Kwa ushari tu walimu wapya ambao mtapangwa kijijini hasa ndani ndani zaidi usikurupuke kuowa maana wakongwe watakushauri uoe ili iwe rahisi kupikiwa kufukiwa n.k, usikurupuke kukopa uliowakuta wengi watakushauri ivyoo ukope mapema soma mazingira vizuri ujue ukikopa utafanyaje kumbuka mshahara wako hauna posho ukiukopea na kununua vitu vya ndani au kujenga au kuolea au kufurahisha wazazi basi jua utaishi maisha magumu na utaona kazi mbaya , na kikubwa zaidi tafuta mitazamo mipya tofauti na uliyoikuta ujue jinsi ya kutoboa kimaisha Ila mtakaopangiwa mikoa ya kusini, Tabora,kigoma, Mungu awape uvumilivu katika kazi