Kazi ya kwanza ya Wizara mpya ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari iwe ni kuruhusu Watanzania kupokea malipo kupitia Paypal

Mleta uzi, Hongera kwa mada nzuri.
Kwa kweli inasikitisha kwamba watanzania tunaweza kununua tu huduma nje ya nchi lakini hatuwezi kulipya au kupokea malipo kutoka nchi za nje. Hili jambo liangaliwe kwa haraka na wizara husika. Nina hakika kama PayPal na Stripe zitaruhusiwa nchini, naamini itapanua wigo wa ajira kwa vijana, ubunifu na hatimaye maendeleo kwa ujumla. Serikali ijikite tu katika kusimamia mfumo/ transaction za fedha.
 
Pamoja na mambo mengine mfumo wa address ni muhimu sana katika eBay na hii ni kwa muuzaji na mnunuaji.
Upo ulazima wa kuwa na physical address kwa wakazi wote nchini .
Yes, Ni kweli. Haya mambo yako chini ya uwezo wa serikali na yanawezekana. Kuna haja kubwa kwa wananchi kuruhusiwa kuendana na technologia ya dunia. Si vizuri kubaki nyuma.
 
Kutokana na sayansi kuwa ni suala mtambuka, nafikiri wizara hii ingepaswa kuwa Wizara ya Sayansi Elimu ya Juu na Teknolojia, kwa kuwa mambo ya "Information & Communication Technology - ICT) yangaliweza kupunguza "mismatch" iliyopo hivi sasa.

Labda pengine hii imetokana na umahiri wa wataalamu wetu kufanikiwa kuzima mitandao ya kijamii nyakati zile za kutangaza matokeo ya uchaguzi wa mwaka huu, na kuweza kukibeba chama tawala kwa ushindi wa kishindo, hali iliyopelekea dhuluma kubwa dhidi ya matakwa halisi ya wapigakura kura.

Hiii inawezakuleta kuleta hisia kuwa "Wezi wetu wa kura hatimaye wamepewa wizara yao rasmi"

Sent from my Nokia 2.1 using JamiiForums mobile app
 

Hiyo wizara kazi yake kubwa itakuwa kutrack watu mitandaoni tu na kupiga fine vyombo vya habari.
 
Huo ni ushauri mzuri kwa mwaka 2026 kwa sasa tunawaza namna ya kuzima mitandao ya kijamii yote.
 
Sioni swala hili likipatiwa ufumbuzi hivi karibuni.

Watu wamelipigia sana kelele hili swala lakini serikali imeweka pamba masikioni. 👇👇

Tujuzane njia ya kupokea pesa kwa Paypal Tanzania

Umuhimu wa huduma ya Paypal Tamzania

Lini Tanzania itaruhusu matumizi ya Paypal?

Ni aibu kwamba mpaka sasa Tanzania hatuna mfumo wa kupokea pesa kwa Paypal

Nimefanya kazi ya mtu, anataka kunilipa kwa PAYPAL lakini imeshindikana

Malipo ya Paypal hivi kweli serikali yetu imeshindwa kuruhusu hili?

Ombi: Tunaiomba BoT iruhusu malipo kwa njia ya Paypal Tanzania isipokuwa iweke vigezo maalum

Kupunguza tatizo la ajira serikali iruhusu huduma ya kupokea pesa kupitia PayPal

Paypal: Upotevu wa mapato na ajira Tanzania

Tanzanians need to receive money via PayPal - sign the petition

Make Tanzanians Receive Money with Paypal

Tanzanians need to receive funds via PayPal

uzi maalumu wa kumshauri mheshimiwa maghufuli kuingilia suala la paypal tanzania

Inasikitisha 2017 haiwezekani kupokea fedha kupitia PayPal ukiwa Tanzania


PAYPAL Status in Tanzania

Malalamiko na Maulizo ni mengi ila hakuna action yoyote iliyochukuliwa.

IMBOMBO NGAFU.


 
Tusubiri miujiza labda!! Hii nchi yetu ina uadui na teknolojia na wabunifu toka enzi...
 
Mkuu Chige ,yaani nataka kutuma 150K US$ huko nyymbani,naambiwa hazitafika,nitachapwa na fimbo ya "money laundering".
Nimetuma 150K US$ kwa mafungu 30,ndio salama yangu.
 
Yes, Ni kweli. Haya mambo yako chini ya uwezo wa serikali na yanawezekana. Kuna haja kubwa kwa wananchi kuruhusiwa kuendana na technologia ya dunia. Si vizuri kubaki nyuma.
Si tu kubaki nyuma bali tunapoteza fursa muhimu kama taifa ya kutuingizia pesa
 
Mkuu Chige ,yaani nataka kutuma 150K US$ huko nyymbani,naambiwa hazitafika,nitachapwa na fimbo ya "money laundering".
Nimetuma 150K US$ kwa mafungu 30,ndio salama yangu.
Yaani hii serikali, we acha tu! Sasa si kutiana hasara huko!! Manake kwa kufanya transfer ya mafungu I bet umeingia gharama maradufu kuliko kama ingekuwa ni single transfer!!

Kazi tunayo safari hii!!
 
No dirty transactions in TZ kalipianeni Kenya PayPal in first world is not used to pay individuals ila watz mmepinda sana!!
Hivi hata Paypal yenyewe unaijua kweli wewe?! Ni First World ya wapi unayoizungumzia kwamba hawaruhusu individuals kulipwa kwa PayPal?!

Halafu ulivyo na mawazo ya ki-ujima, bila aibu unahusisha PayPal na dirty money!! Yaani mtu anafanya biashara online au anatoa service online, akilipwa kwa PayPal kwako hiyo ni dirty money?!

Hivi kuna mahali wanaku-fight dirty money kuliko US and other Western Countries?! Hivi kwa akili yako unadhani PayPal ingeruhusiwa ku-operate kwenye hizo nchi?
 
KI uhalisia paypal itaogeza mapato serekalini kwa kiwango cha kutisha kabisa watanzania watakuwa free kuuza chochote nje hata dawa zao za kienyeji kumbukeni tunayo madawa mengi sana hapa tanzania
 
PayPal ni nzuri ila inabidi itengenezewe regulations kwanza isiwe kienyeji tu tutakuja kulia, jambo la heri ila linaweza tumiwa vibaya na wahalifu .
Man,

PayPal wenyewe regulations mzuri ingawaje haimaanishi nasi hatuwezi kuwa na za kwetu!

Don't forget, PayPal is an American Company, na sidhani kama dunia hii kuna nchi iliyo sensitive na dirt monies kuizidi US!! Sote tumeshuhudia hapa back 2014 FMBE Bank ikipigwa kufuli na rungu likitoka huko huko US!

Haya mambo ya Money Laundering waliotuletea kwenye sheria zetu na hao hao Marekani!!!

So, hata hao PayPal they operate under STRICT US Laws against Money Laundering!! Ndo vile tu Wabongo wengi wanaofanya Forex Trading wanatumia brokers wa vichochoroni lakini kama ingekuwa wanatumia well established brokers, wangegundua kwamba kuna very credible brokers Ulaya na Australia lakini hawaruihusiwi ku-operate in US kwa sababu tu, hawakidhi some US Laws!!!

To be honest, I doubt kama tunaweza kuwa na AML Regulation far better kuzidi waliyonayo PayPal.

Kibongo bongo watu tunaweza kuona hawapo strict kwa sababu transactions zetu ni ndogondogo tu ambazo hazileti suspciopus activity lakini hata hizo ndogo, PayPal huwa ina-monitor velocity yake!!
 
Mkuu Chige ,yaani nataka kutuma 150K US$ huko nyymbani,naambiwa hazitafika,nitachapwa na fimbo ya "money laundering".
Nimetuma 150K US$ kwa mafungu 30,ndio salama yangu.
Paypal kwa tanzania yetu tuiwekee limitations yaani transactions ziwe chini ya dollar $25000 above that pesa ni lzima iwe inapitia bank au vile serekali itaona jinsi ya kupanga kiwango let say pesa hii ikakatwa vat na service charges mbali mbali serelali haioni itapata sana mapesa ona jinsi makampuni ya simu yanavyotukamua ukitoa 10000 wanakata 1000 a bulshit theft
 
hivi kwa nini hawa mbwa wanashindwa hata kujifunzia Kenya nilimsikia rais wao akizungumzia kutengeneza cryptocurrency ila huku hawana habari kabisa
 
Paypal kwa tanzania yetu tuiwekee limitations yaani transactions ziwe chini ya dollar $25000 above that pesa ni lzima iwe inapitia bank au vile serekali itaona jinsi ya kupanga kiwango let say pesa hii ikakatwa vat na service charges mbali mbali
Nadhani ungeongelea labda limit ya kutoa lakini si kiasi gani mtu awe nacho kwenye akaunti ya paypal

Iko hivi mfano unauza katuni yako online kwa mnunuzi ku download hiyo katuni uliyojitengenezea .Kuuza ONLINE UNAUZIA WATEJA DUNIA NZIMA

Sasa chukulia unauza hiyo katuni dola 10 Wateja milioni moja duniani wakaipenda hiyo katuni na kukulipa kwa paypal ina maana hapo utakuwa na dollar milioni 10 Kwenye akaunti yako ya Paypal

Limit huwezi iweka kwa wateja kuwa wanunue wangapi ila kwenye kutoa pesa huko kwaweza kuwepo limit
 
Yah! Yaani PayPal kwetu ni kama inatu-encourage kuwa buyers badala ya kuwa both... buyers na sellers!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…