Kazi ya ulinzi ndugu zangu sio kazi wallah

Kazi ya ulinzi ndugu zangu sio kazi wallah

sema walinzi ni watu poa sana, ukikaa ukapiga nao stori wapo vizuri

nilivyokuwa mdogo nilikuwa nawapelekea chakula walinzi tunapiga stori

sema ni kweli wanaonewa, nakumbuka mzee alikuwa anawawasha vibao anapiga honi anakuta wamelala
na wananywea wanaogopa kusemewa kwenye kampuni zao
Hee huyo mzee wako alikuwa na stress au?
 
Shida mnafanya kazi kampuni za kipumbavu.

Mimi nimefanya kazi ya ulinzi miaka 4 (KK Security, baadaye ikawa Gardaworld).

Mshahara ulikuwa 250,000-280,000 kutegemea na mwezi na siku za kazi.

Likizo yenye malio, na NSSF.

Mpaka naacha nilikuwa na milioni 2 laki 7 NSSF ambazo nilichukua kwa kuanzia.

Sasa unafanya kazi ya ulinzi kampuni hazieleweki kwanini usiumie.

Na sisi hivi Hawa Gardaworld mishahara imepanea, nadhani ni zaidi ya laki 3. Maana wakati tunapata 250,000 basic yetu ilikuwa 150,000. Sasa hivi basic ni 222,000 kwahiyo ukijumlisha na overtime lazima inazidi laki 3
wambie hao mi Niko Garda take home nachukua 370
 
Mkuu we umefanya kazi ya ulinzi kampuni gani? Hata iyo hela uliyotaja sio wanayolipwa garda. Nina jamaa zangu wanafanya iyo kazi na si haba wako vzr. Garda wanapokea around 300-370 uyo ni normal guard, kama una kitengo maybe upo kwny crew au kwny issue za alarm ni zaidi ya iyo. We ulikuwa unafanya kampuni local, hivi vikampuni local ndo wana malipo ya kiwaki.
mkuu mi Niko gada na hapa Niko lindoni take home nachukua 380k na Nina bima plus nif
 
Mi nilikua kwenye mashirika hafu lindo likawa taasisi flani ya kutoa huduma. Kidogo nilikua napata pata tips za wateja. Ila kazi ya tatu kutoka mwisho niliowahi kufanya baada ya nyarugusu na chai mufindi.
Ile na cleaner bora cleaner mkuu, na mm naona hata biashara ya mitumba ina hela mana unaweza kuweka elf 40 ukapiga 70 per half day
 
Back
Top Bottom