Kazi nilizowahi zifanya na zikanishinda kwenye utafutaji

kuna ile stori ya jumaa ambae alisingizia ndugu yake kafarikiii sijui so akaruhusiwa kwenda kuzikaa mwenzio akapigika balaa walidhani wanaenda kuwa makarani kwenye godauni....
 
[emoji28][emoji28][emoji28]

#MaendeleoHayanaChama
 
Kwanza huyo anaesema ukadai chako hamtakii mtu mema kuna kazi za kudai chako na zingine sepa tu. Unaweza dai chako wana wakakuweka mtu kati kuwa umekwamisha kazi kwann usiseme mapema. Binafsi nilisha dai changu sema ilikua tofali kujengea sasa ile kazi tulikua wasaidizi 2 na mafundi wawili. Mwanzo wa kazi jamaa niliekua nae tunasaidia akapandisha tofali 15 juu ile kushuka akasema nakuja naenda nunua sigara. Nikajua huyu harudi nnikamchana fundi oyaa huyu haridi ongeza mtu jamaa wakasema poa asipokuja wanaongeza. Nikapiga kazi wee mpka nikaona haji tena nikawaambia oya huyu ndio haji mazima. Wakasema poa anajenga mmoja mwingine nikomae nae. Aahh ajabu nae komaa nae anasimama nikamwambi yule wa juu namalizia nusu ya kazi hii hiyo nusu nyingine mtajua wenyewe na hela yangu ipo pale pale. Bwana wewe kwenye kulipana tulisumbuana sema walilipa maana wanajua kuwa makosa ni yao. Na wanajua nitakiwasha mno. Ila zile kazi kama mwoga usiende na kama mlaini acha utateseka
 
nakumbuka miaka 4 nyuma hapo Geita kuna ghorofa jirani na Lenny hotel juu kabisa tunaweka zege kwa ajili ya matenki ya maji,sasa shughuli ikaanza kijana wa watu nina siku 2 msosi kwangu dhahabu na mifuko simenti 10 inatakiwa kule juu dah! nakili nilihisi natoka roho mifuko 4 tu kwisha habari yangu. Uzuri foreman wetu alikuwa njema yule jamaa nilimwomba akanielewa tukaendelea na kazi nyingine riziki ikapatikana! Sitoweza sahau hiyo day
 
๐Ÿ˜†
 
Wakuu kuna kitu inaitwa mlima, hii kitu isikie tu kwa jirani hizo sijui zege,kuchunga, kulinda zikasome

Miaka ya nyuma sana bado bwana mdogo napiga chuo cha utalii huku nikiwa najitegemea kulipa kodi ya nyumba na mahitaji mengine, hali ikawa tete zaidi nikawa nimecharara sina kitu demu wangu ambae tulkuwa nae chuo japo yeye alkuwa anasomea mambo mengine, alijua wakati ninao upitia akanipa muongozo wa kupanda mlima, hivyo akaongea na mzee mmoja anipatie nafasi ya kupanda mlima kama porter[ mbeba mizigo ]

Mambo yakatiki nikapata nafasi ya kupanda hivyo nikawa nimeshajiandaa na vifaa vyote vinavyohitajika.

SIKU YA KWANZA: tulikusanyika asubuhi mapema sana pale ofisini kusubiri coaster ya kampuni ije ituchukue kuelekea moshi kwa ajili ya kuanza safari ya kupanda mlima

Tulkuwa jumla ya wabeba mizigo/ma-porter 20 ila wawili ambae ni mm na jamaa flani tulkuwa bado ma-form one hatujawahi kupanda kabisa, huyu mwenzangu alishapewa hints za namna ya kupanda mlima na kaka yake ambae ni guide wa mlima kabisa, hivyo akawa tayari ana experience ya maneno akaanza kunichimba mikwara pale nje kabla coaster haijafika.

โ€œoya mwanangu umejipanga kupanda mlima? Mm kwa week 2 nlkuwa naamka asubuhi nakimbia kilometer 10 na push ups napiga sana sio chini ya 200 na bila hayo mazoezi huwezi toboa hapo juu utakufaโ€

Daah baada ya kusikia haya maneno niliishiwa nguvu kabisa nikajiona kweli mm naenda kufa, kwa maana hata push ups 10 tu siwezi nikipambana ni 6. Nikasali sna na kujitahidi kutosikiliza maneno ya mshakaji maana yamejaa vitisho na kukatisha tamaa, lakini kwa upande mwingine ni vya kweli hapo juu ni pamoto wakuu.

safari ikaanza kuelekea moshi, huko ndani ya gari hao maporter wazoefu wanapiga story za vifo,majanga, vitisho vya mlima asee haki ya mungu nilitamani ile gari iharibike tusifike moshi au nipate dharura yoyote nirudi town.

Hatimae tukafika getini โ€œKilimanjaro national parkโ€
Dakika 10 mbele bado tupo kwenye gari akaja ranger/askari pori akatusalimia, akawa anatupa taarifa โ€œvijana kuweni makini kama afya yako si nzuri usilazimishe kupanda mlima, muda si mrefu tumeshusha maiti 2 ya mzungu na porterโ€ hapo utumbo ukasokota ghafla nikatamani kutoa machozi ila sikuwa na namna nishayavulia nguo maji sharti nikukata mawimbi.

Tukashuka kwenye gari tukapewa kila mtu mzigo wake, ile coaster ikawashwa dereva huyo kwenye kipupwe anarudi zake town, hakika nilitamani kurudi town na ile coaster lakini haikuwezekana na nikamuona yule dereva ni mtu mwenye bahati sana kayapatia maisha.

Safari ikaanza huo mzigo ni kilo 20 unauweka hapo shingoni ukichoka unaukumbatia kama dhambi ili mradi ufike tu, bana nikapiga hatua 5 na ule mzigo shingoni nikapiga kelele uwiiiiiii jamani mm sitafika kwa namna hii, watu hoii sna wakacheka sana wengine matusi juu.

Nikakaza buti bana mara miguu ikaanza kufunguka kwa hii siku ya kwanza camp haikuwa mbali huwezi amini nikajikuta nafika camp wa 2 wale wengine 18 wote nimewapiga chini.

Jioni ikapigwa msosi ugali kwa mboga za majani, ule ugali ndugu yangu haufiki mahali yoyote hizo mboga zenyewe ni mchuzi tu na chakula ni muhimu sana kutoboa mlimani bila chakula hufiki mahali.

Wale jamaa wakaanza tena vitisho vyao ule wakati wa kulala, wanasema kesho mdogoo utakiona cha moto kesho ndo kazi inaanza rasmi[emoji23][emoji23] nikawa kimya tu, kimoyo moyo nikajisemea mafala nyie wavuta bangi msinitishe.

SIKU YA PILI: hii siku kweli ndo ilkuwa tunaanza kazi rasmi maana sio kwa kutembea kule yaani unatembea mpaka unajiuliza hivi ninaenda mbinguni nini? Maana kuna hatua kwenye mlima ukifika mawingu unayona yakiwa chini sio juu tena,

Kitu nilichoharibu nilkula karanga mbichi njiani zikanilegeza miguu na yule form-one mwenzangu ikafika sehemu tukashindwa kutembea tukakaa chini ili mizigo tukaifungua tukatupa sacks 3 za unga huko kwenye vichaka ili mzigo upungue lakini wapi, shughuli ni ile ile ngoma bado mbichi unaambiwa ni hapo tu ila hufiki.

Kuna wagumu wa kampuni nyingine wakatukuta tumekaa chini wakatuuliza nyie form-one tukawajibu ndio, wakasema kazeni asee msikae hapa tena huko nyuma hakuna watu tena sisi ndo wa mwisho na huku kuna wasomali wanafi-raa si mchezo

Hapo kusikia mambo yakuliwa tope tena,tukapata nguvu tukaanza mwendo hatimae tukafika camp nyingine,

Wakuu kama mtakuwa interested ntaendelea na siku ya 3 mpaka ya mwisho kuna mabalaa huko katikati si mchezo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaenda kubeba mfuko wa simenti huku unanjaa..naona ulienda kutafuta kifo..pole sana.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mkuu pole sana..tunasubiri mwendelezo.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hii ya kuogesha wazee hii!! ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ Imenivunja mbavu kweli kweli...๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Ngoma kama hiyo nilimshuhudia mwamba mmoja wa tanesco akikata moto

Kapanda kwenye msitm sijui alijichanganya nini yule jamaa akapolochoka kutoka juu mpka chini akatua kwa kukaa tulisikia mtu anaguna tu MMHHH!! Akakata moto

Kazi nyingne sio poa
Nimecheka kifala Kama mazuri vile dah!
 
shusha vitu mkuu.
 
Niliuza machungwa mitaa ya Tanga mjini, siku wife kanikuta mtaani Hadi ananionea huruma, nimepauka hatarii, mimi mweusi ila nimekuwa kama chungu kwa jua, yaani wie acha TU, hadi machozi yalimtoka
 
Tumekaa zetu maskani mara akaja jamaa yetu kasema kuna hela ya chap twendeni, kufika ni matikiti yamejaa chini kuna fuso kama tatu zinatakiwa kujazwa kwa safari ya Dar. Tukakubaliana dau, jamaa tunasema hii ni hela ya fasta aisee. Tukaanza tukiwa sita hivi, umakaa chini unamrushia aliyeko kwenye gari, nilirusha matikiti hadi nikahisi mabega yatachomoka. Huwezi amini hata fuso moja hatujaza, sijawahi kuchoka namna ile, yaani mikono ilikuwa mizito kiasi kwamba hata kunyanyua mkono kushika kichwa ilikuwa mbinde. Tukapewa kifuta jasho tukaondoka zetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ