Kazi ya mtandaoni

Kazi ya mtandaoni

Ukiona nimeandika hivyo ujue fo really nipo serious na ninachokiongea. Sijali kukatishwa tamaa na wengi ila wachache watakaonihitaji nitawasiliana nao na mwisho nitapata ninachohitaji. Asante.
 
Lazima ni art maana science wengi tena wa miaka hiyo walishaajiriwa
Ukisoma vizuri hapo juu, mimi nina kazi nimeajiriwa na serikali. Ila lengo nikutafuta kazi ya kufanya kwa muda wangu nilionao wa ziada nimesema masaa 7 kwa siku. Ninathamini muda sana, kwa sasa niko free nahitaji mtu wa kuniajiri nimfanyie kazi online si kwa kufundisha tu bali nina ujuzi mwingine nimetaja hapo juu. Asante.
 
Asante ndugu ila forex hapana nshaijaribu, nilisoma hadi vitab na kumpata mentor ila mambo yakawa ndivo sivyo
Tafuta uzi wa Google Adsense, keyword zinalipa zaidi kwa sasa na masharti yao. Humo humu JF. Fungua blog ila tumia blogsot ni nyepesi sana. Kisha tafuta template na custom domain. Unaweza tumia za kulipia kama .com au ya bure kama .tk, ga.

Andika articles kama 20 na kuendelea zenye maneno kuanzia 15000 na kuendelea. Article zako ziwe kwa kiingereza na angalau ziwahusu wazungu.

Kisha omba Google adsense. Kisha anza kushare articles zako zilizokwenye blog. Kadiri wazungu wanavyobonyeza matangazo ndivyo hela inaongezeka. Ukifikisha $100 utatoa kwa western union na maisha yanaendelea.

Mambo yote yapo Google na Youtube. Pia kama upo vizuri unaweza kuanzisha darasa yaani unarekodi vipindi vya masomo ukiwa unafundisha kisha unaweka Youtube. Ukishafika watch hour 1000 na subscriber 1000 unaomba Google adsense unaanza kula pesa.

Mambo yote yapo Google na Youtube.
 
Kwa article ya maneno 2000 unacharge kiasi kwa neno?

Unaweza kufundisha Kiswahili kwa watu ambao hawajui Kiswahili kabisa?
 
Kwa article ya maneno 2000 unacharge kiasi kwa neno? Unaweza kufundisha Kiswahili kwa watu ambao hawajui Kiswahili kabisa?
Ndio, naweza kufundisha mkuu. Article ya maneno 2000 waeza kulipa $40 tu. Karibu sana.
 
Nenda freelancer.com kazi hizo utapata online chap tu
 
Back
Top Bottom