Wewe unajua wazi kwamba haukua uamuzi wa busara KDF kwenda Somalia, juzi tu ulisema kama sababu ilikua ni kuzuia Alshabab kuteka watalii, ni bora mngepeleka KDF ili kuimarisha doria katika mpaka wa Somalia wakati mmkiendelea kujenga ukuta.
Sasa ninakuuliza swali, gharama ya kuwalinda watalii wasitekwe na Alshabab ni uhai wa wakenya wanaouliwa kila siku?. Kabla ya KDF kwenda Somalia na baada ya KDF kwenda Somalia, ni kipindi kipi Kenya ilikua na amani?.
Jaribu kukaa chini na kujichunguza jinsi mnavyofikia maamuzi yenu, msijisikie vibaya kukubali pale mnaposhauriwa, kuendelea na ukaidi kudhani kwamba hamkosei, ni kuendelea kulimbikiza ujinga.