Kazi isiyoangaliana na mlango wa Jela haiwezi kukufanya kuwa Tajiri

Kazi isiyoangaliana na mlango wa Jela haiwezi kukufanya kuwa Tajiri

Halafu matajiri mara nyingi ukichukua mali zao zote ukatoa madeni yao yote habakiwi na fedha za kushtua. Unakuta ana milioni mia au mia mbili kwa mwaka ila mzunguko wake ni bilioni za kutosha ambazo ni mikopo.
 
Dunia ipo vice versa ila haya yote uliyoandika 95% ni Mambo ya kiroho na 5% Physical realm..
Washirikina wanajua Sana haya Mambo siyo yakutumia miguvu na akili zako, bila Mungu wako hutoboi panene.
 
Katika kitu nakubaliana na wewe ni hapo kwenye tabia, asikwambie mtu tabia na utamaduni wa mtu ama familia na ndugu zake zina mchango mkubwa sana katika kufanya wafanikiwe ama wafeli.

Omba sana Mungu akupe tabia zinazolinda maendeleo yako na akuepushe na ndugu au watu wa karibu wenye mambo ya kukuangusha.
Katika Afrika yetu ya kusaidiana kindugu, unaweza jikuta unabeba majukumu kibao ambayo ni mzigo kwako kisa tu kuna ndugu ambao hawafanyi wapaswacho kufanya kwenye maisha yao.
Wanaita attitudes
 
Sekta ya madini bila uchawi inawezekana kabisa na b ni hela ya kawaida tu. Ukizijua siri za uchimbaji madini uhitaji mganga wala ushirikina na utajiri utaupata tena wa halali bila masharti
Hapo kwenye siri ndio uchawi wenyewe sasa
 
Hii nadharia ya kuwapotosha watu huwezi fanikiwa au kuwa tajiri bila dawa ni nadharia iliyoua saikolojia ya waafrika Wengi sana na kuwafanya wazidi kutopea kwenye umasikini zaidi. Ndo maana ulaya waliua waganga na wachawi karibu wote Ili wasiwapotoshe watu kwa kuwaaminisha akili bandia, bali wapate kizazi kinachofikiri kwa kutegemea akili na sio miujiza. Ingekuwa hii nadharia ya kipumbavu inafanya kazi basi waafrika wengi 90% sana wangekuwa matajiri, maana ni asilimia kubwa Sana kutwa viguu na njia kwa waganga wakipeleka kuku but kwann still bado wengi maisha yanawachapa? Maana pana maeneo KILA baada ya watu watatu wa nne ni mganga, mchawi au mshirikina but dhoofu hali.
Nafikili Tanzania napo wangeuwa waganga wote ili tusikwamishane mtu unalima hekari za kutosha unafanyiwa ndumba unavuna gunia kituko na mvua zilinyesha vizuri majirani mavuno safi mbolea uliweka kanuni ulifata ila mavuno sasa wasukuma tunaelewa namaanisha nini
 
Only a low IQ person thinks this way.
Angalia mfumo wa kukusanya kodi barani Africa background ya familia nyingi za kiafrica ubora wa elimu inayotolewa mashuleni mazingira wanayokulia vijana wengi wa kiafrica angalia viongozi wa kiafrica na mfumo mzima wa utawala utamuelewa mtoa mada
 
Only if you a ZERO BRAIN!
Mtu mwenye akili iliyo sawasawa na aliyesoma na kueleimika, hawezi kuwaza upumbavu huu hata siku moja. Mfano hai upo kwamba Mh Dr. Reginald Mengi (RIP), hakuwahi kuwaza huu ujinga na hayupo Mtanzania hata mmoja hadi leo ambaye ameshavunja rekodi yake. Acha ku-impart watu wenye akili, mawazo ya kipumbavu. Unless mtu ni mpumbavu, then unachokiongea kinaweza ku-apply na ku-sound kwake
Waliosoma na kuelimika ndio wanakimbizana kwenye ajira juzi zimetangazwa nafasi 17,412 wakaomba 165,948 sasa kama waliosoma na kuelimika ndio hawa huo utajiri tunaupataje kama kujiajiri tu imekuwa kipengele
 
Masikini siku zote ni watu wenye roho mbaya na wivu maana yake chochote kile utakachofanya ni lazima waumie na kuzusha maneno sasa usiombee uwe na uwezo mkubwa wa kifedha.

Wewe ni mmoja wapo mkuu.
Alichokisema kina leta maana regardless ni masikini au tajiri ni msomi au si msomi don't judge the person judge the content ,,ni wanasiasa wangapi bongo wanaiba billions of money maafisa wa TRA mawaziri wanafanya biashara haramu wanakwepa kodi na mambo chungu nzima (baadhi lakini)

mwisho wa Siku mtoto atarithi zile Mali ambazo upatikanaji wake una walakini atasifiwa na jamii na kuwa rolemodel wa vijana wenzie
 
Sekta ya madini bila uchawi inawezekana kabisa na b ni hela ya kawaida tu. Ukizijua siri za uchimbaji madini uhitaji mganga wala ushirikina na utajiri utaupata tena wa halali bila masharti
Mkuu sehemu iliyotawaliwa na uchawi sasa ni huko bila ramani za waganga utachimba miaka yako yote ya ujana na uzee hadi kifo hutaambulia mali kubwa ila pesa ya kula utapata but pesa ya utajiri sahau mzee
 
Embu tuanze na bilionaire wa kwanza wa dunia wanaotambulika kisheria acha na hawa wamadawa ya kulevya,mfano elon musk,bill gates,bezos wao utajiri wao umeanzaje?wamevunja sheria zipi?
 
Acha sound mkuu.... Sasa wewe si uwe mchawi upate hizo billion.....
 
Back
Top Bottom