Willima
Member
- Jul 27, 2022
- 26
- 39
Wahudumu wa baa hasa wanawake wanapitia changamoto nyingi sana, changamoto hizi hutokana na kudharauliwa kwa kazi hii kwakuwa watu wengi sana huamini Kuwa wahudumu hao hawana tofauti na wanawake wanao jiuza, jambo ambalo sio sawa kwa sababu kazi ya kuhudumu baa sio sawa na kazi ya wanawake wanao jiuza.
Kazi ya kuhudumu baa pia ni kazi inayo takiwa iheshimiwe haswa kwa wahudumu wa kike kwakua kazi hii pia ni njia ya kuingiza kipato kwa wanao fanya kazi hizo, kuwaheshimu wahudumu hao hasa wa jinsia ya kike pia inasaidia kuwapa ujasiri na morali ya kufanya kazi hiyo, na pia kuifanya kazi hiyo kuonekana kuwa ni kazi ya kawaida kama kazi zingine na kuwa wahudumu hao haswa wanawake wafahamu kuwa wao kama wafanya kazi wanahaki zao sawa na wafanyakazi wa mashirika mengine ikiwemo na haki ya kutokumdhalilisha muhudumu huyo. Wateja wanatakiwa kufahamu kuwa wahudumu wa baa haswa wanawake wanahaki na hivyo hawapaswi kuwa dhalilisha kwa namna yoyote ile.
Kazi ya kuhudumu baa inatakiwa ionekane kama ni kazi ya kawaida sana inayaweza kufanywa na wanamke wa aina yoyote hata kwa wahitimu wa chuo kikuu ambao hawajapata kazi ya taaluma yao, na hata kwa wanawake wanao kaa nyumbani tu pasipo kuwa na kazi ya kuwaingizia kipato wasione shida kufanya kazi hiyo kwani hata wafanya kazi wa kazi hiyo wana haki ya kuhesimiwa kama wafanyakazi wengine. Lengo kubwa hapa ni kuifanya kazi ya kuhudumu baa kuonekana kama kazi zingine amboyo inaweza kufanywa na mwanamke yoyote yule na mwanamke huyo aheshimiwe kama mfanyakazi mwingine.