Kazi ya ulinzi ndugu zangu sio kazi wallah

Usiige tabia za mzee wako.
Huwa sipendi tabia za watu wanaowanyanyasa au kuwatendea vibaya watu ambao anajua fika hana analoweza kumfanya.
 
N
Ni kweli mkuu
 
Ila haya makampuni ya ulinzi hasa ya kibongo ni yana tamaa sana.
Nakumbuka kipindi flani nilikua nafanya kazi kama mhasibu kwenye kiwanda flani.
Kiwanda chetu kilikua kimeingia mkataba na kampuni flani ya ulinzi ambayo inamilikiwa na wabongo.
Kwenye makubaliano ni kwamba inatakiwa walinzi sita watakaokua wanaingia kwa shift yani mchana na usiku.
Walinzi watano wasiokua na silaha watakua wanalipwa na kiwanda shilingi laki 6 kila mmoja kwa mwezi na mlinzi mmoja mwenye silaha atakua analipwa shilingi laki 8 kwa mwezi.so kiwanda kikawa kinailipa ile kampuni ya ulinzi 3.8m kila mwezi tena on time kabisa,ila cha ajabu siku moja nikawa napiga story na mmoja wa wale walinzi akaniambia wao mshahara wao wanaolipwa ni shilingi laki mbili kwa mwezi tena kwa mbinde na hapo hakuna cha bima wala nssf.
Nikajisemea tu hizi kampuni za ulinzi za kibongo zimejaa ubabaishaji mwingi sana.
 
Acha tu wengi wamekuwa Omba Omba ,ukipita getini lazima umuachie hata buku 5 maisha yaende ,sasa siku ukitaka kupitisha mali ya kampuni ukimuachia elfu 50 atakataa? Wengi ni Wezi na Omba Omba wakiwa getini.
Yaan Sana☹️
 
Hiyo ndio dunia ya kibeberu.

Kama huna exceptional skills na huna alternative, lazima utatumika sana.

Hata sasa watu wanabebeshwa viroba vya unga kwenye magodawn viwandani usiku mzima kwa Tsh 8,000. Kula na nauli ni juu yako. Hakuna bima, NSSF wala likizo.
 
Unit price ya mlinzi ni 500+ mazingir yote mkuu. Ila ukishskuwa mlinz mambo ni tofaut sana, kulipwa tu mpaka ukadai kwa nguvu na kazi umefanya mwenyew
 
kama sijakuelewa,ila sema astaghafirullah..
yaani unamaanisha wanaofanya izo kazi za ulinzi ni hawajasoma na walikuq wanalala kipindi cha shule.
una miaka mingapi.
 
Hongereni wakuu kwa hustles na at least hii thread imeonesha uhalisia wa wengi tuliopo jf kuwa sio wote tunalipwa millions. Wengine 300k ni mshahara ideal kabisa kutokana na mishe tunazofanya.

Cha msingi ni halali na maisha yanaenda
cha msimgi mkono unaenda kinywani mzee,
binafsi mimi pamoja na elimu yangu ila niliji switch kutokuchagua kazi ya kufanya wala kumuonea aibu mtu yeyote dunia hii ambaye hanipi kula hata akiongea chchte.
nishalinda makampuni mengi sana paka halmashauri mgambo jiji nimefanya.
uhalisia wa kazi ya ulinzi kampuni linalolipa 300k hiyo kampuni bora watu wanalitafuta hilo chimbo vbya.
 
Hongera master.. Kazi yangu ya kwanza "internship" Nililipwa chini ya 300k japo gharama za siku ofisi inaniwezesha..
So naelewa master ukifika level flani unamshukuru Mungu maana ukilinda sana hadhi mwisho wa siku hufanyi lolote la msingi kwa kuogopa watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…