa za kutoka nje ya nchi na kuongeza mauzo ya nje ya nchi kwa kiasi kikubwa.
Uchumi wa saa 24 utapandisha thamani ya pesa ya nchi yetu ,utaongeza tuweze kubaki na ziada nyingi,utapunguza mfumuko wa bei na kiwano cha riba ,utaongeza fursa nyingi za ajira na kuongeza ubora wa maisha.

Uwezekano ni mkubwa kwa kipindi hiki kwa serikali kuongeza mazingira mazuri ya kuboresha amani na usalama ,ili kuweka urahisi wa utendaji kazi kwa wananchi wakati wote.

Kurahisisha upatikanaji wa umeme na kuwapatia watumiaji wa umeme mita za kisasa zinazoweza kutumia mitambo mikubwa ya uzalishaji kwa masaa 24 kwa lengo tu la kuongeza tija na uzalishaji.

Kwa Afrika nchini Kenya na Ghana wanatumia sera ya masaa 24,jiji la Sydney pia linatuma sera ya masaa 24,Wales nchin Australia pia wanatekeleza sera ya masaa 24 kwa uchache tu.KAZI INAYOENDELEA KWA UCHUMI WA MASAA 24 kama itatekelezwa nchini inaweza kuushona ipasavyo ufchumi huu wa Tanzania na unaweza kushonwa kiasi cha kumtosha yeyote atakayeitumia.

Ni kweli yapo makamuni yanayoitumia hii sera ya masaa 24 ,lakini hizi kampuni hazina msaada wamoja kwa moja kutoka kwa serikali,na kwasababu baadhi ya makampuni kuweza kufanya kazi kwa masaa 24 kunaonyesha kwamba hili suala hata kwa Tanzania kisera linawezekana,lina umuhimu sana na linaweza kuzalisha ajira endelevu nyingi sana kama litachukuliwa maanani ipasiwavyo kwa jitihada za kimakusudi zitakazofanywa na serkali.

Kwasasa,zaidi ya asilimia 70 ya vitu vinavyotumika Tanzania vingi tunavitoa nje,mbaya zaidi vingine malighafi zake zote zinazalishwa Tanzania ,zinapelekwa nje ya nchi tena zinaenda kuongezewa thamani na kurudishwa nchini (ni aibu sana)kwa mfano viungo vya chai au pilau,vitunguu saumu vingi vinalimwa Tanzania vinapelekwa kuuzwa kule na kurudishwa huku vikiwa vimesagwa na kuwekewa lebo ya Kenya.

Haitoshi tu kuishia hapo hata baadhi ya watu wanazalisha batiki au vikoi kwa kuweka lebo ya nchi nyingine na sio Tanzzania ili tu kuwauzia watanzania kwani wakisikia kimezalishwa au kutengenezwa na mtanzania wanapoteza Imani ya kutumia bidhaa hizo,tujifunze utamaduni wa kutengeneza vyakwetu ,tujifunze utamaduni wa kuvijali na kuthamini kazi za watanzania wenzetu,jasho letu,uzalendo wetu.

Kwamfano, mara nyingi inapotokea siku zza maadhimisho ya mwanamke wizara ya maendeleo ya jamii hujaribu kuhamasisha wajasiriamali wauze batiki na mara nyingi huwa hawaandaliwii mapema, katika uzalishaji huo,pendekezo ni kutafuta mbinu mbadala ya kuwachagua wajasiriamali hao na kuwawezesha na kuchagua sare moja ambayo itatengenezwa na wajasiriamali hao chipukizi na wizara kununua kwa wao wajasiriamali halafu kutuuzia wananchi ,kwa hivyo italeta tija zaidi.

Kuweka motisha kupitia sera ya kazi kwa saa 24 itapunguza kwa kiasi kikubwa gharama ya kufanya biashara na kuwezesha biashara kufanyika saa 24 na ushindani kiuchumi kuimarika kupitia uboreshwaji wa huduma kwa wateja na uzalishaji.

Itakuwa vyema sana kama wazo la watu kulipwa kwa masaa wanayofanya kazi litafanyiwa kazi hii italeta ari na weledi pia kuongeza uzalishaji kazini.

Pia itarahisisha mwenye ujuzi kufanya kazi sehemu zaidi ya moja na kukuza kipato chake binafsi.
 
Attachments

  • istockphoto-464983900-1024x1024.jpg
    istockphoto-464983900-1024x1024.jpg
    97.3 KB · Views: 7
  • Sydney-24-hour-Economy-Strategy.pdf
    Sydney-24-hour-Economy-Strategy.pdf
    3.4 MB · Views: 5
Upvote 3
Haitoshi tu kuishia hapo hata baadhi ya watu wanazalisha batiki au vikoi kwa kuweka lebo ya nchi nyingine na sio Tanzzania ili tu kuwauzia watanzania kwani wakisikia kimezalishwa au kutengenezwa na mtanzania wanapoteza Imani ya kutumia bidhaa hizo,tujifunze utamaduni wa kutengeneza vyakwetu ,tujifunze utamaduni wa kuvijali na kuthamini kazi za watanzania wenzetu,jasho letu,uzalendo wetu
 
Yamkini tukiweza kuruhusu na kufungua sehemu nyingi za kiuchumi kufanya kazi usiku na mchana tutaongeza wigo kubwa la kuwapatia nafasi wasiokuwa na ajira kupata ajira.

Tukiachilia hivi karibuni baadhi ya mabasi yaliyoachiwa kufanya kazi ya usafirishaji wa abiria usiku na baadhi ya makampuni kuruhusiwa kufanya kazi kwa masaa 24. Tanzania sidhani kama imewahi kuwa na sera inayozungumzia ufanyaji wa kazi kwa masaa 24.

Ikitokea kuruhusiwa uwepo wa sera ya Uchumi huu wa ufanyaji kazi kwa masaa ishirini na nne tutajipatia motisha ya kodi,nguvu nafuu na ya kuaminika, nishati ya kutosha na msaada wa kifedha kwa biashara ambazo zitafanya kazi kwa masaa 24.

Kwa tutumia hii sera ,serikali ikishirikiana na taasisi binafsi kuanzisha viwanda vya kutosha na biashara ambazo zinaweza kufanya kazi kwa masaa 24.Huu Uchumi wa masaa 24 kimsingi ,unaweza kujikita na USINDIKAJI WA KILIMO,viwanda vya dawa,viwanda vya uzalishaji ,ujenzi ,viwanda vya uchimbaji,makampuni ya usafi wa mazingira na usimamizi wwa taka,makampuni ya burudani na starehe,shughuli za kidigitali,mchakato wa ufanyaji biashara kimtandao,huduma za kifedha,maduka ya jumla na rejareja, na huduma za usafirishaji.

Pia sehemu za asasi za kijamii ambazo zina wateja wengi wanaopaswa kupatiwa huduma na zenyewe zinapaswa kutumia sera hiyo kama vile bandari zote,ofisi za pasipoti na ofisi zile ambazo zitakuwa na ulazima kwa hekima na matakwa ya wananchi zitumie Uchumi wa masaa 24.

Uchumi wa masaa 24 utapaswa kutekelezwa kwa kuzingatia michepuo na afua zingine za kimaendeleo za nchi kama vile elimu na mafunzo ,huduma za kiafya, kilimo, upatikanaji wa nyumba nafuu kwa wafanya kazi na wananchi wasiojiweza,upatikanaji wa usafiri mzuri wa umma ,utoaji wa haki kwa ufanisi na kwa wakati,hayo ni baadhi tu ya matamanio ya andiko hili kuupeleka Uchumi wa Tanzania katika hatua ya juu zaidi ya kidunia .

Uchumi huu wa masaa 24 utajikita pia katika kukuza ujasiriamai na uvumbuzi hasahasa kwa vijana.Serikali ikipendezwa itaendelea kutoa ushirikiano kwa vijana kwa kuwapatia mitaji na rasilimali kwa wajasiriamali viijana kusudi waweze kuanzisha na kukuza biashara zao,hii ni pamoja na kuwapatia fedha,ujuzi,mafunzo na ukaribu katika kuwapatia soko la ndani na nje la bidhaa zao na badala yake kusaidia nchi kupunguza kwa kiasi kikubwa uingizwaji wa bidhaa za kutoka nje ya nchi na kuongeza mauzo ya nje ya nchi kwa kiasi kikubwa.
Uchumi wa saa 24 utapandisha thamani ya pesa ya nchi yetu ,utaongeza tuweze kubaki na ziada nyingi,utapunguza mfumuko wa bei na kiwano cha riba ,utaongeza fursa nyingi za ajira na kuongeza ubora wa maisha.

Uwezekano ni mkubwa kwa kipindi hiki kwa serikali kuongeza mazingira mazuri ya kuboresha amani na usalama ,ili kuweka urahisi wa utendaji kazi kwa wananchi wakati wote.

Kurahisisha upatikanaji wa umeme na kuwapatia watumiaji wa umeme mita za kisasa zinazoweza kutumia mitambo mikubwa ya uzalishaji kwa masaa 24 kwa lengo tu la kuongeza tija na uzalishaji.

Kwa Afrika nchini Kenya na Ghana wanatumia sera ya masaa 24,jiji la Sydney pia linatuma sera ya masaa 24,Wales nchin Australia pia wanatekeleza sera ya masaa 24 kwa uchache tu.KAZI INAYOENDELEA KWA UCHUMI WA MASAA 24 kama itatekelezwa nchini inaweza kuushona ipasavyo ufchumi huu wa Tanzania na unaweza kushonwa kiasi cha kumtosha yeyote atakayeitumia.

Ni kweli yapo makamuni yanayoitumia hii sera ya masaa 24 ,lakini hizi kampuni hazina msaada wamoja kwa moja kutoka kwa serikali,na kwasababu baadhi ya makampuni kuweza kufanya kazi kwa masaa 24 kunaonyesha kwamba hili suala hata kwa Tanzania kisera linawezekana,lina umuhimu sana na linaweza kuzalisha ajira endelevu nyingi sana kama litachukuliwa maanani ipasiwavyo kwa jitihada za kimakusudi zitakazofanywa na serkali.

Kwasasa,zaidi ya asilimia 70 ya vitu vinavyotumika Tanzania vingi tunavitoa nje,mbaya zaidi vingine malighafi zake zote zinazalishwa Tanzania ,zinapelekwa nje ya nchi tena zinaenda kuongezewa thamani na kurudishwa nchini (ni aibu sana)kwa mfano viungo vya chai au pilau,vitunguu saumu vingi vinalimwa Tanzania vinapelekwa kuuzwa kule na kurudishwa huku vikiwa vimesagwa na kuwekewa lebo ya Kenya.

Haitoshi tu kuishia hapo hata baadhi ya watu wanazalisha batiki au vikoi kwa kuweka lebo ya nchi nyingine na sio Tanzzania ili tu kuwauzia watanzania kwani wakisikia kimezalishwa au kutengenezwa na mtanzania wanapoteza Imani ya kutumia bidhaa hizo,tujifunze utamaduni wa kutengeneza vyakwetu ,tujifunze utamaduni wa kuvijali na kuthamini kazi za watanzania wenzetu,jasho letu,uzalendo wetu.

Kwamfano, mara nyingi inapotokea siku zza maadhimisho ya mwanamke wizara ya maendeleo ya jamii hujaribu kuhamasisha wajasiriamali wauze batiki na mara nyingi huwa hawaandaliwii mapema, katika uzalishaji huo,pendekezo ni kutafuta mbinu mbadala ya kuwachagua wajasiriamali hao na kuwawezesha na kuchagua sare moja ambayo itatengenezwa na wajasiriamali hao chipukizi na wizara kununua kwa wao wajasiriamali halafu kutuuzia wananchi ,kwa hivyo italeta tija zaidi.

Kuweka motisha kupitia sera ya kazi kwa saa 24 itapunguza kwa kiasi kikubwa gharama ya kufanya biashara na kuwezesha biashara kufanyika saa 24 na ushindani kiuchumi kuimarika kupitia uboreshwaji wa huduma kwa wateja na uzalishaji.

Itakuwa vyema sana kama wazo la watu kulipwa kwa masaa wanayofanya kazi litafanyiwa kazi hii italeta ari na weledi pia kuongeza uzalishaji kazini.

Pia itarahisisha mwenye ujuzi kufanya kazi sehemu zaidi ya moja na kukuza kipato chake binafsi.
Mapumziko muhimu....afya ya akili na mapumziko ya ubongo n muhimu.
 
Back
Top Bottom