Kazi isiyoangaliana na mlango wa Jela haiwezi kukufanya kuwa Tajiri

Kazi isiyoangaliana na mlango wa Jela haiwezi kukufanya kuwa Tajiri

Only if you a ZERO BRAIN!
Mtu mwenye akili iliyo sawasawa na aliyesoma na kueleimika, hawezi kuwaza upumbavu huu hata siku moja. Mfano hai upo kwamba Mh Dr. Reginald Mengi (RIP), hakuwahi kuwaza huu ujinga na hayupo Mtanzania hata mmoja hadi leo ambaye ameshavunja rekodi yake. Acha ku-impart watu wenye akili, mawazo ya kipumbavu. Unless mtu ni mpumbavu, then unachokiongea kinaweza ku-apply na ku-sound kwake
Mfatilie vizuri huyu jamaa utagundua kuna pesa flan hivi alizipiga ndio zikampa breakthrough ya utajiri
 
Uzi uko shallow, ume base kwenye hisia kuliko uhalisia. Aidha, unapeleka imani hasi na kufikirisha kwamba jinai ndiyo njia hakika ya kùfikia utajiri.

SAHIHiSHO
Utajiri unaletwa na ubunifu na kufanya kazi kwa bidii:

Katika kundi la matajiri 10 duniani wameupata utajiri kutokana na kazi zao za kibunifu

1, Elon Musk (Tesla);
2. Bill Gates (Microsoft );
3. Etc

Tumeshuhudia ata hapa kwetu vijana wabunifu wakitusua kama akina Joseph Kusaga, Diamond Platinums na wengine.

Jinai hailipi, usiaminishe jamii vitu vya uongo
 
Kwema Wakuu!

Ikiwa kazi unayoifanya haijawahi kukuletea Polisi, au haijawahi kukupeleka kwenye vyombo vya kisheria ujue hiyo kazi haiwezi kukufanya kuwa Tajiri.

Utajiri na uvunjifu wa sheria ni pande mbili za sarafu moja.
Huwezi kuwa tajiri bila kuivunja sheria ya nchi, mahali popote Katika hii dunia.

Kazi yoyote yenye hatari za kukamatwa na Polisi kazi hiyo ujue inauwezo wa kukufanya uwe tajiri.

Kadiri unavyozidi kupata pesa ndivyo unavyoukaribia Mdomo wa Jela, hivyo ndio maana ni lazima ufanye Kolabo na Wakubwa ili kuyavunja Meno ya Jela ili hata siku ukiingiamo ndani yake jela haiwezi kukusaga saga.

Hiyo ni kanuni ya Kidunia.

Kanuni ya Afrika, pesa unaweza ukapata pasipo hata kutumia Uchawi au uganga Ila Inategemea na kiwango cha Pesa.

Milioni 5 sijui 10M mpaka milioni 100M hizo unaweza ukazipata Kwa nguvu zako mwenyewe hata pasipo kujiingiza kwenye Uchawi. Wala hata serikali isiwe na time na wewe.

Lakini kuna pesa ili uishike na kuilinda basi itakupasa Ujiingize kwenye Uchawi na uganga huko.
Ngumu Sana na nadra Sana mtu amiliki milioni Mia tano tuu bila ndumba hiyo ni ngumu Sana.

Najua kuna watu watanibishia, lakini huo ndio ukweli.

Kisheria na kihaki hakuna Logic ya mtu kuwa Tajiri wa mabilioni ya pesa pasipo kuvunja sheria tena Kwa makusudi kabisa, hakuna kitu Kama hicho.

Taikon leo amecheka baada ya kukutana na Bilionea mmoja huku Kahama, bilionea huyu nilimuuliza ni Kwa nini yeye ni Tajiri akanijibu; "Kwa sababu siogopi kuvunja sheria" Nikabaki namkodolea macho tu!

Nipumzike sasa!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Kahama
Nadiriki kusema kuwa bichwa lako la habari ni ujinga wa hali ya juu.

Hizo ni fikra zanfailures.

Were ni katikabhawa: Maongezi vijana wa Tanzania; 96% ni pumba
 
Siku ukiingia kwenye sekta ya michezo hasa mpira wa hapa bongo utajua ni Kwa kiwango gani Watanzania ni washirikina..

Nilikuwa pale Morogoro, vitiku tuu vya mchangani, kwenye kombe la Mbuzi au kushidania milioni moja, huwezi amini timu zinaenda Kwa Waganga wa kienyeji.

Wadau wa mpira watakuja kukueleza,
Sasa hiyo ina relate vipi na kuingia jela ?
 
Uzi uko shallow, ume base kwenye hisia kuliko uhalisia. Aidha, unapeleka imani hasi na kufikirisha kwamba jinai ndiyo njia hakika ya kùfikia utajiri.

SAHIHiSHO
Utajiri unaletwa na ubunifu na kufanya kazi kwa bidii:

Katika kundi la matajiri 10 duniani wameupata utajiri kutokana na kazi zao za kibunifu

1, Elon Musk (Tesla);
2. Bill Gates (Microsoft );
3. Etc

Tumeshuhudia ata hapa kwetu vijana wabunifu wakitusua kama akina Joseph Kusaga, Diamond Platinums na wengine.

Jinai hailipi, usiaminishe jamii vitu vya uongo
Kukwepa kodi ni jinai au sio jinai?
 
Watu wengine wanaokamatwa sana na polisi ni wachezasha Play Station.
Wauza gongo, wawindaji haramu kwa ajili ya nyama (si wale wa pembe za ndovu na faru). Kutwa kucha wako police utajiri wao hatuuoni.
 
Mkuu napingana na wewe, huyu jamaa unaona hizo account zake?

inasoma USD178K sawa na tsh milioni 409. Account ya pili inasoma 186USD sawa na tsh million 427 jumla unapata million 836. Hapa unasemaje mkuu??View attachment 2289032View attachment 2289040
Tapeli huyo kijana.. Uwe na 800ml ukae chumba cha kupanga Kimara. Tumieni akili ndio maana anawatapeli pesa zenu
 
Halafu matajiri mara nyingi ukichukua mali zao zote ukatoa madeni yao yote habakiwi na fedha za kushtua. Unakuta ana milioni mia au mia mbili kwa mwaka ila mzunguko wake ni bilioni za kutosha ambazo ni mikopo.
Ndivyo ilivyo mkuu, ili upate million 200 lazima ufanye biashara ya billions. Kwahiyo hapo usishangae chochote
 
Mzee wa fasihi unaweza ukamiliki pesa nyingi bila ndumba mfano fanya biashara ya real estate jiingize biashara za kuuza viwanja utapata b za kutosha, panda miti eka 20 au zaidi baada ya miaka 12 utapata b za kutosha.
Hujui miti huwa yaungua?
 
Binafsi naamini maisha mazuri kila mtu akifanya juhudi kubwa anaweza kuyafikia. Lakini utajiri una namna kuu tatu:
  1. Kuurithi: Mfano Manji, Mo Dewji n.k yaani unakuta kila kitu kimeandaliwa (Mfumo) wewe kazi yako ni kuteleza!!!.
  2. Bahati: Mfano umechimba dhahabu,almasi,Tanzanite, umecheza kamari ukabahatika, umeenda kufanya tukio kubwa la ujambazi ukafanikiwa n.k
  3. Kipaji: Mfano wanamichezo,wanamuziki,wacheza filamu,waandishi wa vitabu n.k .Hii kwa nchi yetu ndiyo imeanza kuchukua nafasi ingawaje siyo kwa kiasi kikubwa kama kwa wale wa dunia ya kwanza.
Nb:Vitu vitakavyo kufanya utajirike ni siasa na biashara. Ni mtazamo.
MO hajarithi maana Wazazi wake wapo hai
 
Back
Top Bottom