Kazi ya kubadilisha mandhari ya mji iliyopangwa kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing na kuwa ya Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing itamalizika leo, tarehe 28 Februari. Mandhari zinazobadilishwa ni pamoja na maeneo 9 ya maua, picha 60, bendera elfu 18 n.k. Mandhari hizo zitakuwepo hadi tarehe 20 mwezi Mei.