Kazi za viwandani sio kazi, ni zaidi ya mateso

Siku Mama alipokuja kuniona nimekonda kama njiti alilia sana akanambia kama umetoka kwenye tumbo langu sitaki ufanye kazi hii.Mtoa mada umenikumbusha enzi hizo kiwanda cha korosho dadekii jioni una ambulia 3000 au 4000,Mhindi korosho ukikata vibaya na kisu imekula kwako kilo zinapangua.
 
Hii haikubaliki Zanzibar kazi ya siku moja hamna chini ya 20,000 kwanini wabongo wanakubali huu upuuzi,ndio sababu ya kujaza watu mitaani kila mtu anauza kitu..Waandamane kwa wazili anaehusika wasikubali kulipwa chini ya 20,000 kwa siku.kuna kiwanda koja tu hapa Kisemvule cha Wajerumani maadui wa serikali( Beberu) ndio kinalopa 20,000.
 
Ila sasa kuliko ukalipwe elfu nne kwa siku,,, Mbona kuna kazi nyingi tu za kufanya kama mtu una nguvu na afya.... Kuna vibarua vya saidia fundi, Kuna Biashara nyingi kama kutembeza matunda, umachinga vyote hivi vinalipa sana na Havitaki hata mtaji mkubwa. Ukiwa na elfu 20 tu unaanza biashara na unaweza pata faida hata hiyohiyo elfu 20 kwa siku
 
Unataka Watu walipwe elfu 20 ili waringe na wajae viburi na madharau kwa wengine? No way!

adriz de mbusii
 
Uzi kama huu tumeujadili sana humu.

Labda leo nikupe tu ushauri kama ni muhanga wa hizi kazi achana nazo anza kubeti.

Tafuta odds 2 tia buku 2 sikikizia buku 4 yako.

Hiyo buku 2 fanya kama ni sadaka ya kukuza mtaji.

Risk zipo na hili ulitambue ila tafuta odds zenye high possibility za positive outcome.
 
Mkuu bado hule mchongo wako uchwara wa mabango ya yas upo uje utupige tena?
Halafu kuna wapuuzi humu kila siku wanawaambia vijana wasihangaike kwenda nje! Hivi wanajua malipo ya viwandani Ulaya hawa? Enzi hizo karibu miaka 30 iliopita kiwanda cha magari X kwa saa ilikuwa Β£15 kazi masaa 12. 4 days on 3 days off
 
Anyway, jiongeze hapo hapo kazini mkuu. Kazi za bongo ukitegemea unacholipwa na boss hautoboi.
Aibe ? Maana hicho ndicho alichobakiza nakumbuka kuna mwamba alikabidhiwa kazi fulani hivi wakawa wanamlipa malipo ya kijinga halafu eneo analofanya kazi lina shehena ya mabaki ya ujenzi ya pesa nyingi, usiku akawa anavusha yale mabaki ya shehena kuanzia mbao mpaka misumari aliuza kwa siku alikua anaingiza kuliko ile pesa wanayomlipa.. walikuja kushtuka alipoacha kazi wakakuta mzigo wa mabaki ya vifaa vya ujenzi umepukutika kumbe mwamba alikua anaviuza usiku watu anawaingiza geti kubwa anaenda kuchukua bidhaa anawaonyesha wakikubari kununua anawapitishia geti dogo la nyuma ili camera zisije zikavujisha mafaili
 
Hii ukiwa hauna tamaa...mtaji mia tano..

Unaweza kulaza 5000 kikubwa usiwe na tamuuulaaa..

Wewe tafuta pesa ya kula...hio ndio ukisikia kuendesha familia na pesa ya ku bet.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…