Kelele za Bandari ya Bagamoyo zimeishia wapi? Haitojengwa, hakuna wa kukujengea bure!

Kelele za Bandari ya Bagamoyo zimeishia wapi? Haitojengwa, hakuna wa kukujengea bure!

Kijakazi

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2007
Posts
7,093
Reaction score
10,469
Ni lini Watanzania tutakuja kuelewa kwamba hakuna kitu cha bure? Yaani Mchina atoke kwao aje kukujengea wewe Bandari kwa lipi hasa?

Inanikimbusha Mji wa Kigamboni kwamba USA wanakuja kujenga Mji wa kisasa Kigamboni, USA wachukue fedha za walipa kodi wao wakujengee wewe Mji, kwa lipi haswa?

Ni lini tutaelewa kwa nchi inajengwa na wenye nchi?

Malizeni Bwawa la Nyerere > 2000 MW acheni kujidanganya.
 
Kwa UPUMBAVU WA FORENI TU KUTOKA BANDARINI MPAKA UBUNGO. MASAA HADI 3 - 4 ACHA IJENGWE TU HIYO YA BWAGAMOYOWAKO.
 
Waseme $30bilion zitatoka wapi na watazirudisha vipi, sio tu kuja na miradi mikubwa ya pesa nyingi waviachie vizazi vijavyo mizigo wasioweza kuibeba.

Tumeshaambiwa na WB nchi yetu ina madeni yasiyovumilika, sasa ni wakati wa kuwa makini na haya mambo tusizidi kujitumbukiza shimoni.
 
Mbona Tazara walijenga?

Unajua sababu ya kujengwa tazara ? Ilikuwa ni kusafirisha shaba ya Zambia, kipindi hicho kulikuwa na cold war Zambia ilizuiwa kusafirisha mzigo wa China kutumia Bandari nyingine kama Durban au Beira na option pekee ilikuwa Dar ndo maana TAZARA ikajengwa, kwa lengo moja tu kusafirisha Copper ya Zambia kwenda China, unajua kwa nini leo hii imekufa ? Kwa sababu cold war imeisha Zambia anaruhusiwa kutumia Bandari nyingine kama Beira au Durban, tazara haina kazi hivyo imekufa.
 
Kwa UPUMBAVU WA FORENI TU KUTOKA BANDARINI MPAKA UBUNGO. MASAA HADI 3 - 4 ACHA IJENGWE TU HIYO YA BWAGAMOYOWAKO.

Haitojengwa, kwa maana hakuna pesa za kujengewa!
 
Wakati wa mchakato unafanyika mlikuwa mnapiga kelele
Sahv kuna ukimya,mnapiga kelele

Ova
 
Hiyo hela tutakopa wapi tena, maana tumeshawekwa kwenye 'heavily indebted poor countries' labda tuanze kuuza ndege.
 
Ni lini Watanzania tutakuja kuelewa kwamba hakuna kitu cha bure? Yaani Mchina atoke kwao aje kukujengea wewe Bandari kwa lipi hasa?

Inanikimbusha Mji wa Kigamboni kwamba USA wanakuja kujenga Mji wa kisasa Kigamboni, USA wachukue fedha za walipa kodi wao wakujengee wewe Mji, kwa lipi haswa?

Ni lini tutaelewa kwa nchi inajengwa na wenye nchi?

Malizeni Bwawa la Nyerere > 2000 MW acheni kujidanganya.
Kwa hakika furaha yangu itakuwa kubwa mno iwapo bandari hii haitojengwa. Mambo mengine ni roho mbaya tu na si chochote.
 
Kuna siku watu watachapwa viboko..tuna haraka sana na baadhi ya mambo bila kujari athari zake
 
Back
Top Bottom