Kazi ya Kuajiriwa vs Kujiajiri: Uhuru wa Fedha au Mateka wa Ndoto?

Last_Joker

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2018
Posts
272
Reaction score
414
Wacha tuseme ukweli, siku hizi watu wakiambiwa "nimeajiriwa", wengi hawachangamkii kama zamani.
Lakini ukisema "nimejiajiri", jicho la heshima linapanda — watu wanakuona kama Elon Musk au Bakhressa wa kitaa! 😂

Lakini ukweli ni upi? Kazi ya kuajiriwa ni kifungo cha ndoto zetu au ndio njia pekee ya kuwa stable? Na kujiajiri ni uhuru wa kweli au ni mateso yaliyofichwa kwenye jina la “boss”?

Kuajiriwa: Security au Presha ya Kudumu?​

Faida kubwa ya kuajiriwa?
Stable income. Kila mwisho wa mwezi mshahara unadondoka kwenye akaunti, hata kama mwezi haukuwa mrefu kama maelezo ya HR.

Kuna health insurance, NSSF, posho za lunch na usafiri, na unajua kesho una pa kwenda.

Lakini… kuna reality nyingine:
  • Unapanga likizo, boss anasema project bado haijakamilika subiri.
  • Una idea nzuri kazini, inafanyiwa kazi bila wewe kutajwa.
  • Una miaka 7 kazini, mshahara haujafika hata kwenye kima cha ndoto zako.
  • Ukiwa sick, unaogopa sick-leave.
  • Ukitoka kazini saa 10, bado unapokea simu za kazi saa 4 usiku.
So, ni kazi au utumwa wa karne ya 21?

​

Kujiajiri: Uhuru au Stress ya Kila Uchwao?​

Watu wanapenda kujiajiri kwa sababu:
  • Hakuna boss wa kumfanyia reporting kila siku.
  • Unaamua lini uanze kazi, lini ulale.
  • Faida yote ni yako — hakuna mtu wa ku-cut 70% ya jasho lako.
  • Unafanya kile unachopenda (kama kweli unapenda hiyo hustle yako).
Lakini reality ni ngumu kuliko trailer ya movie ya kutisha:
  • Kutokuwa na uhakika wa mapato.
  • Mara mteja anakudai, mara wateja hawana hela au hawaonekani.
  • Kuamka na kulala ukiwa na stress ya “leo tunauza au tunakula reserve?”
  • Ukiugua, biashara imesimama au inaendelea kwa kusuasua na hofu kibao
  • Hakuna leave, hakuna pension, hakuna security.
Kujiajiri ni full-time pressure disguised as freedom.

Basi Kipi Ni Bora?​

Hakuna jibu moja.
Kuna watu wanafanikiwa sana kuajiriwa — wana savings, wamejenga, wanamiliki assets, wana plan za miaka 10 mbele.
Wengine wamejiajiri lakini miaka 5 bado wanauza mafagio na kuhamia majukwaa ya motivational speeches bila capital ya kweli.

Cha muhimu ni kujijua na kujipanga.
Ukiajiriwa — jitahidi usiwe mateka. Tumia mshahara wako kama mtaji wa ndoto zako.
Ukijiajiri — kuwa na discipline ya ku-manage hela zako kama mtu aliyeajiriwa na serikali au shirika lenye kulipa vizuri.

Sasa Tueleze Wewe:​

Upo upande upi?
Team Kuajiriwa (kwa sasa au milele)
Team Kujiajiri (bila boss, lakini na pressure)​

Tuambie ni nini imekufanya uchague upande huo?
 
Kujiajiri kuna hitaji akili na nidhamu ya hali ya juu. Hakuna fala anayeweza kujiajiri akatoboa. Ukiona mtu amejiajiri akafanikiwa huyo hata akiajiriwa anaweza kufanya maajabu makubwa. Kuajiriwa kuna changamoto zake lakini nadhani kuna afadhali hasa kwa zile nafasi ambazo ningumu kupima kiwango cha kazi kilichofanyika ila kama umeajiriwa sales and marketing 🤣 noma
 
Huwa nawashauri baadhi ya watu... kama umeajiriwa na unashindwa kutimiza majukumu yako kwasababu ya uvivu, ulevi, ngono, matumizi mabaya ya pesa, kushindwa kujituma haitakaa itokee miujiza ukajiajiri ukatoboa.
 
Wacha tuseme ukweli, siku hizi watu wakiambiwa "nimeajiriwa", wengi hawachangamkii kama zamani.
Lakini ukisema "nimejiajiri", jicho la heshima linapanda — watu wanakuona kama Elon Musk au Bakhressa wa kitaa! 😂

Lakini ukweli ni upi? Kazi ya kuajiriwa ni kifungo cha ndoto zetu au ndio njia pekee ya kuwa stable? Na kujiajiri ni uhuru wa kweli au ni mateso yaliyofichwa kwenye jina la “boss”?

Kuajiriwa: Security au Presha ya Kudumu?​

Faida kubwa ya kuajiriwa?
Stable income. Kila mwisho wa mwezi mshahara unadondoka kwenye akaunti, hata kama mwezi haukuwa mrefu kama maelezo ya HR.

Kuna health insurance, NSSF, posho za lunch na usafiri, na unajua kesho una pa kwenda.

Lakini… kuna reality nyingine:
  • Unapanga likizo, boss anasema project bado haijakamilika subiri.
  • Una idea nzuri kazini, inafanyiwa kazi bila wewe kutajwa.
  • Una miaka 7 kazini, mshahara haujafika hata kwenye kima cha ndoto zako.
  • Ukiwa sick, unaogopa sick-leave.
  • Ukitoka kazini saa 10, bado unapokea simu za kazi saa 4 usiku.
So, ni kazi au utumwa wa karne ya 21?

​

Kujiajiri: Uhuru au Stress ya Kila Uchwao?​

Watu wanapenda kujiajiri kwa sababu:
  • Hakuna boss wa kumfanyia reporting kila siku.
  • Unaamua lini uanze kazi, lini ulale.
  • Faida yote ni yako — hakuna mtu wa ku-cut 70% ya jasho lako.
  • Unafanya kile unachopenda (kama kweli unapenda hiyo hustle yako).
Lakini reality ni ngumu kuliko trailer ya movie ya kutisha:
  • Kutokuwa na uhakika wa mapato.
  • Mara mteja anakudai, mara wateja hawana hela au hawaonekani.
  • Kuamka na kulala ukiwa na stress ya “leo tunauza au tunakula reserve?”
  • Ukiugua, biashara imesimama au inaendelea kwa kusuasua na hofu kibao
  • Hakuna leave, hakuna pension, hakuna security.
Kujiajiri ni full-time pressure disguised as freedom.

Basi Kipi Ni Bora?​

Hakuna jibu moja.
Kuna watu wanafanikiwa sana kuajiriwa — wana savings, wamejenga, wanamiliki assets, wana plan za miaka 10 mbele.
Wengine wamejiajiri lakini miaka 5 bado wanauza mafagio na kuhamia majukwaa ya motivational speeches bila capital ya kweli.

Cha muhimu ni kujijua na kujipanga.
Ukiajiriwa — jitahidi usiwe mateka. Tumia mshahara wako kama mtaji wa ndoto zako.
Ukijiajiri — kuwa na discipline ya ku-manage hela zako kama mtu aliyeajiriwa na serikali au shirika lenye kulipa vizuri.

Sasa Tueleze Wewe:​

Upo upande upi?​
Team Kuajiriwa (kwa sasa au milele)​
Team Kujiajiri (bila boss, lakini na pressure)​

Tuambie ni nini imekufanya uchague upande huo?
Kuajiriwa utumwa sana pia kuishi ndani ya Shelia
 
Huwa nawashauri baadhi ya watu... kama umeajiriwa na unashindwa kutimiza majukumu yako kwasababu ya uvivu, ulevi, ngono, matumizi mabaya ya pesa, kushindwa kujituma haitakaa itokee miujiza ukajiajiri ukatoboa.
Hapa mbona kama umemkatia tamaa, what if mtu akajiajiri ndio ikawa njia nzuri ya yeye kubadilika na kufanya makubwa.
 
Risk takers tunyooshe vidole juu.

Nimejiajiri na nafikiri nimefanikiwa.
Mtupe njia sasa na sisi ambao bado tunapambana na ajira huku tukiwa na hamu ya kujiajiri, tuone kipi sawa.
 
You can do both my friend.
Yes, unaweza fanya yote. Mimi nimeajiriwa lakini natoka kazini saa tisa na nusu, ijumaa saa sita na nusu na weekend niko free. Kazi yangu imeniwezesha pia kupata mtaji wa biashara ambayo anaisimamia dada yangu. Kwa hiyo inategemea aina ya ajira , mazingira ya kazi na mshahara unaopata.
Mimi siwezi kuacha ajira yangu maana ni nzuri sana, imenipa exposure etc. Ukisafiri hata siku 3 una 5 una 1 M ya allowance huku unalala 5 star hotel.
 
Kuna kitu kinaitwa Entrepreneur Mindset .

Swala kuifanya 100 iwe miambili ni swala gumu sana na ambalo linahitaji Sana Akili.

Ukiona MTU anaweza kuendelea popote iwe kaajiriwa au kajiajiri ujue yupo vizuri kiakili.

Ndo maana hauitaji hela nyingi kuendelea au kupiga hatua Ila mipango mizuri ya kuizalisha 50 kuwa 100.

Ukifatilia Sana watu waliofanikiwa katika kujiajiri wana nidhamu , kujituma na hawakati tamaa hata iweje.

Kuna jamaa alikuwa na duka la kawaida Sana alikuwa ni na frame yake nyumbani kwetu.

Alianza 2010 Ila leo 2025

Anamililiki Nyumba 03
Ana Eneo dogo kajenga frame
Na kafungua duka la jumla.
Ana Mgahawa katikati ya mji.

Safari yake nimekuwa ninaiona kwa macho

-nidhamu
-Kutokata tamaa
-Kuishi low key na Ku-chase dreams

Kwahiyo Mafanikio aliyonayo kwa sasa Anawazidi watu wengi waliojariwa.

Ni vizuri MTU akajipima wapi panamfaa then ajitose.

Pia biashara unaweza Ku-generate profit kupitia Ku-reduce running cost .

Kwahiyo ukiwa umejiajiri ukata kuishi Kama umeajiriwa ngumu kufanikisha malengo.

mfano ukiwa hauna Kazi ukapata ajira unalipwa 1M hautaanzia chini kimaisha Ila pamoja na kutoanzia chini bado hatofika juu kirahisi

Ila ukiwa umejiajiri utaanzia chini hapa nazungumzia watu wanaoanza na mtaji mdogo .

Sasa unakuta MTU mauzo yakiwa makubwa anaanza kula bata. wanawake , mwisho unarudi nyuma.
 
Back
Top Bottom