DOKEZO KCMC sitorudi nikiwa na akili timamu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Acha watu waongee ukweli, utumbo wao inabidi usemwe tuu na next time please hakikisheni mna document mpaka majina yao, vyeo , utumbo uliofanyika, muda etc hii itatusaidia sisi wamiliki kuchukua hatua zinazostahili kuweka mambo sawa, tunawalipa hawa hawafanyi kazi bure na nyie mnalipia huduma mnatakiwa kuzipata bila usumbufu au kona kona za wapuuzi wachache tuliowaajiri, msikae kimya na uliyeleta huu uzi asante sana
 
Pole sana. Mm pia nashangaa kwa nini waninyime majibu ya vipimo vyangu? Nilienda kupiga x-ray hospital ya Dar Group. Jambo la ajabu walikataa kunipa picha yangu ya x-ray ingawa nililipa huduma hiyo
Walikupiga boss na hawakukufanyia x-ray, wahuni watupu wamejaa kwenye afya, hakuna sehemu yenye afadhari kila kona ni upigaji tuu
 
Binafsi nikiugua sipendi kwenda hospital labda nipelekwe
 
Hapo KCMC nilienda kumwona mgonjwa saa za kuona wagonjwa,nipofika ward husika nikaulizwa umekuja kumwona mgonjwa gani?nikasema mgonjwa X,nikaambiwa huyu kuna mtu ameshakuja kumwona,huwa tuna ruhusu mtu mmoja tu kumwona mgonjwa aisee niliduwaa sana pale na mimi nilifunga safari toka wilaya nyingine!kifupi nilikwazika sana na siitamani hiyo hospital.
 
Nenda CCBRT wakayamalizie macho yako, mwaka 2016 nilikwenda CCBRT nikapima macho na nikalipa shs.50,000/= nikaambiwa nirudi siku ya pili, niliporudi siku ya pili nikaambiwa siku yangu ilikuwa jana siyo leo hivyo natakiwa nilipe tena ili nitibiwe! Nilipochachamaa wakanipa vijidawa na kuniagiza watanitibu bure! siku inayofuata, nikaachana nao nikafunga safari toka Dar nikaenda KCMC nilifika jioni nikalala kwenye gesti iliyo nje ya hospitali. Asubuhi nikaingia hospitali kwenye saa saba nikapimwa nikapewa kitanda japo sikulala asubuhi nikaingia, mchana nikafanyiwa upasuaji nikalala wodini, siku iliyofuata asubuhi wakaiondoa plasta na kuniruhusu, jicho lilikuwa jipya zaidi ya la kijana na siku iliyofuata nikarudi Dar, kwa kifupi CCBRT siitaki kwani kuna malalamiko ya wengi kuharibikiwa macho kabisa. Mwaka jana 2021 nilikwenda tena KCMC kwa ajili ya jicho jingine na nilikaa kwa siku zilezile nne kama mwanzo, sikuona wala kusikia malalamiko kama yako, japo kuna watu wanataka wapimwe na kufanyiwa upasuaji siku hiyohiyo! Huenda nawe ni mmoja wapo, pole kwa mkasa.
 
Halafu inaendeshwa na shirika la dini, hizi imani za Kizungu zilizokuja kwa meli.
 
Hii hiko Hosp nyingi kwa sasa
AICC unapajua,, hata pale ipo..

Ukienda na bima ndio utabaki na ile karatasi 1
Ukiwa wa cash, utapata tu risiti za bills
Ila ukiomba printout unapewa
 
No offence, Taasisi zilizo chini ya KKKT zina changamoto nyingi sana kwenye kutoa huduma.
Kcmc Hopsital, Kcmc University, Tumaini University kuna ufisadi sana.
hydom pia wako hoi,wachungaji na maaskofu wanajaza mifuko
 
ndo maana walichukua vipimo daktari anaju njia bora ya kutuliza tatizo,au mtu atundikiwe drip ndo uridhike?
 
mpaka sasa kwangu ni the best wanajitahidi hata kama kuna changamoto lakini wanajitahidi
 


Umefanya la maana I hope wahusika wafikishiwe habari!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…