Kazi ya kufua na kufyeka nyasi nafanya

Kazi ya kufua na kufyeka nyasi nafanya

Swensa

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2024
Posts
2,880
Reaction score
4,295
Mambo vipi wakuu natafuta kazi zile za chap chap kama vile kufyeka nyasi naondoka na hela, kufua nguo za kike na za kiume imladi umeshaziloweka na sabuni ya unga nakuja nafika nafua fasta unanilipa kiasi tulichokubaliana nasepa,

Nafanya usafi vyooni kama kukiweka safi kila siku kiasi tunakubaliana, napalilia na kuondoa majani uwanja wako,

Napatikana MUSOMA WAKUU mi jinsia ME naomba msaada wenu
 
Je cost yako ni ngapi na kwa soko la Bongo kwa watu kukosa disposable income je uoni kwamba utakuwa unapewa peanuts tofauti na msuli unaopiga ? Unless una agency (kuunganisha watu upate commission) au kufanya kazi premium (gardening na bustani) unaweza kukuta unachopata hakitoshi hata panadol (pain killer) utakazohitaji kwa kuuma kichwa kwa kudai vijisenti vyako ambavyo ni vichache na unapewa kwa masimango....

1759314795542.png
 
Mambo vipi wakuu natafuta kazi zile za chap chap kama vile kufyeka nyasi naondoka na hela, kufua nguo za kike na za kiume imladi umeshaziloweka na sabuni ya unga nakuja nafika nafua fasta unanilipa kiasi tulichokubaliana nasepa,

Nafanya usafi vyooni kama kukiweka safi kila siku kiasi tunakubaliana, napalilia na kuondoa majani uwanja wako,

Napatikana MUSOMA WAKUU mi jinsia ME naomba msaada wenu
Kila la kheri kwenye harakati zako!
 
Wakuu kazi sipati humu nipo oline wakuu nashida njaa Leo basi mnitupie kwenye namba yangu 5k nikale kazi hamtaki kunipa😔
 
Wakuu kazi sipati humu nipo oline wakuu nashida njaa Leo basi mnitupie kwenye namba yangu 5k nikale kazi hamtaki kunipa😔
Duh I Cried because I had no Shoes Until I saw someone with no Feet....;
 
Mkuu sijui kingereza naomba unisaidie kwa kiswahili
1759323864890.png
Kila shida yako kuna mwingine yupo katika hali mbaya zaidi huyo unayemuomba buku 5 ili upate mlo mmoja huenda yeye ni bajeti yake ya siku tano....

Endelea kupambana ila kumbuka iwapo wote tungesema tuweke matatizo yetu hadharani kila mtu ayaone na achague.., wengi wetu tungesomba ya kwetu na kuondoka nayo kwa furaha....
 
Leo weekend wakuu hakuna mwenye nguo Wala kazi mbalimbali nifanye Leo jua Musoma halipo wakuu nguo zitakaukaje au imladi nifue tu nianike😁🤣 utajua wewe uvae mbichi
 
Back
Top Bottom