Kazi ya ualimu na changamoto zake vijijini

Kazi ya ualimu na changamoto zake vijijini

Umeongea kitu kikubwa mno
Nashukuru kuliona hilo.Tujitahidi kuwashauri watoto,wadogo,kaka zetu waliojiluwa wasifanye makosa yaliyofanywa na wenzao,wameishapoteza miaka kadhaa mtaani wanatakiwa wawe smart.Akina Dada ndio tabu sana hukutana na matapeli wa mapenzi kisha hutapeliwa mishahara yao kupitia mikopo na majamaa huingia mitini na pesa na kuwatelekeza.Sijui kwa nini serikali haina vitengo vya ku washauri(mantorship) hawa vijana mpaka wanaharibikiwa.Nimeshuhudia wengi sana wakipoteza muelekeo.
 
kwa mabinti ni likelly kutengeneza ndoa na 'waume' walioko mijini ili wahamie huko,vinginevyo hudakwa fasta na wanakijiji wasio type yao, utakuta mvuvi au mkulima kaoa mwalimu
 
Changamoto ziko nyingi kulingana na mazingira ya kijiji,unakuta mwalimu amelowea huko, anakata mkaa sambamba na wanakijiji huku akijua athari za ukataji misitu hovyo
 
Mliopagwa halmashauri za kigoma mtanyooka tu

Speaking from experience of 5 yrs
Bila kusahau wale wa Same milimani- lugulu, vudee, myamba, kilangale, chome, suji, chanjagaa, bombo, mshiwi, ntenga nk pia mtanyooka tu😀😀😀
 
Kijijini ndo pazuri mkuu,Maana cost of living is so cheap,kule kuna vyakula vya kutosha pamoja na Bei ya pango sio kubwa sana,ukiwa na 'akili' unaweza uka invest na kupiga hela ya maana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa ushari tu walimu wapya ambao mtapangwa kijijini hasa ndani ndani zaidi usikurupuke kuowa maana wakongwe watakushauri uoe ili iwe rahisi kupikiwa kufukiwa n.k, usikurupuke kukopa uliowakuta wengi watakushauri ivyoo ukope mapema soma mazingira vizuri ujue ukikopa utafanyaje kumbuka mshahara wako hauna posho ukiukopea na kununua vitu vya ndani au kujenga au kuolea au kufurahisha wazazi basi jua utaishi maisha magumu na utaona kazi mbaya , na kikubwa zaidi tafuta mitazamo mipya tofauti na uliyoikuta ujue jinsi ya kutoboa kimaisha Ila mtakaopangiwa mikoa ya kusini, Tabora,kigoma, Mungu awape uvumilivu katika kazi
 
kwa mabinti ni likelly kutengeneza ndoa na 'waume' walioko mijini ili wahamie huko,vinginevyo hudakwa fasta na wanakijiji wasio type yao, utakuta mvuvi au mkulima kaoa mwalimu
Hii tabia ya kujidai sijui wanakijiji siyo type yako wakat unanjaa tu itakutafuna ndani kwa ndani heshimu kila mmoja, nyie ndo wale mkipata nafas mnawadharau walio chin yenu na kujiona bora zaid ya wengine
 
Back
Top Bottom