YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,902
- 52,001
Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambayo ni mpya tunatarrajia ifanye mambo makubwa ya kuongeza ajira kwa vijana mitandaoni.
Tanzania kumekuwa na tatizo kubwa la ajira. Njia moja ya kuondoa hilo tatizo ni kwa watu kutafuta kazi za kufanya online, yaani mitandaoni. Kazi zipo nyingi. Mfano, waweza pata kazi ya kutafsiri website ya kampuni au mtu kwa Kiswahili au kutafsiri kitabu. Unafanya online malipo yanakuwa kwa njia ya PayPal hela inaingia hata kwenye simu yako ya mkononi, hata mwajiri au mnunuzi awe Ulaya au Marekani au popote duniani.
Waandishi wa vitabu waweza andika vitabu na kuviuza online na watunmzi wa nyimbo bk waweza kulipwa online kwa njia ya paypal chap chap mtu aki click tu na kudownload kitabu au wimbo nk malipo muda huo huo yanaingia.
Pia, mtu waweza chora hata katuni, ramani za nyumba n.k ukauza online. Au, ukajitungia wimbo wako wa kienyeji binafsi nyumbani kwako bila hata kwenda studio, ukauweka kwa mfumo wa video au audio ukauuza online kwenye maduka kibao ya online.
Tatizo kwa Tanzania haijaruhusu matumizi ya kupokea pesa kwa njia ya PayPal ambapo mtu aki-click tu kununua bidhaa yako, pesa yako inaingia chapchap kwenye PayPal account yako.
Kenya walisharuhusu; vijana wengi hushinda mitandaoni wakitengeneza pesa wakiuza bidhaa zao, viwe vichekesho, michezo ya kuigiza n.k ambavyo huviuza online. Wanaweka clip zao kwenye maduka ya online mtu ananunua anamlipa online kupitia Paypal.
Kuna shughuli nyingi za ujasiliamali online. Kikwazo kwa nchi yetu ni upataji wa pesa wa kazi yako au mauzo yako online. Bado tuko enzi za mawe tukiamini minjia ya kizamani ya kupokea hela. Na hivyo kuifanya nchi yetu kuwa ni ya kulipa zaidi pesa za kigeni na si ya kupokea pesa za kigeni.
Serikali ikiruhusu upokeaji pesa kupitia PayPal itafanya vijana wengi waingie mitandaoni kutafuta pesa.
Biashara za online zaweza kufungua Watanzania wengi kupata pesa toka nje, sababu ni juhudi ya mtu binafs na ubunifu wake i tu auze nini. Waweza kujirekodi unarukaruka kama ngedere ukiimba hovyohovyo tu bila hata vyombo halafu ukaita wimbo Crazy Monkey Song ukauweka online na ukauza. Wapo watu wana pesa wanapenda vituko wananunua.
Taasisi za elimu nazo ziweke kwenye mitaala ujasiliamali wa online wasibakie tu kufundisha ujasiriamali wa kuzurura tu juani wa kimachinga.