Kazi nilizowahi zifanya na zikanishinda kwenye utafutaji

Vipi ulifika kibo au mawenzi?
 
Niliuza machungwa mitaa ya Tanga mjini, siku wife kanikuta mtaani Hadi ananionea huruma, nimepauka hatarii, mimi mweusi ila nimekuwa kama chungu kwa jua, yaani wie acha TU, hadi machozi yalimtoka
Hiyo moment ya kutoka machozi nishawahi kuexperience unakutana na mtu mnafahamiana mwanzo you start to feel weak na machozi yanakuwa kama yanataka kutoka ila hayatoki.
 
Mkali Sibeko wewe ilibidi udeal na kina Nina Zamdela ukiwa kwenye penthouse yako.
 
Vipi ulifika kibo au mawenzi?
Kibo na mawenzi unapita kabisa, unaendelea kupanda juu kuitafuta uhuru peak huko ndo mziki mzee baba inafika stage unahisi kuharisha ila hakuna kinachotoka si mchezo, oxygen hakuna kabisa ukifika level flani ya mlima, huko mzungu anakojoa mbele yako unavua na kumvalisha chupi mwnyw maana hajiwezi yupo nyang'anyang'a

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanaume sio lazima kila kitu mtwambie wanawake mioyo yetu ni dhaifu sana tunaweza ropoka tukawaharibia dili zenu. Mi mr akipitiaga changamoto hasemi ila akishasolve ananishirikisha..
Huwa ni vizuri mshirikisha mke wako mapito yako ili msije peana lawama

unajua "hata yale mambo" kama akili haiko sawa huwezi yatimiza kikamilifu

sasa ndio ukute umeficha, muda ukifika huna time akili yote ime JAM, hivi

kwa niwajuavyo wanawake mlivyo na wivu na mawazo yenu meusi si mtaanza

hisi mwanaume kashafanya yake huko ndio mana hawezi vizuri au hana mizuka ile

uliyoizoea,nk... Ndio mana tunasema ili kuepusha yote hayo uwazi kwa mke wako ni vizuri

Mke akielewa unayoyapitia hata kuwa na visirani vya hapa na pale,usiri sio mzuri

japo nakubaliana na wewe kuwa si kila jambo la kusema ila yale mazito mazito kusema lazima asee,tusije tiana lawama.
 
plus mawimbi maji yakawa yanaingia kwenye chombo chetu tuna kazi ya kuyatoa na visado boti linapigwa pushi na mawimbi mara chemli imeanguka imepasuka mpemba mmoja akanambia "wajua kuogelea weye ..mimi siokoi ntu nanusuru roho yangu mie "
😅😅😅 Dah nimecheka sana
 
Haijalishi unapitia changamoto gani katika maisha

Haijalishi unapitia magumu gani katika maisha yako

yawezekana umechoka,unahisi kama unateseka peke ako

si kweli', ukipitia huu uzi utagundua wote wanayoyasimulia haya

sifa yao kuu ni 1 "uvumilivu" na "kutokukata tamaa",usikatishwe tamaa

na mapito unayoyapitia kwa wakati huu,wenzako walishayapitia na sasa

imebaki kama simulizi za kuchekesha,lakini nakwambia hivi sio vichekesho

wakati watu wakiyapitia haya walikua wakilia machozi,wakivuja jasho,mioyo yao

ilikufa ikasinyaa,nk lakini leo hii zimegeuka kama "SHUHUDA" tunacheka tunafurahia

Chochote unachopitia sasa,Hali ngumu yoyote unayoiona mbele yako sasa amini

nakwambia ni "linapita" hutoteseka milele,hutoonewa milele,hutolia milele,hutohuzunika

milele,kesho yako itakua kicheko na simulizi na shuhuda kwa wengine,Kwa sasa

piga moyo Konde songa zako mbele Mkombozi wa kesho yako ni wewe mwenyewe,Usichoke kupambana,Mungu yupo anakuona.

And lets all say Amen!

Ameeen.......
 
Miaka flani hapo moro nasoma chuo cha ujenzi,
Life ngumu,nikashauriwa na jamaa yangu kwanini usiuze hata miwa inalipa...

Nikatafuta jamaa anauza miwa anipe hints, akuwa mchoyo wa michongo.Akanipa maelekezo yote.
Enzi zile wanakodi baiskel kulikua hamna boda,
Mtaji ulikua buku 15 tu.

Nikakodi baiskeli yangu huyooo nikakitafuta chuo cha SUA,nikakipita nikanyonga ngwinjo kuelekea ni "kauzeni" kama sijakosea...majina mengi nimesahau..
Niliendesha baiskeli zaidi ya masaa 2,
Kila ninaposimama kuulizia naambiwa ni hapo mbele..
Unasonga tu hufiki,hatimaye kuna ka mtaa nikafika nikaelekezwa mbele kidogo kuna kijumba.

Nikakuta kuna wazee wakarimu kweli,wakanipa kijana anipeleke shambani sasa...

Ebooo ikabidi niwaulize bado hatujafika?wakasema sio mbali ni hapo tu...nikajiuliza hii hapo tu si ndio ile naambiwa toka kule mwanzo na sikua nafika,Nikasema nishafika mpaka hapa wacha nijipe moyo...

Mana sikua nimezoea kufanya kazi ngum wala kuendesha baiskeli masafa marefu,miguu ilikua inatetemeka na kuchoka kwa umbali mrefu.

Tulitembea tena na baiskel kwa mda,mpaka tunafika sehem kuna kijumba mbele kuna kijinjia si kijinjia hasa ni ki mfereji...

Tukawacha baiskeli na ndala zangu tukaanza fata hicho ki mfereji...
Baada ya mwendo mbele tulikuta shamba kubwa sana la miwa....

Tulipofika dogo akaita mara kadhaa,kuna mzee akaitika akasema niko huku.

Tukasalimiana na mzee nikakaribishwa shamba kwa ukarimu.
Nikaulizwa nataka miwa ya bei gani,nikasema ya buku 10,akasema sawa unaweza kukata,mana mimi nimebanana nina miwa naanda muda si mrefu inakuja kuchukuliwa..

Nikasema naweza,nikapewa panga.

Nikauliza nikate mingapi,
"Niko busy kijana kata unayoweza kubeba"

Wee tamaa ikaniingia nikasahau safari ya nilikotoka.
Miwa ilikua ni mingi mno mingine iko chini tu ni kukataa tu,hapo moyoni nikasema kama ni hivi nitatoboa mapema.

Nikakata mizigo miwili mikubwa ya haja kwa msaada wa dogo [emoji38].

Kimbembe kwenye kubeba kuifikisha njiani baiskeli ilipo sasa.
Kwanza miwa ni mirefu na minene,pili ukibeba mingi inanesanesa na kukuyumbisha.

Mjomba ilibidi niigawe mara nne na bado nilifika kwenye baiskeli kwa tabu sana.
Nikajisemea tabu gani hiii..

Kwenye kuifunga kwenye baiskeli sasa ni mingi haikutosha ikabidi mingine ibaki,mzee anacheka tu...

Kimbembe kingine kuikokota hio baiskel ni shughuli...
Ki ukweli nilifika mjini ila miwa mingine mingi niliacha njiani kidogo niitupe yote.nisije nikafa bure na niliyokuwa nayo kwenye baiskel niliikatakata vipande vipande mana ni mirefu ilikua inanesanesa inasababisha baiskeli kuyumba. .

Sikuwahi kurudi tena na sitarudi.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwamba kukaa lindoni ukaona ni kifo lkn hujaona kifo kutembea njiani saa 8 au 9 usiku. Na hukuwaza ulikuwa tayari unakata tiketi ya segerea kwa kuondoka lindoni na kuacha mali ulizokabidhiwa? Ila nahisi hapa kwenye ulinzi hujanyoosha maelezo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…