Mtanzanias
JF-Expert Member
- Jul 30, 2021
- 1,747
- 3,725
Nafikiri ubora wa timu unaangaliwa pia na upana wa kikosi chenye wachezaji wanaoweza kutoa ubora ule ule walionao wachezaji wanaoanza kikosi cha kwanza, Yanga wameonyesha ni timu yenye kikosi kipana kisichomtegemea mchezaji mmoja kupata matokeo.
Wameonyesha hilo kwenye mechi za ligi tofauti na timu nyingine zote zinazoshiriki ligi kuu na pia wameendelea kuonyesha kwenye mchezo wa leo kombe la Azam na wameondoka na ushindi mnono dhidi ya timu ya daraja la kwanza kurugenzi ya Simiyu, Wachezaji wafuatao wa kikosi cha kwanza awakucheza kabisa;
Djigui Diarra
Kibwana Shomari
Yannik Bangala
Dickson Job
Joyce Lomalisa
Feisal Salum
Kharid Aucho
Jesus Moloko
Fiston Mayele
Salum Abubakar
Abutwalib Msheri
Kwa maana hiyo ni timu ambayo imejengwa vizuri kwa uwiano wa viwango vya wachezaji tumeona jana Mozes Phiri kafunga goli 3 na leo kajibiwa na bwana mdogo Clement Mzize aliyeweka kambani goli 4, Phiri kacheza na timu inayoshiriki ligi ya mkoa lakini bwana mdogo kacheza na timu inayoshiriki ligi daraja la kwanza(first league) na ameperfom bila ya uwepo wa Mayele, Simba jana wamejaza mastaa wao wanawategemea dhidi ya timu dhaifu lakini utofauti wa ubora wa vikosi umeonekana leo baada ya Wananchi kuchezesha kikosi b na wakaibuka na ushindi wa goli 8 zile zile walizoshinda wale walioweka full mkoko. Pongezi kwa kijana Mzize anakuja vizuri akitulia.