Kazi ya kuhudumu baa hasa kwa wanawake ionekane kuwa kazi ya heshima kama kazi nyingine

Willima

Member
Joined
Jul 27, 2022
Posts
26
Reaction score
39
Wahudumu wa baa hasa wanawake wanapitia changamoto nyingi sana, changamoto hizi hutokana na kudharauliwa kwa kazi hii kwakuwa watu wengi sana huamini Kuwa wahudumu hao hawana tofauti na wanawake wanao jiuza, jambo ambalo sio sawa kwa sababu kazi ya kuhudumu baa sio sawa na kazi ya wanawake wanao jiuza.

Kazi ya kuhudumu baa pia ni kazi inayo takiwa iheshimiwe haswa kwa wahudumu wa kike kwakua kazi hii pia ni njia ya kuingiza kipato kwa wanao fanya kazi hizo, kuwaheshimu wahudumu hao hasa wa jinsia ya kike pia inasaidia kuwapa ujasiri na morali ya kufanya kazi hiyo, na pia kuifanya kazi hiyo kuonekana kuwa ni kazi ya kawaida kama kazi zingine na kuwa wahudumu hao haswa wanawake wafahamu kuwa wao kama wafanya kazi wanahaki zao sawa na wafanyakazi wa mashirika mengine ikiwemo na haki ya kutokumdhalilisha muhudumu huyo. Wateja wanatakiwa kufahamu kuwa wahudumu wa baa haswa wanawake wanahaki na hivyo hawapaswi kuwa dhalilisha kwa namna yoyote ile.

Kazi ya kuhudumu baa inatakiwa ionekane kama ni kazi ya kawaida sana inayaweza kufanywa na wanamke wa aina yoyote hata kwa wahitimu wa chuo kikuu ambao hawajapata kazi ya taaluma yao, na hata kwa wanawake wanao kaa nyumbani tu pasipo kuwa na kazi ya kuwaingizia kipato wasione shida kufanya kazi hiyo kwani hata wafanya kazi wa kazi hiyo wana haki ya kuhesimiwa kama wafanyakazi wengine. Lengo kubwa hapa ni kuifanya kazi ya kuhudumu baa kuonekana kama kazi zingine amboyo inaweza kufanywa na mwanamke yoyote yule na mwanamke huyo aheshimiwe kama mfanyakazi mwingine.
 
Aaah labda waanze kwanza kujiheshimu wenyewe bhana japo sio wote ambao hawajiheshimu
 
Aaah labda waanze kwanza kujiheshimu wenyewe bhana japo sio wote ambao hawajiheshimu
Wewe unapaswa kutoa heshima yako kwakua hata waowenyewe hawapendi kudhalilishwa, hakuna binadamu anae penda kudhalilishwa.
 
Hupendi kudhalilishwa ila unajidhalilisha unategemea niniπŸ˜…
 
We jamaa kwa kurudia content haujambo... whats wrong? jana umetoka kuelezea ishu hii hii
 
Vp unatamani siku moja binti yako afanye kazi hyo ya u baamed ....tuanzie hapo
 
We jamaa kwa kurudia content haujambo... whats wrong? jana umetoka kuelezea ishu hii hii
Kuna demu yupo bar anakula na amemwelewa,anasubiri majibu yenu Ili yampe nguvu ya kumweka manz ndan as wife material 😜🚴
 
Inaonekana umekolea na unataka kumuweka ndani kabisa Barmaid. Kama ataweza jituliza mbona shega tu, vuta kitu maana huyu keshaona nyoka za aina zote, anaweza tulia.
 
Usituletee porojo hapa.
Kama unaona ma barmaid Ni watu wa heshima chumbia mmoja.
Pombe yenyewe sio kitu Cha heshima, iwejemuuzaji awe MTU wa heshima?
Wateja wa pombe nao sio watu wa heshima, iweje muuza pombe awe MTU wa heshima. Mwanamke anayeshikwa tako na kila mlevi anaweza kua MTU wa heshima?
Mwanamke muuza pombe na umalaya ni Kama traffic na rushwa.
 
Ni kweli master hii iheshimike kabisa pia mlete shemeji hapa buza kuna bar mpya itamfaa na ataheshimika kama shemeji yetu
 
huko ni kama kwenye madanguro tu kwa hio hata penyewe hapana heshima so ngumu sana kupata heshima huko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…