Kazi za ovyo kwenye nchi hii

Kazi za ovyo kwenye nchi hii

Ulichoandika hakina uhusiano na nilichoandika.

Kwenye post yangu uliyoninukuu sijaongelea kipato.

sijaongelea kuhusu wewe kupitwa kipato na mwalimu.

Nimesema mtu anaweza akafanya kazi si kwasababu ya mshahara wa kazi husika, bali kwa sababu ya mapenzi yake na kazi husika (nikatolea mfano ualimu).
Usiwapangie kwa sababu wewe huipendi kazi hiyo.

Unanikataza nini?
Mkuu Nakukataza kunipangia cha kuandika.
 
Mkuu mimi nina ndugu wanafanya hizo kazi wengine wameanza tangu 2012,lakin wanavibanda vya kukaa tu... Njaa zimewajaa wanaombaomba tu utaskia "dogo tutumie hata kilo 20 za mchele nile na wanao hapa"
Hii ndio njaa?
 
Hii
Assalaam aleykum,

Wanajamvi leo acha tuongee ukweli hata kama tutakwazana ila tutajua tu. Kuna kazi ukikubali kufanya au kuajiriwa ni mateso/za hovyo na huwezi kutoboa labda uende kinyume na sheria, hakuna marupurupu, mishahara midogo na mazingira ya kazi yamekaa kimtego mtego sana.

1. ASKARI POLISI
i. Magereza.
ii. Mrafiki

2. WALIMU (kufundisha)
Hizi kazi watumishi wake wamejaa njaa, dhiki, ulafi na shida tupu.

3.
4.
5.
Hii thread yako haina ustawi kwa jamii , Je tusipokuwa na Polisi unafikiri hali ya usalama itakuwaje ? Je tusipokuwa na waalimu ni nani atafundisha watoto wetu ? Kila taaluma ina nafasi na umuhimu wake wa kipekee , tusiwakatishe tamaa na kuwabeza maana haiwasaidii , badala yake tuwatie moyo na kuwapambania maslahi yao yaweze kuboreshwa.
 
Wapi nimekupangia cha kuandika?
weka namba ya post inayoonyesha nimekupangia cha kuandika.
Ndo hayo ya kunipangia we gusa quoted reply mpaka utakapofika kwenye comment yako ya kwanza
 
Ukiwa mmiliki wa gari utaona kazi ya mpiga debe ni kazi mbaya na utamuona mpiga debe ni kama mtu asie na malengo na maisha yake, Ila kwake yeye hiyo ndo kazi inayompa heshima na anailisha familia yake na kaepuka na aibu za kuanika shida zake mbele za watu.

Ndo maana dunia hii mtu hutakiwi kudharau kazi unayoifanya hata kama wanao kuzunguka wanaidharau maana ukiiacha kazi kwaajili ya watu wanaidharau hao walioidharau kazi yako hawatakupa hela ya kusogeza maisha yako
Kaka Lucha Salute kwako Mkuu.
 
Kamshahara kadogo ila ni Kinga ya maisha yako mpaka kifo. Unaweza ukatumia huo mshahara kukopa na maisha yakaendelea. Hujaona watu wa kazi hizo wenye maisha poa? Sawa hakuna marupurupu ila jitafutie mwenyewe hayo marupurupu.
 
Ila kazi ya upolisi ukiwa kitengo unakula mema ya nchi sio mbaya kama inavosemwa,maana kama unaingiza angalau 50 kila siku nje ya mshahara upo vizuri
Polisi kazi nzuri mno nina ndugu yetu yupo umoja wa mataifa huko anapiga pesa tu,kilichompeleka huko ni kazi ya polisi.

Huyu juha muanzisha uzi acha aendelee kushikiwa akili ila wenye akili timamu tunajionea polisi si kazi ya hovyo,polisi anayefanya mambo ya hovyo huyo ndo mtu wa hovyo lakini kazi yake ya upolisi itaendelea kuwa nzuri na si ya hovyo.
 
Kwenye karne ambayo majority hawana kazi zenye ujira..., hakuna kazi ya hovyo ili mradi mkono unakwenda kinywani..... Ingawa kuna vitu ambavyo sio kazi tumevibatiza kwamba ni kazi (uchawa, siasa n.k.) Huwezi kusema kazi ambayo mtu anatoa elimu (kufanikisha wellbeing ya jamii) kwamba ni ya hovyo; unless wewe ni wa hovyo au unaangalia vitu kwa mafungu na sio kwa ukamili wake
 
Assalaam aleykum,

Wanajamvi leo acha tuongee ukweli hata kama tutakwazana ila tutajua tu. Kuna kazi ukikubali kufanya au kuajiriwa ni mateso/za hovyo na huwezi kutoboa labda uende kinyume na sheria, hakuna marupurupu, mishahara midogo na mazingira ya kazi yamekaa kimtego mtego sana.

1. ASKARI POLISI
i. Magereza.
ii. Mrafiki

2. WALIMU (kufundisha)
Hizi kazi watumishi wake wamejaa njaa, dhiki, ulafi na shida tupu.

3.
4.
5.
Mrafiki ndiyo kazi gani hiyo?
 
Mwalimu au askari wa aina yoyote ile kuwa tajiri au maskink ni uamzi wako tu
 
Back
Top Bottom