Kazi ya Sticker za usalama barabarani ni nini?

Kazi ya Sticker za usalama barabarani ni nini?

Joined
Sep 10, 2023
Posts
32
Reaction score
81
Wadau naomba kuuliza jambo hapa,ivi kazi ya sticker za usalama barabarani huwa ni nini?
Na ni utaratibu gani unatakiwa ufuatwe ili kuzipata hizi?

Maana sielewi na ninachokiona huku mtaani,kumekua na wimbi la vijana wanaosimama sehemu mbali mbali wakiwa wamevalia reflector jacket wengine za sensa🤣

Wanasimamisha magari na kuwauzia madereva hizi sticker kwa gharama ya sh. 5000.

Sometimes hawa wamekua wanasimama kwenye check point za polisi na unashangaa polisi anakusimamisha lakin anaekufata ni raia na kizibao chake anakuja kuuliza kuhusu sticker.

Hapa napata mkanganyiko hi kitu ipo kisheria au ni mradi wa mtu tu?
 
Yani kumekua na masticker mengi mengi hayaelewiki kuna zingine unaambiwa za makundi maalumu,haieleweki kabisa inatakiwa uwe na sticker ngapi.
 
Wakiona sticker ipo watakuuliza Fire Extinguisher ipo ili waone mwaka wake wa mwisho ukikutana na kichefuchefu atakuuliza Triangle ili mradi apate kosa lolote achukue rushwa tu hakuna kingine...
 
Ni stika inayokuruhusu uendelee kuendesha gari kwa usalama bila kusumbuliwa na raia wanaovaa sare fulani na kuzitumia kujikusanyia pesa za matumizi mbali mbali
 
Hizo sticker hazina umuhimu wowote ule. Ni chanzo kimojawapo tu cha wizi wa mchana kwa wamiliki wenye magari.
Mwanzo ilikua ili upate sticker unapeleka gari traffic wanaikagua ndio unapata sticker. Siku hiz sticker unaipata hata gari ikiwa mkweche. Halafu ukiwa huna sticker ya usalama barabarani faini 30000😂
 
Magufuri alifuta mambo ya stika nakumbuka yalirudi baada ya wahuni kuwa huru hiyo ni mchango wao tuu maana hakuna Control number ya Serikali unalipia ili upate hiyo Stika unakutana na muhuni anapokea hela kwenye kibegi Nchi hii ngumu sana...na wahuni wengine wanachapisha stika nyingi mtaani ili mradi wauze tu na wao za mtaani wanazijua...
 
Back
Top Bottom