Keir Starmer kuwa Waziri Mkuu mpya wa Uingereza huku Rishi Sunak akikubali kushindwa

Keir Starmer kuwa Waziri Mkuu mpya wa Uingereza huku Rishi Sunak akikubali kushindwa

Kingsmann

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2018
Posts
4,805
Reaction score
17,850
BB1prqwj.jpeg
Sir Keir Starmer atakuwa waziri mkuu ajaye wa Uingereza baada ya Rishi Sunak kukubali kushindwa katika kukabiliana na chama cha Labour.

Waziri Mkuu Sunak alisema wapiga kura wametoa "uamuzi wa kutisha" juu ya chama chake baada ya miaka 14 madarakani.

BB1prsu0.jpeg
Kiongozi wa chama cha Labour Sir Keir Starmer alisema watu kote nchini Uingereza walikuwa wametangaza kuwa "tayari kwa mabadiliko".

Katika hotuba yake ya kukubali kushindwa baada ya kushikilia kiti chake cha Richmond na Northallerton, Bw Sunak alisema: "Chama cha Labour kimeshinda Uchaguzi huu Mkuu na nimempigia simu Sir Keir Starmer kumpongeza kwa ushindi wake."

Bw Sunak aliongeza: “Leo, tutabadilishana mamlaka kwa njia ya amani na yenye utaratibu na nia njema kwa pande zote. "Na ni jambo ambalo linapaswa kutupa imani sote katika utulivu na mustakabali wa nchi yetu."

"Watu wa Uingereza wametoa uamuzi mzito usiku wa leo, kuna mengi ya kujifunza ... na ninawajibika kwa hasara hiyo. Kwa watahiniwa wengi wazuri, wa Kihafidhina waliofanya kazi kwa bidii ambao wamepoteza usiku wa leo, licha ya juhudi zao zisizo na kuchoka, rekodi zao za mitaa na utoaji, na kujitolea kwao kwa jumuiya zao. Samahani."

=====

Pia soma: UK General Election: Waingereza leo kupiga kura kumchagua Waziri Mkuu na Wabunge
 
Wamewawekea majasusi kutoka civil services kwenye uongozi wa labour ilikuwa lazima ishinde baada ya chaos ya miaka 6 kwenye uongozi wa juu ndani ya conservatives.

Key player hapo ni ‘Rachel Reeves’ shadow chancellor ‘the city’ (financial and equity markets) wana imani nae uchumi utabaki salama chini yake sio mtu atakepeleka policies hatari kwao. Ndio maana huu uchaguzi wamekaa kimya.

Keir Starmer ni career civil servant last alikuwa DPP

Rachel Reeves kafanya kazi bank kuu, katoka hapo kaenda foreign office, mshauri mkuu wa mambo ya sera za uchumi na dunia, baadae U.K. embassy in US kushauri uchumi. Kurudi U.K. private banking, kaacha kazi ya mshahara wa pound million kadhaa with bonus kwenda kwenye siasa; wakati head hunters wa mabank wanamgombania.

Wamejaza civil servants kadhaa huko juu ambao sio career politicians, kushindwa ilikuwa possibility ndogo sana.
 
Lilikuwa ni suala tu la muda. Kwanza mtu mwenye aliipata hiyo nafasi kwa bahati nasibu tu. Halafu akajifanya kiherehere kuingia kwenye vita dhidi ya Urusi.

Na bado viherehere wenzake wengine. Wote watatoka madarakani na hivyo kuingia serikali mpya. Na hii ni kuan,ia hapo Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Marekani kwenyewe, nk. Kote wananchi wanafanya mabadiliko baada ya nchi zao kujiingiza kwenye mgogoro wa Urusi vs Ukraine na hivyo kuwasababishia athari za kutosha tu za kiuchumi.
 
Unadhani kuingia vitani na Urusi ni sera yake binafsi??
 
Unadhani kuingia vitani na Urusi ni sera yake binafsi??
Inawezekana ikawa ni sera ya nchi husika, serikali husika, chama husika, au hata kiongozi husika. Ila mwisho wa siku wananchi wengi katika nchi za Ulaya wamechoshwa na athari ya hivyo vita, na kwa sasa wameamua kupaza sauti zao kupitia sanduku la kura.
 
Ni sahihi,lakini haiwezekani ikawa ni sera ya kiongozi. Hyo inakuwa ni sera ya Taifa mkuu. Kama unataka kuamini hilo subiri hyo serikali itakayo undwa kama haita jihusisha na vita ya Urusi.
 
Lilikuwa ni suala tu la muda. Kwanza mtu mwenye aliipata hiyo nafasi kwa bahati nasibu tu. Halafu akajifanya kiherehere kuingia kwenye vita dhidi ya Urusi.

Na bado viherehere wenzake wengine. Wote watatoka madarakani na hivyo kuingia serikali mpya. Na hii ni kuan,ia hapo Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Marekani kwenyewe, nk. Kote wananchi wanafanya mabadiliko baada ya nchi zao kujiingiza kwenye mgogoro wa Urusi vs Ukraine na hivyo kuwasababishia athari za kutosha tu za kiuchumi.
Sera dhidi ya Urusi sio suala binafsi la Sunak. Ngoja aje huyu mzoefu wa serikali ndio utajua hujui.
 
Inawezekana ikawa ni sera ya nchi husika, serikali husika, chama husika, au hata kiongozi husika. Ila mwisho wa siku wananchi wengi katika nchi za Ulaya wamechoshwa na athari ya hivyo vita, na kwa sasa wameamua kupaza sauti zao kupitia sanduku la kura.
Uingereza 🇬🇧 na Waingereza wanaamini adui wao mkubwa ni Mrusi ...
 
Siasa za Uingereza nazo ni tiamaji sana, kidogo tu utqsikia huyo jamaa kajiuzulu.
Uingereza raia wake ni too demanding na wana deko la kuwa na historia ya viongozi wazuri zamani. Hawaridhiki na hawakubali mapungufu kidogo au uwezo pungufu kidogo wa kiongozi. Na hawana muda wa tumpe muda sijui tuwe na imani, mara anashauriwa vibaya. Wao ukifanya kosa moja ndio wamemaliza hivyo hawana imani na wewe.
 
Back
Top Bottom