Kuna kitu kinaitwa Entrepreneur Mindset .
Swala kuifanya 100 iwe miambili ni swala gumu sana na ambalo linahitaji Sana Akili.
Ukiona MTU anaweza kuendelea popote iwe kaajiriwa au kajiajiri ujue yupo vizuri kiakili.
Ndo maana hauitaji hela nyingi kuendelea au kupiga hatua Ila mipango mizuri ya kuizalisha 50 kuwa 100.
Ukifatilia Sana watu waliofanikiwa katika kujiajiri wana nidhamu , kujituma na hawakati tamaa hata iweje.
Kuna jamaa alikuwa na duka la kawaida Sana alikuwa ni na frame yake nyumbani kwetu.
Alianza 2010 Ila leo 2025
Anamililiki Nyumba 03
Ana Eneo dogo kajenga frame
Na kafungua duka la jumla.
Ana Mgahawa katikati ya mji.
Safari yake nimekuwa ninaiona kwa macho
-nidhamu
-Kutokata tamaa
-Kuishi low key na Ku-chase dreams
Kwahiyo Mafanikio aliyonayo kwa sasa Anawazidi watu wengi waliojariwa.
Ni vizuri MTU akajipima wapi panamfaa then ajitose.
Pia biashara unaweza Ku-generate profit kupitia Ku-reduce running cost .
Kwahiyo ukiwa umejiajiri ukata kuishi Kama umeajiriwa ngumu kufanikisha malengo.
mfano ukiwa hauna Kazi ukapata ajira unalipwa 1M hautaanzia chini kimaisha Ila pamoja na kutoanzia chini bado hatofika juu kirahisi
Ila ukiwa umejiajiri utaanzia chini hapa nazungumzia watu wanaoanza na mtaji mdogo .
Sasa unakuta MTU mauzo yakiwa makubwa anaanza kula bata. wanawake , mwisho unarudi nyuma.