Kazi isiyoangaliana na mlango wa Jela haiwezi kukufanya kuwa Tajiri

Kazi isiyoangaliana na mlango wa Jela haiwezi kukufanya kuwa Tajiri

Ulipoingiza habar za uchawi na uganga ndipo ulipokosea... Huko kwengine umesema ukweli...
 
ROBERT HERIEL ni ngumu Mtanzania wa leo ambaye Kama hakusoma saint kayumba basi kasoma saint Marie na huko kote aliambiwa ukimaliza kusoma unahitaji kuwa nani ? Leo umueleze haya akuelewe ila ni ukweli mchungu sana tena sana ila tunaendelea kulitafuta lango la jela iwe ukonga, keko , songwe au isanga kikubwa utajiri hata tukienda kuzilia jela sawa tu [emoji120][emoji120]
 
Taikoni wa fasihi karibu nyumbani ushirombo-
 
Msuva ana bilioni moja na kaipata hapa hapa Africa. Haya hilo wasemaje?
Msuva ni mpambanaji Sana ,big up kwake huyu mwamba.kuna siku nilipita check point moja nikiwa naenda dar frm Dom,nikakuta watu wa misitu wameikamata Lori lake likiwa na shehena ya gunia za ubuyu.jamaa anatafuta pesa kwa Hali na mali.big up Sana mwamba.
 
Binafsi naamini maisha mazuri kila mtu akifanya juhudi kubwa anaweza kuyafikia. Lakini utajiri una namna kuu tatu:
  1. Kuurithi: Mfano Manji, Mo Dewji n.k yaani unakuta kila kitu kimeandaliwa (Mfumo) wewe kazi yako ni kuteleza!!!.
  2. Bahati: Mfano umechimba dhahabu,almasi,Tanzanite, umecheza kamari ukabahatika, umeenda kufanya tukio kubwa la ujambazi ukafanikiwa n.k
  3. Kipaji: Mfano wanamichezo,wanamuziki,wacheza filamu,waandishi wa vitabu n.k .Hii kwa nchi yetu ndiyo imeanza kuchukua nafasi ingawaje siyo kwa kiasi kikubwa kama kwa wale wa dunia ya kwanza.
Nb:Vitu vitakavyo kufanya utajirike ni siasa na biashara. Ni mtazamo.
 
Wanasiasa ndio watu wanaomiliki Mali nyingi zizizo halali.

Kwa mfano Kama kwetu Kenya Kuna mwanasiasa mmoja maarufu ambaye utajiri wake unasemekana kuwa bilioni 35 za kikenya.

Aisee huyu mwamba ni mkatili Sana maana Ana skendo nyingi Sana za wizi wa Mali za serikali na kunyang'anya wanyonge mashamba yao.

Nikitaja skendo za huyo jamaa mnaweza mkashangaa Sana ila acha niishie Hapa tu Ila inauma Sana Yaani😥
Arap mashamba sio?
 
Kwema Wakuu!

Ikiwa kazi unayoifanya haijawahi kukuletea Polisi, au haijawahi kukupeleka kwenye vyombo vya kisheria ujue hiyo kazi haiwezi kukufanya kuwa Tajiri.

Utajiri na uvunjifu wa sheria ni pande mbili za sarafu moja.
Huwezi kuwa tajiri bila kuivunja sheria ya nchi, mahali popote Katika hii dunia.

Kazi yoyote yenye hatari za kukamatwa na Polisi kazi hiyo ujue inauwezo wa kukufanya uwe tajiri.

Kadiri unavyozidi kupata pesa ndivyo unavyoukaribia Mdomo wa Jela, hivyo ndio maana ni lazima ufanye Kolabo na Wakubwa ili kuyavunja Meno ya Jela ili hata siku ukiingiamo ndani yake jela haiwezi kukusaga saga.

Hiyo ni kanuni ya Kidunia.

Kanuni ya Afrika, pesa unaweza ukapata pasipo hata kutumia Uchawi au uganga Ila Inategemea na kiwango cha Pesa.

Milioni 5 sijui 10M mpaka milioni 100M hizo unaweza ukazipata Kwa nguvu zako mwenyewe hata pasipo kujiingiza kwenye Uchawi. Wala hata serikali isiwe na time na wewe.

Lakini kuna pesa ili uishike na kuilinda basi itakupasa Ujiingize kwenye Uchawi na uganga huko.
Ngumu Sana na nadra Sana mtu amiliki milioni Mia tano tuu bila ndumba hiyo ni ngumu Sana.

Najua kuna watu watanibishia, lakini huo ndio ukweli.

Kisheria na kihaki hakuna Logic ya mtu kuwa Tajiri wa mabilioni ya pesa pasipo kuvunja sheria tena Kwa makusudi kabisa, hakuna kitu Kama hicho.

Taikon leo amecheka baada ya kukutana na Bilionea mmoja huku Kahama, bilionea huyu nilimuuliza ni Kwa nini yeye ni Tajiri akanijibu; "Kwa sababu siogopi kuvunja sheria" Nikabaki namkodolea macho tu!

Nipumzike sasa!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Kahama
Taikon nahis hukumuekewa vizuri,zaidi ungemuomba afafanue.
Kuvunja sheria ni suala pana.
Je,yeye huvunja sheria zepi?
Zipo za asili,binafsi,za shule,kampuni,za nchi,za dini!
So waweza vunja shrmeria na bado usifanikiwe kwa maana hukujua ni sheria zipi uvunje!
Nashauri wewe(kumbuka unajina sasa ndani ya JF) ulitakiwa umalizie kwa caution... mfano1"at ur own risk" AU "Makinika"
 
Mkuu napingana na wewe, huyu jamaa unaona hizo account zake?

inasoma USD178K sawa na tsh milioni 409. Account ya pili inasoma 186USD sawa na tsh million 427 jumla unapata million 836. Hapa unasemaje mkuu??
Screenshot_20220713-170550.jpg
Screenshot_20220713-171150.jpg
 
Taikon nahis hukumuekewa vizuri,zaidi ungemuomba afafanue.
Kuvunja sheria ni suala pana.
Je,yeye huvunja sheria zepi?
Zipo za asili,binafsi,za shule,kampuni,za nchi,za dini!
So waweza vunja shrmeria na bado usifanikiwe kwa maana hukujua ni sheria zipi uvunje!
Nashauri wewe(kumbuka unajina sasa ndani ya JF) ulitakiwa umalizie kwa caution... mfano1"at ur own risk" AU "Makinika"

Nashukuru Sana Mkuu!

Matajiri na watu wazito hawapendi maswali na Wana sentesi fupifupi
 
Wanasiasa ndio watu wanaomiliki Mali nyingi zizizo halali.

Kwa mfano Kama kwetu Kenya Kuna mwanasiasa mmoja maarufu ambaye utajiri wake unasemekana kuwa bilioni 35 za kikenya.

Aisee huyu mwamba ni mkatili Sana maana Ana skendo nyingi Sana za wizi wa Mali za serikali na kunyang'anya wanyonge mashamba yao.

Nikitaja skendo za huyo jamaa mnaweza mkashangaa Sana ila acha niishie Hapa tu Ila inauma Sana Yaani😥
Masikini siku zote ni watu wenye roho mbaya na wivu maana yake chochote kile utakachofanya ni lazima waumie na kuzusha maneno sasa usiombee uwe na uwezo mkubwa wa kifedha.

Wewe ni mmoja wapo mkuu.
 
Only if you a ZERO BRAIN!
Mtu mwenye akili iliyo sawasawa na aliyesoma na kueleimika, hawezi kuwaza upumbavu huu hata siku moja. Mfano hai upo kwamba Mh Dr. Reginald Mengi (RIP), hakuwahi kuwaza huu ujinga na hayupo Mtanzania hata mmoja hadi leo ambaye ameshavunja rekodi yake. Acha ku-impart watu wenye akili, mawazo ya kipumbavu. Unless mtu ni mpumbavu, then unachokiongea kinaweza ku-apply na ku-sound kwake
Acha kuwaongelea watu,wewe unajua kaupataje utajiri,umefanya utafiti juu ya htimisho ulokuja nalo??
 
Nitavunja sheria zote ila siwezi kujiingiza katika uchawi wala kutoa uhai wa mtu
 
Utajiri unaanzia Tsh ngapi? Kuna mzee mmoja alikuwa na mkataba na kampuni ya USA awalimie aina fulani ya maharage kwa specs zao, wanampa kila kitu kuanzia planters sijui tractor na shamba linakatiwa insurance na kila msimu anapokea mamilioni ya kutosha kutoka USA. Huyo ni mkulima.

Kuna region internal auditor wa taasisi fulani ya fedha anasimamia nchi tatu mshahara wake kwa mwezi ni mamilioni ya kutosha...Huyo ni mhasibu.

Mifano ipo mingi sana ya kazi ambazo ni halali na zinalipa.... Hata ukiwa na kampuni ukabahatisha tenda moja na taasisi kubwa ya nje mwaka mzima inalipa vizuri na unakuwa tajiri.

Unless tafsiri ya utajiri kwako ni kubwa sana.
Au unaongelea utajiri ule wa kina bakresa?
 
Kwema Wakuu!

Ikiwa kazi unayoifanya haijawahi kukuletea Polisi, au haijawahi kukupeleka kwenye vyombo vya kisheria ujue hiyo kazi haiwezi kukufanya kuwa Tajiri.

Utajiri na uvunjifu wa sheria ni pande mbili za sarafu moja.
Huwezi kuwa tajiri bila kuivunja sheria ya nchi, mahali popote Katika hii dunia.

Kazi yoyote yenye hatari za kukamatwa na Polisi kazi hiyo ujue inauwezo wa kukufanya uwe tajiri.

Kadiri unavyozidi kupata pesa ndivyo unavyoukaribia Mdomo wa Jela, hivyo ndio maana ni lazima ufanye Kolabo na Wakubwa ili kuyavunja Meno ya Jela ili hata siku ukiingiamo ndani yake jela haiwezi kukusaga saga.

Hiyo ni kanuni ya Kidunia.

Kanuni ya Afrika, pesa unaweza ukapata pasipo hata kutumia Uchawi au uganga Ila Inategemea na kiwango cha Pesa.

Milioni 5 sijui 10M mpaka milioni 100M hizo unaweza ukazipata Kwa nguvu zako mwenyewe hata pasipo kujiingiza kwenye Uchawi. Wala hata serikali isiwe na time na wewe.

Lakini kuna pesa ili uishike na kuilinda basi itakupasa Ujiingize kwenye Uchawi na uganga huko.
Ngumu Sana na nadra Sana mtu amiliki milioni Mia tano tuu bila ndumba hiyo ni ngumu Sana.

Najua kuna watu watanibishia, lakini huo ndio ukweli.

Kisheria na kihaki hakuna Logic ya mtu kuwa Tajiri wa mabilioni ya pesa pasipo kuvunja sheria tena Kwa makusudi kabisa, hakuna kitu Kama hicho.

Taikon leo amecheka baada ya kukutana na Bilionea mmoja huku Kahama, bilionea huyu nilimuuliza ni Kwa nini yeye ni Tajiri akanijibu; "Kwa sababu siogopi kuvunja sheria" Nikabaki namkodolea macho tu!

Nipumzike sasa!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Kahama
Unakaribia na ukweli, kwamba ukifuatisha mifumo huwezi kuwa tajiri.
 
Back
Top Bottom