Kazi nilizowahi zifanya na zikanishinda kwenye utafutaji

kuna ile stori ya jumaa ambae alisingizia ndugu yake kafarikiii sijui so akaruhusiwa kwenda kuzikaa mwenzio akapigika balaa walidhani wanaenda kuwa makarani kwenye godauni....
 
Unajua kwanini watu wanaachaga malipo na kuondoka kimya kimya?!

Ni kwasababu ukienda omba malipo utaonekana mzembe na hata kama bosi

akisema akupe atakupa huku akikusema (siku nyingine acheni kukimbilia kazi za wanaume) Ulikua unajijua mtoto wa mama ulikuja kufanya nini hapa?

yani kuna maneno flani utatamkiwa hadi unaweza juta kufata hayo malipo, Sasa kwakua wengi tushajua kifuatacho ni kitu gani, Huwa tunajikataaa kimya kimya.

Maboss wengine umwambie umeshindwa kazi anakulipisha hela ya vifaa alivyowanunulia,mfano mimi ile kazi ya kuchota mavi kwenye chemba Boss alienda nunua gloves,ndooo,Boots akatuletea akiamini ni majembe ya kazi..

Mimi yakanishinda nikakimbia,hivi boss kama huyu umfate umwambie nilipe hata kidogo unafkiri kifuatacho nini?

Mkuu kuna maboss hawapendi kubipiwa kabisa wako serious wanataka kuona matendo na utimize ulichosema utafanya,sasa wewe itikia unaweza halafu fanya yakushinde halafu kadai malipo uone boss atapokupeleka!

Mungu hakukosea kukuumba na miguu mkuu,misala kama hiyo unaikimbia tu Hela kitu gani mzee
[emoji28][emoji28][emoji28]

#MaendeleoHayanaChama
 
Kwanza huyo anaesema ukadai chako hamtakii mtu mema kuna kazi za kudai chako na zingine sepa tu. Unaweza dai chako wana wakakuweka mtu kati kuwa umekwamisha kazi kwann usiseme mapema. Binafsi nilisha dai changu sema ilikua tofali kujengea sasa ile kazi tulikua wasaidizi 2 na mafundi wawili. Mwanzo wa kazi jamaa niliekua nae tunasaidia akapandisha tofali 15 juu ile kushuka akasema nakuja naenda nunua sigara. Nikajua huyu harudi nnikamchana fundi oyaa huyu haridi ongeza mtu jamaa wakasema poa asipokuja wanaongeza. Nikapiga kazi wee mpka nikaona haji tena nikawaambia oya huyu ndio haji mazima. Wakasema poa anajenga mmoja mwingine nikomae nae. Aahh ajabu nae komaa nae anasimama nikamwambi yule wa juu namalizia nusu ya kazi hii hiyo nusu nyingine mtajua wenyewe na hela yangu ipo pale pale. Bwana wewe kwenye kulipana tulisumbuana sema walilipa maana wanajua kuwa makosa ni yao. Na wanajua nitakiwasha mno. Ila zile kazi kama mwoga usiende na kama mlaini acha utateseka
 
nakumbuka miaka 4 nyuma hapo Geita kuna ghorofa jirani na Lenny hotel juu kabisa tunaweka zege kwa ajili ya matenki ya maji,sasa shughuli ikaanza kijana wa watu nina siku 2 msosi kwangu dhahabu na mifuko simenti 10 inatakiwa kule juu dah! nakili nilihisi natoka roho mifuko 4 tu kwisha habari yangu. Uzuri foreman wetu alikuwa njema yule jamaa nilimwomba akanielewa tukaendelea na kazi nyingine riziki ikapatikana! Sitoweza sahau hiyo day
 
Kwenye maisha kuna mambo mengi sana watu wanapitia mpaka unamuona mtu ana biashara akikwambia mapito aliyopitia mpaka kufikia hapo "acha kabisa", (naongelea wapambanaji) wale wapewa mitaji na ndugu/wazazi hampo eneo hili.

Basi bana tutoke huko leo acha tucheke (kwa watao ona inachekesha) tuchangamshane, lakini zaidi tuelimishane na kujifunza mawili matatu, maana hata katika ujinga kuna vya kujifunza, elimu ipo kila mahali.

Katika maisha yangu bana mimi sikuwahi pewa mtaji wa kufanya chochote hadi kufika hapa nilipo, sio ndugu sio wazazi sio BIKO wala any jackpot bali ni akili na kuthubutu kwangu katika sehemu tofauti tofauti.

Leo nitasimulia baadhi ya kazi nilizo thubutu ila yakanishinda(maisha si mepesi asee). Yalinishinda na nilizikimbia bila kuaga wala kuongea kitu na muajiri wangu. Wakati naanza maisha niliambiwa na brother angu mmoja kauli yake hii "mdogo angu usije ukachagua kazi, fanya kila kazi ya halali unayoijua."

Huo usemi ulinikaa kichwani kila nilipotembea ulikua ukijirudia rudia kichwani mwangu, ila jamani acheni niwambie wahenga kuna misemo yao sio ya kuifatisha kabisa. Hebu acha nianze simulizi zangu hapa;

ULINZI
Nikiwa katika harakati za kutafuta kazi yakufanya nipate mtaji wakufanya kitu njiani kwenye nguzo ya umeme nikaona tangazo la kampuni ya ulinzi inatafuta vijana wa ulinzi. Kigezo cha elimu kilikua darasa la 7 tu, haina cha mdhamini zaidi ya pasport size zako. Kigezo kingine kilichonishawishi nikakamatika waliandika "hata kama hujapitia mafunzo ya mgambo wanakupokea."

Kampuni nyingi za ulinzi usipokua na mafunzo ya mgambo hawakupokei (hili nilishachunguza maana nilishakataliwa kampuni flani flani) kwa kukosa sifa hiyo tu. Basi baada ya kuona hizo vigezo zao nikaona hapa hapa ndio pakutokea, haina kurudi nyuma. Huwa nina utaratibu wa kutembea na pasport size kwenye wallet kila ninapoenda, basi kwakua kigezo kikubwa n pasport size na ninayo nikaona acha niende.

Kufika ofisi zao nikaingia nikajitambulisha nikahojiwa maswali kadhaa basi baada ya hapo wakaniuliza "upo tayari kuanza kazi lini?" Nikawajibu "yani hata sasa hivi" (hapo ndipo nilipojichanganya). Wakaniambia safi kabisa kijana, kaa pale subiri tukutaftie uniform.

Nikawa nimekaaa reception pale wakaingia store wakanletea sare, ila sare zilikua oversize yani kubwa mno kwangu na ilibidi nizivae pale pale. Basi sikua na ajizi nikazitupia mwilini kwakua zilikua kubwa sikua na haja ya kuvua nguo nilizokua nimezivaa. Nilivaa juu yake zile, viatu nilikua fresh tu (napenda vaa Timberlands) na uzuri hiyo siku nilikua na Black Tims chni hivyo kwenye upande wa viatu nilikua safi.

Baada yakukamilika kimavazi nikawa nimekaa pale kusubiri kupelekwa eneo la kazi. wakati tumekaa pale akaingia kiongozi wao nikaona watu wote wamesimama, kwakua namimi nishakua askari ikabidi nisimame kikakamavu kama askari. Ripoti ikatolewa idadi ya askari na mimi nikiwepo, kisha jamaa akapita tukakaa chini.

Mida ya saa 11 tukafatwa na gari nikapanda kwenye gari safari yakuanza sambazwa vituo vyetu vya kazi ikaanza. Basi nikapelekwa kwenye lindo langu, nikamkuta mwamba kapanda hewani kinoma. Basi kufika pale akanielekeza vyakulinda, akanikabidhi daftari la vitu vya kulinda na tukazunguka nae kuvihakiki kwamba vipo kisha tulipomaliza akaniambia yeye anasepa, tukaagana akaniacha.

Ilikua ni kama dispensary flani hivi kubwa kubwa, wanafunga saa mbili. Basi baada ya kufunga haoo wakaniaga wakaondoka, nikabaki peke yangu usiku huo.

Sijui ikawaje umeme ukakatika eneo hilo tu na nyumba za jirani ambazo nyingi ni ofisi tu za watu sio makazi ya watu kuishi, hivyo kuna ukimya mno. Giza likatawala, uoga ukaja, ukakolea. Kama dk 15 hivi kupita nikaskia watu wameruka ukuta wamedondokea kwandani, nikakimbia kujificha kwenye kistore flani, nikawa nachungulia.

Nikaona majamaa wawili wameingia wanachukua vyuma vyuma ambavyo ni 1 ya vitu niliambiwa nilinde, siwezi sema lolote nawaangalia mkojo umenibana, roho inadunda inataka kuchomoka. Ghafla nawaona wengine wawili wanatokea wakawa wanne ila hawa wawili walikua na nondo wamezishika na mwingine kashka kishoka.

Mkojo ukazidi kunibana nikawa naona hii leo ndio mwisho wangu, kupigana siwezi mimi hawa watu wote nawafanyaje? Hapo store kulikua na pipa nikadumbukia, ila kabla sijadumbukia nikawapigia kelele wajamaa nikawaambia "NYIE TOKENI HAPO" halafu nikadumbukia kwenye pipa nikajifunika.

Nikawasikia na wao wamekurupuka wamekimbia, nikawa nimekaa kwenye pipa kama dk 10, nilisikia ukimya umezidi nikatoka kimya kimya kiminyato. Kuchungulia kweli sioni mtu, palepale nikasema hapana, nitakufa mimi siwezi hii kazi. Nikavua nguo zao nikafungua geti nikapita na mishe zangu nikaondoka na kazi ikaishia hapo, hiyo ni saa nane usiku inaenda saa tisa huko.

KUNG'OA KISIKI
Nikiwa katika tafuta tafuta nikafika nyumba moja nikaomba kazi, akatoka mama mmoja akaniambia kuna kisiki cha kutoa, unaweza? Nikamwambia bila shaka nipate tu jembe, akasema vifaa vyote vipo je kazi nitaifanya kwa shilingi ngapi? Nikjisemea kimoyo moyo, yani najipangia mwenyewe malipo? Nikaropoka Nikamwambia Boss hii kazi nzito ukinipa 15,000 itanitosha.

Akasema sawa kijana ukikitoa vizuri ntakuongeza 15,000 nyingine, nikamwambia sawa bosi. Hapo nina mizuka kama yote,nikawa najisemea hapa nina 30k ya chap chap, kazi ikaanza.

Piga jembe, piga shoka natikisa kisiki kinaniangalia kama hamna nilichokifanya. Lima sana kwatua sana natingisha kisiki kinantolea macho tu. Boss anakuja anauliza maendeleo namwambia shaka ondoa hiki kinatoka chote utafurahia.

Akiondoka naanza kazi tena pga shoka kata mizizi lakini wapi, nilianza kazi saa nne asubuhi kufika saa tisa mchana kazi haielekei kuisha au kukamilika. Nikamwambia bosi nakuja naenda dukani fata vocha nimpigie mama mara moja home. Nilivyopita huko huko sikurudi nyuma, nikaona ntaja kufa mimi.

Duniani kuna visiki nyie acheni kabisa kuna miti ukiambiwa utoe kisiki chake hata upewe wiki unaweza usiweze kwa namna ardhi ilivyo ngumu. Mti una mizizi kama mkia wa pweza kuupata huo mzizi mkuu tu ni kazi ya masiku, ah nilikimbia mimi.

KUUZA LOTION NA VYOMBO VYA PLASTIKI
Kama kawaida niko zangu barabarani natembea sina hili wala lile nikaona tangazo wanatafutwa wafanyakazi, watu wa Sales and Marketing. Kigezo kikubwa uwe umefika chuo kwa level yoyote, uwe na vyeti vyako tu kuthibitisha elimu yako, Mshahara kuanzia 300,000 - 500,000. Nikaona yes hapahapa, nikachukua namba za simu nikarudi home kusanya vyeti vyangu, kesho yake asubuhi sana nikapiga simu nikiwa nimekamilika.

Nikaelekezwa ofisi zilipo, kufika pale tukaambiwa wale mliokuja na vyeti vyenu mtakua viongozi kwahiyo leo leo mtaanza kazi hii. Tukaelekezwa majukumu, ajabu nikaona tunaletewa mabeseni, ma lotion-lotion (yale wanayopaka wadada wa kazi). Kisha tukaambiwa viongozi nyie mtazunguka kutangaza hizi biashara za kampuni, kampuni ikishajulikana basi kazi rasmi ya mshahara wa 300k to 500k itaanza.

Kwasasa tutalipwa kulingana na mauzo ya siku, sisi viongozi tukapewa mzigo wetu na mabegi na lotion zetu kila kundi tulikua na mwenyeji mmoja aliekua anatutembeza huko mtaani. Basi bwana tukatoka pale na mabeseni yetu tukaingia mtaani kila kikundi tupo watu wanne. Tukifika sehemu watu wamekaa yule mwenyeji anajitambulisha, anaongea maneno 20 kidogo kisha anasema leo ana ofaa ya vitu flani flani, (nilipooona vile nkakumbuka aina ya kazi niliyoipata).

Tulizunguka kuanzia ile asubuhi hadi jioni kwa mguu, sijala hata kitu yule mwenyeji wetu alinunua maji ya kandoro akatugaia na sisi kidogo. Aisee, imefika jioni muda wa kurudi nikikumbuka tulipotoka ni wapi halafu tunatakiwa kurudi kwa miguu tena! Nikaona Enough is Enough! Nikawambia wazee nimebanwa haja kubwa ngoja ntafute pori nakuja. Nikaingia pori flani nikatokea mbele panda boda boda straight hadi stand, nikalipa kisha panda dala dala hadi home. Nafika maskani saa 1 nina njaa sio kawaida na vyeti vyangu kwenye begi, kazi ikaishia hapo.

KUTEMBEZA MAJI NA SODA
Nakumbuka ndio miaka hiyo naingia Dar nikapata wana siwajui ila niliwaona tu ni wapambanaji nikawaelezea nia yangu,shida yangu wakaniambia, "imeisha hiyo wakwetu, twende ukachukue mzigo upge kazi." huyu jamaa yeye alikua anauza maji ya kutembeza, juice, soda za take away, biskut nk.

Nikamwambia mimi mtaji sina lakini, akasema usijali nakupeleka kwa boss wangu atakupa mzigo. Kweli tukatoka hao tukafika kwa muhindi mmoja hivi akanitambulisha, akamwambia "mimi iko letea wewe kijana ya kazi." Muhindi akauliza "hii hapana sumbua kama ile nyingine?" Jamaa akamwambia hii iko safi kabisa, basi baada ya hapo nikapewa kitrey Jamaa akanipakia mzigo wa kwenda kuzungusha.

Unachotakiwa ni unaenda na mzigo, unauza kwa bei ya reja reja ila wewe unachukua kwa bei ya jumla. Take away pale tulikua tunachukua kwa 800 wewe unauza 1000 na faida ni 200. Basi jioni mzigo utakaobaki unarudisha kwa muhindi, fresh maisha yanaenda.

Basi bana jamaa akanipakia trei langu kajaza soda, maji yaani vinywaji vyote muhimu. Mzigo huo yaani kujitwisha tu lazima mtu akutwishe. Tukatoka hao, jamaa akaniambia sasa mwanangu hapa tunagawana mitaa wewe pita kule mimi kule tutakutana badae. Nikamwambia fresh.

Tukaachana, tembea tembea na wewe mzigo ni mzito sina mfano. Kujitwisha peke ako huwezi, napishana na watu hata kununua maji hawanunui. Mchana ukakolea, jua likakolea kiu ikanikamata. Acha kabisa kuhusu kiu, bora ushikwe na njaa utavumilia ila sio kiu cha maji.

Hapo nimejikaza imefika saa 11 inaenda 12 jioni sijauza hata biskuti! Kiukweli ilifika mahali nikaona hapa ninapoendea ni kufa kizembe. Nikatafuta kivuli nikajitua mzigo wangu, nikachukua fanta passion nikafungua nikainywa yote! Kiu hakijaisha na njaa ndio imekolea, nkachukua Biskuti na fanta nyingine nikashushia.

Baada ya hapo nikaamka nikaomba kutwishwa, safari moja kwa moja mpaka kwa muhindi. Kufika pale ashukuriwe Mungu sikumkuta, nilikuta wafanyakazi, nikawaambia mzigo wangu msiguse naenda chooni mara 1 nakuja. Nikauweka pale nilivyotoka ndio kimoja yani sikugeuza shingo. Nilijiona ntaja kufa kwenye kazi za wahindi kizembe.

Basi kuna kazi nyingi sana nimeshazifanya hadi kufikia hapa nilipo. Bandiko lenyewe hili naliandika nafuta naliandika nafuta, yani tangu wiki iliyopita naandikaga tu. Kazi zingine nitaziendeleza kwenye comment maana kama ni kujaribu tu wanangu nimejaribu sana tu.

Naomba kuishia hapa tukutane kwenye comment hapo tuendeleze mikasa. Ila yote kwa yote tufahamu jambo moja katika utafutaji, ni marufuku kukata tamaa. Fanya kila uwezalo, feli, kosea, anguka, zomewa ila mwiko kukata tamaa. Uta aibika lakini nakuhakikishia mwisho wake huwa ni mzuri tu.

Hakunaga mwisho mbaya au mbovu kwa mtafutaji mpambanaji, nimeshuhudia na nimeliona kwangu binafsi hamna kitu na enjoy kama background ya maisha yangu ya nyuma. I have many many untold stories ambazo ki ukweli ndio siri ya mafanikio yangu, siku ntakuja na ID feki ntaachia makombora.

Haya ninayo yasimulia ni trailer tu, picha kamili zipo nitazisimulia siku moja. All in all tupambane, tusikate tamaa maisha ni mazuri sana ukijishughulisha. No matter what, fanya unachoona ni sahihi kikikushinda usilazimishe jaribu kingine. Usigande na jambo moja yawezekana bahati yako haipo kwenye hilo unalofanya.

Ushauri ni mwingi nazidi kurefusha thread tu, aisee tukutane chini hapo. Sema mwanangu Mbekenga unazingua yani unaosha vyombo ughaibuni unaogopa mwambia wife, au umekosea hukumaanisha wife ulimaanisha mchepuko au kimanzi flani?

Men, we dont hide our hustles kwa wake zetu. We tell them ukweli mweupe, uamuzi ni wao wauchukie au waupokee. kuna heshima katika hiyo kazi yako ya kuosha vyombo mkuu, mwambie waifu utaona atakavyo kuheshimu. Change brother, mfanye mke rafiki yako acha mambo ya kizamani.

Ila umepambana japo wewe hiyo haijakushinda, tuambie kilichokushinda maana vyombo unaendelea kuosha means hamna changamoto yoyote eneo hilo. Tupe zile ngumu kumeza ulizoona hapana hizi siwezi.
😆
 
Wakuu kuna kitu inaitwa mlima, hii kitu isikie tu kwa jirani hizo sijui zege,kuchunga, kulinda zikasome

Miaka ya nyuma sana bado bwana mdogo napiga chuo cha utalii huku nikiwa najitegemea kulipa kodi ya nyumba na mahitaji mengine, hali ikawa tete zaidi nikawa nimecharara sina kitu demu wangu ambae tulkuwa nae chuo japo yeye alkuwa anasomea mambo mengine, alijua wakati ninao upitia akanipa muongozo wa kupanda mlima, hivyo akaongea na mzee mmoja anipatie nafasi ya kupanda mlima kama porter[ mbeba mizigo ]

Mambo yakatiki nikapata nafasi ya kupanda hivyo nikawa nimeshajiandaa na vifaa vyote vinavyohitajika.

SIKU YA KWANZA: tulikusanyika asubuhi mapema sana pale ofisini kusubiri coaster ya kampuni ije ituchukue kuelekea moshi kwa ajili ya kuanza safari ya kupanda mlima

Tulkuwa jumla ya wabeba mizigo/ma-porter 20 ila wawili ambae ni mm na jamaa flani tulkuwa bado ma-form one hatujawahi kupanda kabisa, huyu mwenzangu alishapewa hints za namna ya kupanda mlima na kaka yake ambae ni guide wa mlima kabisa, hivyo akawa tayari ana experience ya maneno akaanza kunichimba mikwara pale nje kabla coaster haijafika.

“oya mwanangu umejipanga kupanda mlima? Mm kwa week 2 nlkuwa naamka asubuhi nakimbia kilometer 10 na push ups napiga sana sio chini ya 200 na bila hayo mazoezi huwezi toboa hapo juu utakufa”

Daah baada ya kusikia haya maneno niliishiwa nguvu kabisa nikajiona kweli mm naenda kufa, kwa maana hata push ups 10 tu siwezi nikipambana ni 6. Nikasali sna na kujitahidi kutosikiliza maneno ya mshakaji maana yamejaa vitisho na kukatisha tamaa, lakini kwa upande mwingine ni vya kweli hapo juu ni pamoto wakuu.

safari ikaanza kuelekea moshi, huko ndani ya gari hao maporter wazoefu wanapiga story za vifo,majanga, vitisho vya mlima asee haki ya mungu nilitamani ile gari iharibike tusifike moshi au nipate dharura yoyote nirudi town.

Hatimae tukafika getini “Kilimanjaro national park”
Dakika 10 mbele bado tupo kwenye gari akaja ranger/askari pori akatusalimia, akawa anatupa taarifa “vijana kuweni makini kama afya yako si nzuri usilazimishe kupanda mlima, muda si mrefu tumeshusha maiti 2 ya mzungu na porter” hapo utumbo ukasokota ghafla nikatamani kutoa machozi ila sikuwa na namna nishayavulia nguo maji sharti nikukata mawimbi.

Tukashuka kwenye gari tukapewa kila mtu mzigo wake, ile coaster ikawashwa dereva huyo kwenye kipupwe anarudi zake town, hakika nilitamani kurudi town na ile coaster lakini haikuwezekana na nikamuona yule dereva ni mtu mwenye bahati sana kayapatia maisha.

Safari ikaanza huo mzigo ni kilo 20 unauweka hapo shingoni ukichoka unaukumbatia kama dhambi ili mradi ufike tu, bana nikapiga hatua 5 na ule mzigo shingoni nikapiga kelele uwiiiiiii jamani mm sitafika kwa namna hii, watu hoii sna wakacheka sana wengine matusi juu.

Nikakaza buti bana mara miguu ikaanza kufunguka kwa hii siku ya kwanza camp haikuwa mbali huwezi amini nikajikuta nafika camp wa 2 wale wengine 18 wote nimewapiga chini.

Jioni ikapigwa msosi ugali kwa mboga za majani, ule ugali ndugu yangu haufiki mahali yoyote hizo mboga zenyewe ni mchuzi tu na chakula ni muhimu sana kutoboa mlimani bila chakula hufiki mahali.

Wale jamaa wakaanza tena vitisho vyao ule wakati wa kulala, wanasema kesho mdogoo utakiona cha moto kesho ndo kazi inaanza rasmi[emoji23][emoji23] nikawa kimya tu, kimoyo moyo nikajisemea mafala nyie wavuta bangi msinitishe.

SIKU YA PILI: hii siku kweli ndo ilkuwa tunaanza kazi rasmi maana sio kwa kutembea kule yaani unatembea mpaka unajiuliza hivi ninaenda mbinguni nini? Maana kuna hatua kwenye mlima ukifika mawingu unayona yakiwa chini sio juu tena,

Kitu nilichoharibu nilkula karanga mbichi njiani zikanilegeza miguu na yule form-one mwenzangu ikafika sehemu tukashindwa kutembea tukakaa chini ili mizigo tukaifungua tukatupa sacks 3 za unga huko kwenye vichaka ili mzigo upungue lakini wapi, shughuli ni ile ile ngoma bado mbichi unaambiwa ni hapo tu ila hufiki.

Kuna wagumu wa kampuni nyingine wakatukuta tumekaa chini wakatuuliza nyie form-one tukawajibu ndio, wakasema kazeni asee msikae hapa tena huko nyuma hakuna watu tena sisi ndo wa mwisho na huku kuna wasomali wanafi-raa si mchezo

Hapo kusikia mambo yakuliwa tope tena,tukapata nguvu tukaanza mwendo hatimae tukafika camp nyingine,

Wakuu kama mtakuwa interested ntaendelea na siku ya 3 mpaka ya mwisho kuna mabalaa huko katikati si mchezo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nakumbuka miaka 4 nyuma hapo Geita kuna ghorofa jirani na Lenny hotel juu kabisa tunaweka zege kwa ajili ya matenki ya maji,sasa shughuli ikaanza kijana wa watu nina siku 2 msosi kwangu dhahabu na mifuko simenti 10 inatakiwa kule juu dah! nakili nilihisi natoka roho mifuko 4 tu kwisha habari yangu. Uzuri foreman wetu alikuwa njema yule jamaa nilimwomba akanielewa tukaendelea na kazi nyingine riziki ikapatikana! Sitoweza sahau hiyo day
Unaenda kubeba mfuko wa simenti huku unanjaa..naona ulienda kutafuta kifo..pole sana.

#MaendeleoHayanaChama
 
Wakuu kuna kitu inaitwa mlima, hii kitu isikie tu kwa jirani hizo sijui zege,kuchunga, kulinda zikasome

Miaka ya nyuma sana bado bwana mdogo napiga chuo cha utalii huku nikiwa najitegemea kulipa kodi ya nyumba na mahitaji mengine, hali ikawa tete zaidi nikawa nimecharara sina kitu demu wangu ambae tulkuwa nae chuo japo yeye alkuwa anasomea mambo mengine, alijua wakati ninao upitia akanipa muongozo wa kupanda mlima, hivyo akaongea na mzee mmoja anipatie nafasi ya kupanda mlima kama porter[ mbeba mizigo ]

Mambo yakatiki nikapata nafasi ya kupanda hivyo nikawa nimeshajiandaa na vifaa vyote vinavyohitajika.

SIKU YA KWANZA: tulikusanyika asubuhi mapema sana pale ofisini kusubiri coaster ya kampuni ije ituchukue kuelekea moshi kwa ajili ya kuanza safari ya kupanda mlima

Tulkuwa jumla ya wabeba mizigo/ma-porter 20 ila wawili ambae ni mm na jamaa flani tulkuwa bado ma-form one hatujawahi kupanda kabisa, huyu mwenzangu alishapewa hints za namna ya kupanda mlima na kaka yake ambae ni guide wa mlima kabisa, hivyo akawa tayari ana experience ya maneno akaanza kunichimba mikwara pale nje kabla coaster haijafika.

“oya mwanangu umejipanga kupanda mlima? Mm kwa week 2 nlkuwa naamka asubuhi nakimbia kilometer 10 na push ups napiga sana sio chini ya 200 na bila hayo mazoezi huwezi toboa hapo juu utakufa”

Daah baada ya kusikia haya maneno niliishiwa nguvu kabisa nikajiona kweli mm naenda kufa, kwa maana hata push ups 10 tu siwezi nikipambana ni 6. Nikasali sna na kujitahidi kutosikiliza maneno ya mshakaji maana yamejaa vitisho na kukatisha tamaa, lakini kwa upande mwingine ni vya kweli hapo juu ni pamoto wakuu.

safari ikaanza kuelekea moshi, huko ndani ya gari hao maporter wazoefu wanapiga story za vifo,majanga, vitisho vya mlima asee haki ya mungu nilitamani ile gari iharibike tusifike moshi au nipate dharura yoyote nirudi town.

Hatimae tukafika getini “Kilimanjaro national park”
Dakika 10 mbele bado tupo kwenye gari akaja ranger/askari pori akatusalimia, akawa anatupa taarifa “vijana kuweni makini kama afya yako si nzuri usilazimishe kupanda mlima, muda si mrefu tumeshusha maiti 2 ya mzungu na porter” hapo utumbo ukasokota ghafla nikatamani kutoa machozi ila sikuwa na namna nishayavulia nguo maji sharti nikukata mawimbi.

Tukashuka kwenye gari tukapewa kila mtu mzigo wake, ile coaster ikawashwa dereva huyo kwenye kipupwe anarudi zake town, hakika nilitamani kurudi town na ile coaster lakini haikuwezekana na nikamuona yule dereva ni mtu mwenye bahati sana kayapatia maisha.

Safari ikaanza huo mzigo ni kilo 20 unauweka hapo shingoni ukichoka unaukumbatia kama dhambi ili mradi ufike tu, bana nikapiga hatua 5 na ule mzigo shingoni nikapiga kelele uwiiiiiii jamani mm sitafika kwa namna hii, watu hoii sna wakacheka sana wengine matusi juu.

Nikakaza buti bana mara miguu ikaanza kufunguka kwa hii siku ya kwanza camp haikuwa mbali huwezi amini nikajikuta nafika camp wa 2 wale wengine 18 wote nimewapiga chini.

Jioni ikapigwa msosi ugali kwa mboga za majani, ule ugali ndugu yangu haufiki mahali yoyote hizo mboga zenyewe ni mchuzi tu na chakula ni muhimu sana kutoboa mlimani bila chakula hufiki mahali.

Wale jamaa wakaanza tena vitisho vyao ule wakati wa kulala, wanasema kesho mdogoo utakiona cha moto kesho ndo kazi inaanza rasmi[emoji23][emoji23] nikawa kimya tu, kimoyo moyo nikajisemea mafala nyie wavuta bangi msinitishe.

SIKU YA PILI: hii siku kweli ndo ilkuwa tunaanza kazi rasmi maana sio kwa kutembea kule yaani unatembea mpaka unajiuliza hivi ninaenda mbinguni nini? Maana kuna hatua kwenye mlima ukifika mawingu unayona yakiwa chini sio juu tena,

Kitu nilichoharibu nilkula karanga mbichi njiani zikanilegeza miguu na yule form-one mwenzangu ikafika sehemu tukashindwa kutembea tukakaa chini ili mizigo tukaifungua tukatupa sacks 3 za unga huko kwenye vichaka ili mzigo upungue lakini wapi, shughuli ni ile ile ngoma bado mbichi unaambiwa ni hapo tu ila hufiki.

Kuna wagumu wa kampuni nyingine wakatukuta tumekaa chini wakatuuliza nyie form-one tukawajibu ndio, wakasema kazeni asee msikae hapa tena huko nyuma hakuna watu tena sisi ndo wa mwisho na huku kuna wasomali wanafi-raa si mchezo

Hapo kusikia mambo yakuliwa tope tena,tukapata nguvu tukaanza mwendo hatimae tukafika camp nyingine,

Wakuu kama mtakuwa interested ntaendelea na siku ya 3 mpaka ya mwisho kuna mabalaa huko katikati si mchezo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu pole sana..tunasubiri mwendelezo.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hii ya kuogesha wazee hii!! 😂😂😂😂😂 Imenivunja mbavu kweli kweli...😂😂😂😂😂
 
Ngoma kama hiyo nilimshuhudia mwamba mmoja wa tanesco akikata moto

Kapanda kwenye msitm sijui alijichanganya nini yule jamaa akapolochoka kutoka juu mpka chini akatua kwa kukaa tulisikia mtu anaguna tu MMHHH!! Akakata moto

Kazi nyingne sio poa
Nimecheka kifala Kama mazuri vile dah!
 
shusha vitu mkuu.
 
Niliuza machungwa mitaa ya Tanga mjini, siku wife kanikuta mtaani Hadi ananionea huruma, nimepauka hatarii, mimi mweusi ila nimekuwa kama chungu kwa jua, yaani wie acha TU, hadi machozi yalimtoka
 
Tumekaa zetu maskani mara akaja jamaa yetu kasema kuna hela ya chap twendeni, kufika ni matikiti yamejaa chini kuna fuso kama tatu zinatakiwa kujazwa kwa safari ya Dar. Tukakubaliana dau, jamaa tunasema hii ni hela ya fasta aisee. Tukaanza tukiwa sita hivi, umakaa chini unamrushia aliyeko kwenye gari, nilirusha matikiti hadi nikahisi mabega yatachomoka. Huwezi amini hata fuso moja hatujaza, sijawahi kuchoka namna ile, yaani mikono ilikuwa mizito kiasi kwamba hata kunyanyua mkono kushika kichwa ilikuwa mbinde. Tukapewa kifuta jasho tukaondoka zetu.
 
Back
Top Bottom