Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Kwema Wakuu!
Ikiwa kazi unayoifanya haijawahi kukuletea Polisi, au haijawahi kukupeleka kwenye vyombo vya kisheria ujue hiyo kazi haiwezi kukufanya kuwa Tajiri.
Utajiri na uvunjifu wa sheria ni pande mbili za sarafu moja.
Huwezi kuwa tajiri bila kuivunja sheria ya nchi, mahali popote Katika hii dunia.
Kazi yoyote yenye hatari za kukamatwa na Polisi kazi hiyo ujue inauwezo wa kukufanya uwe tajiri.
Kadiri unavyozidi kupata pesa ndivyo unavyoukaribia Mdomo wa Jela, hivyo ndio maana ni lazima ufanye Kolabo na Wakubwa ili kuyavunja Meno ya Jela ili hata siku ukiingiamo ndani yake jela haiwezi kukusaga saga.
Hiyo ni kanuni ya Kidunia.
Kanuni ya Afrika, pesa unaweza ukapata pasipo hata kutumia Uchawi au uganga Ila Inategemea na kiwango cha Pesa.
Milioni 5 sijui 10M mpaka milioni 100M hizo unaweza ukazipata Kwa nguvu zako mwenyewe hata pasipo kujiingiza kwenye Uchawi. Wala hata serikali isiwe na time na wewe.
Lakini kuna pesa ili uishike na kuilinda basi itakupasa Ujiingize kwenye Uchawi na uganga huko.
Ngumu Sana na nadra Sana mtu amiliki milioni Mia tano tuu bila ndumba hiyo ni ngumu Sana.
Najua kuna watu watanibishia, lakini huo ndio ukweli.
Kisheria na kihaki hakuna Logic ya mtu kuwa Tajiri wa mabilioni ya pesa pasipo kuvunja sheria tena Kwa makusudi kabisa, hakuna kitu Kama hicho.
Taikon leo amecheka baada ya kukutana na Bilionea mmoja huku Kahama, bilionea huyu nilimuuliza ni Kwa nini yeye ni Tajiri akanijibu; "Kwa sababu siogopi kuvunja sheria" Nikabaki namkodolea macho tu!
Nipumzike sasa!
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Kahama