..mtoa mada ana hoja.
..lakini suala analolipinga limekuwepo kwa muda mrefu itakuwa ni vigumu kuachana nalo.
..kuna mambo mengi ya itifaki tunatakiwa tuachane nayo, na hili analoongelea mtoa mada ni mojawapo.
..kwa mfano, kuna utaratibu wa utitiri wa viongozi kuwepo uwanja wa ndege kumuaga na kumpokea Raisi anapokwenda na kutoka safari. Nadhani utamaduni huo unaweza kurekebishwa, na shughuli hiyo ikafanywa na watu wachache zaidi.
..hata hili la Raisi kuhutubia akiwa Dsm, sikuona ulazima wa VP na PM kuwepo hapo. Nadhani suala hili lingeshughulikiwa kama ziara ya Raisi mikoani ambapo huwa na mawaziri wachache na mkuu wa mkoa husika.
..Zaidi, hivi kulikuwa na ulazima wa kuwakusanya hao wazee na kuzungumza nao kwa niaba ya wazee wa nchi nzima? Kwanini Raisi asihutubie taifa zima kupitia LUNINGA?