Kazi isiyoangaliana na mlango wa Jela haiwezi kukufanya kuwa Tajiri

Kazi isiyoangaliana na mlango wa Jela haiwezi kukufanya kuwa Tajiri

Msuva ana bilioni moja na kaipata hapa hapa Africa. Haya hilo wasemaje?
Hafanyi biashara hicho ni kipaji. Nadhani Taikon alitakiwa kuwa specific kwa upande wa biashara. Magendo,biashara hsramuvja vitu vya namna hiyo ni kweli utajiri ni njenje ila na polisi ni njenje. Kwasisi tuliozaliwa mazingira ya msgendo hizi mambo tunazielewa.
 
Hafanyi biashara hicho ni kipaji. Nadhani Taikon alitakiwa kuwa specific kwa upande wa biashara. Magendo,biashara hsramuvja vitu vya namna hiyo ni kweli utajiri ni njenje ila na polisi ni njenje. Kwasisi tuliozaliwa mazingira ya msgendo hizi mambo tunazielewa.
Umeeleweka
 
Kwema Wakuu!

Ikiwa kazi unayoifanya haijawahi kukuletea Polisi, au haijawahi kukupeleka kwenye vyombo vya kisheria ujue hiyo kazi haiwezi kukufanya kuwa Tajiri.

Utajiri na uvunjifu wa sheria ni pande mbili za sarafu moja.
Huwezi kuwa tajiri bila kuivunja sheria ya nchi, mahali popote Katika hii dunia.

Kazi yoyote yenye hatari za kukamatwa na Polisi kazi hiyo ujue inauwezo wa kukufanya uwe tajiri.

Kadiri unavyozidi kupata pesa ndivyo unavyoukaribia Mdomo wa Jela, hivyo ndio maana ni lazima ufanye Kolabo na Wakubwa ili kuyavunja Meno ya Jela ili hata siku ukiingiamo ndani yake jela haiwezi kukusaga saga.

Hiyo ni kanuni ya Kidunia.

Kanuni ya Afrika, pesa unaweza ukapata pasipo hata kutumia Uchawi au uganga Ila Inategemea na kiwango cha Pesa.

Milioni 5 sijui 10M mpaka milioni 100M hizo unaweza ukazipata Kwa nguvu zako mwenyewe hata pasipo kujiingiza kwenye Uchawi. Wala hata serikali isiwe na time na wewe.

Lakini kuna pesa ili uishike na kuilinda basi itakupasa Ujiingize kwenye Uchawi na uganga huko.
Ngumu Sana na nadra Sana mtu amiliki milioni Mia tano tuu bila ndumba hiyo ni ngumu Sana.

Najua kuna watu watanibishia, lakini huo ndio ukweli.

Kisheria na kihaki hakuna Logic ya mtu kuwa Tajiri wa mabilioni ya pesa pasipo kuvunja sheria tena Kwa makusudi kabisa, hakuna kitu Kama hicho.

Taikon leo amecheka baada ya kukutana na Bilionea mmoja huku Kahama, bilionea huyu nilimuuliza ni Kwa nini yeye ni Tajiri akanijibu; "Kwa sababu siogopi kuvunja sheria" Nikabaki namkodolea macho tu!

Nipumzike sasa!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Kahama


Hii fasihi yako kwangu mimi naiona haina mashiko kwasababu wingi au uchache wa pesa unapimwa na hisia na mazingira ya mtu husika ndani ya wakati fulani, mfano kuna mtu kulingana na hisia na mazingira yake kwa wakati huo ukimpa sh 10,000/= atakushukuru mno lakini hiyo hiyo pesa ukimpa mtu mwingine ni sawa kama umempa sh 500/= nk, hivyo hapo utaona pesa kwa mtu inategemea hisia, Mazingira na wakati, mfano wa wingi wa pesa kwa mtu ni sawa law of relativity katika physics.

--unasema Kwamba kuna njia mbili za kumuwezesha mtu kumiliki viwango tofauti vya pesa!!!--- mtu anaweza kumiliki pesa kiwango chochote katika njia hizo zote mbili sema tu kuna njia za haraka ya kupata pesa na zina hatari zake na kuna njia ngumu ya kupata pesa na nidhamu/masharti (disciplines/conditions) yake, mfano wa njia ya haraka ni kama utapeli, ujambazi wa kuvamia benki nk, njia hizi unapata pesa kwa haraka lakini ni njia ya hatari sana. Njia ngumu ni kama kufanya biashara nyingi zenye faida kidogo kidogo huku ukizingatia nidhamu ya matumizi ya mapato nk, point yangu ni hii; Uchache au wingi wa pesa ni hisia katika mazingira ndani wakati fulani ambamo mtu anapata au kumiliki pesa na upatikanaji wa viwango vya pesa havina kanuni maalumu mfano kwenda kwa waganga nk.
 
Uchawi hapana,

Nimeshikilia hapo kwenye kuvunja sheria tu [emoji110][emoji110]
 
Back
Top Bottom