Kazi isiyoangaliana na mlango wa Jela haiwezi kukufanya kuwa Tajiri

Kazi isiyoangaliana na mlango wa Jela haiwezi kukufanya kuwa Tajiri

Hii nadharia ya kuwapotosha watu huwezi fanikiwa au kuwa tajiri bila dawa ni nadharia iliyoua saikolojia ya waafrika Wengi sana na kuwafanya wazidi kutopea kwenye umasikini zaidi. Ndo maana ulaya waliua waganga na wachawi karibu wote Ili wasiwapotoshe watu kwa kuwaaminisha akili bandia, bali wapate kizazi kinachofikiri kwa kutegemea akili na sio miujiza. Ingekuwa hii nadharia ya kipumbavu inafanya kazi basi waafrika wengi 90% sana wangekuwa matajiri, maana ni asilimia kubwa Sana kutwa viguu na njia kwa waganga wakipeleka kuku but kwann still bado wengi maisha yanawachapa? Maana pana maeneo KILA baada ya watu watatu wa nne ni mganga, mchawi au mshirikina but dhoofu hali.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Usijidanganye Mkuu.

Alafu wenye akili hawanaga Utajiri[emoji3][emoji3]

Mtu akishakuwa na akili kamwe hawezi kuwa Tajiri labda akili ya kawaida lakini kama unamaanisha Akili nyingi basi utakuwa unakosea.

Kwa hapa Afrika hakuna Tajiri wa hivyo
Wenye akili alafu nimatajiri wapo serikalini asilimia kubwa zaid ni mafisadi
 
Huwezi kwenda jela kama unayo pesa labda wakikumate umevunja sheria then huna pesa. Mfano umedokoa pesa za umma jumla ya milioni 300 kidogo kidogo zikaishia kufungulia zipu na vizibo vya bia huna hata nyumba ya kuweka Dhamana Ili upate pesa ya kuwapa walinda sheria Ili kuununua UHURU wako. Kwa hizi nchi za kiafrica unaweza ukakamatwa na rushwa na ukatoa rushwa ukawa huru, sema labda ushindwe dau, mfano umekamatwa na rushwa ya milioni 1 wao wanataka milioni 5,we huna hapa ni lazima uende jela. Afrika mifumo ilishaoza tunaishi kwa system ya kila mtu umla mnyonge wa size yake.
 
Kwema Wakuu!

Ikiwa kazi unayoifanya haijawahi kukuletea Polisi, au haijawahi kukupeleka kwenye vyombo vya kisheria ujue hiyo kazi haiwezi kukufanya kuwa Tajiri.

Utajiri na uvunjifu wa sheria ni pande mbili za sarafu moja.
Huwezi kuwa tajiri bila kuivunja sheria ya nchi, mahali popote Katika hii dunia.

Kazi yoyote yenye hatari za kukamatwa na Polisi kazi hiyo ujue inauwezo wa kukufanya uwe tajiri.

Kadiri unavyozidi kupata pesa ndivyo unavyoukaribia Mdomo wa Jela, hivyo ndio maana ni lazima ufanye Kolabo na Wakubwa ili kuyavunja Meno ya Jela ili hata siku ukiingiamo ndani yake jela haiwezi kukusaga saga.

Hiyo ni kanuni ya Kidunia.

Kanuni ya Afrika, pesa unaweza ukapata pasipo hata kutumia Uchawi au uganga Ila Inategemea na kiwango cha Pesa.

Milioni 5 sijui 10M mpaka milioni 100M hizo unaweza ukazipata Kwa nguvu zako mwenyewe hata pasipo kujiingiza kwenye Uchawi. Wala hata serikali isiwe na time na wewe.

Lakini kuna pesa ili uishike na kuilinda basi itakupasa Ujiingize kwenye Uchawi na uganga huko.
Ngumu Sana na nadra Sana mtu amiliki milioni Mia tano tuu bila ndumba hiyo ni ngumu Sana.

Najua kuna watu watanibishia, lakini huo ndio ukweli.

Kisheria na kihaki hakuna Logic ya mtu kuwa Tajiri wa mabilioni ya pesa pasipo kuvunja sheria tena Kwa makusudi kabisa, hakuna kitu Kama hicho.

Taikon leo amecheka baada ya kukutana na Bilionea mmoja huku Kahama, bilionea huyu nilimuuliza ni Kwa nini yeye ni Tajiri akanijibu; "Kwa sababu siogopi kuvunja sheria" Nikabaki namkodolea macho tu!

Nipumzike sasa!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Kahama
Only if you a ZERO BRAIN!
Mtu mwenye akili iliyo sawasawa na aliyesoma na kueleimika, hawezi kuwaza upumbavu huu hata siku moja. Mfano hai upo kwamba Mh Dr. Reginald Mengi (RIP), hakuwahi kuwaza huu ujinga na hayupo Mtanzania hata mmoja hadi leo ambaye ameshavunja rekodi yake. Acha ku-impart watu wenye akili, mawazo ya kipumbavu. Unless mtu ni mpumbavu, then unachokiongea kinaweza ku-apply na ku-sound kwake
 
Jamaa aliiba mali ya tajiri, alipofikishwa mahakamani alicheza na sheria na kushinda kesi. Ikabidi tajiri amlipe jamaa mda wake aliopoteza. Alichoiba na alicholipwa sasa ni tajiri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwezi kwenda jela kama kwenu asili Hakuna mtu aliyewahi kwenda jela, jela ni roho inayofatilia, wafungwa ni wale wale yaani ni lazima huko nyuma katika familia yenu amewahi mtu kwenda jela, na ukienda jela ni lazima kizazi chako mtu ataenda jela.
Unaweza ukafanya tafiti.
Afrika jela ni kuzimu ndogo afrika nzima maisha ya jela ufanana.
 
Only if you a ZERO BRAIN!
Mtu mwenye akili iliyo sawasawa na aliyesoma na kueleimika, hawezi kuwaza upumbavu huu hata siku moja. Mfano hai upo kwamba Mh Dr. Reginald Mengi (RIP), hakuwahi kuwaza huu ujinga na hayupo Mtanzania hata mmoja hadi leo ambaye ameshavunja rekodi yake. Acha ku-impart watu wenye akili, mawazo ya kipumbavu. Unless mtu ni mpumbavu, then unachokiongea kinaweza ku-apply na ku-sound kwake

Ohooo!

Huwezi elewa nazungumzia kitu gani hata ungesoma mpaka upate PhD
 
Back
Top Bottom