joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Unajua maana ya maendeleo, kuendelea maana yake ni kuboresha hali ya maisha ya leo kuwa bora kuliko jana, Tanzania tumekua tukipiga hatua ya kuboresha hali za raia wetu kila siku, kama ulivyosema katika kipindi cha Kikwete tulikua hatujitoshelezi kwa chakula, leo hii tinazalisha zaidi ya mahitaji yetu na tunauza chakula cha ziada kwa nchi zingine, umeme vijijini ilikua ni nadra, sasa hivi karibia vijiji vyote umeme unawaka, huduma za Afya na hali ya usalama vimeimarika sana.Hayo matatizo yapo nchi zote za kusini mwa jangwa la sahara siyo kenya tu.
Kwani mkuu ni uongo GDP yao siyo kubwa kuzidi yetu? Au ukweli umekuwa uongo? Hata sisi SGR tukiweka siasa pembeni tumekopa sana.
Janga likija hasa la njaa ni nchi chache za Afrika linaweza kulimaliza. Unahisi Tanzania itokee ukame, au nzige waharibu mazao serikali itaweza wapa watu chakula. Umesahau kipindi cha Kikwete watu wana njaa wanapelekea eti debe la mahindi. Sasa wewe debe la mahindi utakula shilingi ngapi tena inapewa familia.
No need to hate, KCB imefanya poa.
Kenya wao ni tofauti sana, hayo matatizo niliyoyataja ni toka wapate uhuru wao, hakuna ambalo linapata nafuu, hali inazidi kuwa mbaya kadri siku zinavyoongezeka, ni aibu kwa nchi kama ya Kenya kukumbwa na njaa tangu wapate uhuru hadi leo na hawatafuti ufumbuzi wa tatizo kwa takriban miaka 60 sasa.
Sent from my TECNO-L8 using JamiiForums mobile app