Hii inatisha sana, raisi huyu mteule ameapa kutenda kazi zake za UHALIFU...!!!
mzee usicheke maana hili ni kubwa inabidi mzee KT alifatilia maana ni batili..ila naona haijastukiwa tu..ile ni batili ile..na nadhani waandaaji wamefanya makusudi..maana wanajua ni mhalifu kweliMay be am getting crazy! Kila nikiangalia huyo mzee na kipara anatamka mbele ya hadhara na kuahidi kutenda uhalifu!!! oh,, God nacheka sana hadi nahurumia mbavu zangu sasa kwani zinauma!
HESHIMA MBELE MH. YOMBA JAMENI. NAONA KIDOGO UKAJARIBU KUSEMA KWAMBA MIMI NAWEZA KUWA NA SUPPORT RAILA KWAJILI YA UKABILA BASI INAHUZUNISHA SANA. HIO ITAKUA NA MAANA KAZI YOTE TUMEFANYA KENYA FROM 1982 KUPANDA MEBGU ZA DEMOKRASIA TUKIWA VIONGOZI WA WANAFUNZI CHUOO KIKUU HADI SASA TUFUNZAPO KUKO HUKO NI KAZI BURE. NAJUA HAUMANISHI HILI LAKINI NI MUHIMU KUFAHAMU RAILA ANA SAPPOT YA MIKOA 6 AU 87% YA WAKENYA AU MAJORITY YA MAKABILA 40. DATA YA BBC NI DATA POTEVU, MAONI YA MH. ZITTO USIYAPUUZE ANA UELEWA WA SIASA ZA KENYA MPAKA HATA MIMI NADHANI KWAMBA YEYE NI MKENYA. SHUKRAN KWA MAONI YAKO MKUU YOMBA. KIBAKI MUST GO AND HE WILL GO.
HAPPY NEW YEAR KWA WAHESHIMIWA WOTE WA JAMBO FORUMS, MUNGU IBARIKI TANZANIA
mzee usicheke maana hili ni kubwa inabidi mzee KT alifatilia maana ni batili..ila naona haijastukiwa tu..ile ni batili ile..na nadhani waandaaji wamefanya makusudi..maana wanajua ni mhalifu kweli
Kwa hali ya sasa ya Kenya nadhani mimi namlaumu sana mwasisi wa Taifa lile, yaani Mzee Kenyatta kuliko huyu Kibaki. Inawezekana kabisa kuwa Kibaki hakuwa na haja ya kufanya yaliyotokea ila ameshinikizwa na wakikuyu walioko katika position nyingine kama Mahakama, Jeshi, Polisi na hata kwenye hiyo ECK yenyewe. Mzee kenyatta ndiye aliyejenga mazingira yanayowafanya Wakikuyu waone kama ni haki yao kuwa watawala wa Kenya. Laiti Mzee Kenyatta angejenga misngi imara ya utaifa kama alivyofanya mwenzie Nyerere, leo hii watu wasingekuwa wanashabikiana kwa ukabila bali wangekuwa wanashabikiana kwa sera kama ilivyo hapa Tanzania ingawa watu wetu hawajakomaa sana kisiasa kama wenzao wa Kenya.
Lawama pekee ninazomtupia Kibaki ni kuwa alishindwa kufahamu kuwa utawala wake umekuja katika mazingira delicate sana kuliko yale aliyokuwamo Kenyatta, na uchaguzi huu umafenyika katika mazingira ambayo siyo ya wakikuyu dhidi ya waluo kama wakati wa Kenyatta. Nilivyoona ramani ya Kenya utaona kuwa ni wakikuyu tu waliomsupport (Central, East and NorthEast) wakati Odinga kapata support ya makabila mengine yote. Angewakanya henchmen wake kuwa pamoja na kuwa aliyeshinda si mkikuyu, ni mkenya ambaye amechaguliwa kidemokrasi no matter by what margin. Afterall angekumbuka kuwa huyu huyu Odinga ndiye aliyemsaidia yeye kuingia Ikulu mwaka 2002 kwa msingi wa utaifa ambao yeye kaamua kuubomoa. Vile vile amevuruga any future prospects za kuaminiana kati ya wakikuyu na makabila mengine ambayo ilikuwa imeanza kurudi nchini Kenya tangu Kenyata amwue Tom Mboya, na Moi amwue Robert Ouko.
Sidhani kama Kenyatta anastahili lawama katika hili la ukikuyu. Mzee Kenyatta alitawala miaka 15, tena akiwa babu. Alifanya kazi na Jaramogi Odinga kidogo, halafu miaka mingi na Moi. Hasa ile miaka ya 1970's basically ni Moi alikuwa anaendesha hiyo nchi, mzee Kenyatta alishajichokea! Na hata baada ya hapo, Moi alipata miaka mingine 24, muda wa kutosha kabisa kurekebisha kasoro hizo. Moi alisema anafuata "nyayo", binafsi sielewi ni nyayo zipi, lakini kama alifuata hizo za siasa za ukabila, wakenya ni mashahidi, na wanaosoma hii forum wanaweza kutoa maoni yao.
Miaka ile ya 1970's, wakenya wengi waliopinga serikali ya Kenya walikuwa wakikuyu pia, japo mzee Kenyatta mkikuyu mwenzao alikuwa madarakani. Ukisoma maandishi ya akina Ngugi wa Thiong'o, Ngugi wa Mirii, Micere Mugo, n.k., na mambo yaliyowapata baada ya kuandika maandishi hayo hutahitaji ushahidi zaidi. Vitabu vya Ngugi kama "Detained" na "Devil on the Cross" vinashambulia serikali moja kwa moja. Vingine "A Grain of Wheat", "Petals of Blood", vyote wanalia kuwa uhuru bado. Mzee Odinga naye kilio chake kilikuwa hichohicho alipoandika "Not Yet Uhuru", lakini kwa sababu ya mizizi ya ukabila iliyokuwapo tangu kabla, hakuweza kuungana na hawa wakikuyu ingawa wote walikuwa wakipinga serikali hiyohiyo katika muktadha uleule. Na waandishi wa kikikuyu wakaamua kujitoa wazi na kuanza kutukuza "ukikuyu" badala ya u-Kenya. Alishaanza Ngugi wa Thiong'o ku-blend upinzani wa kisiasa na utamaduni wa kikikuyu kwenye "The River Between" na "Weep Not, Child", akitukuza hasa mila ya ukeketaji na kubeza wasiotahiriwa. Akaleta nyingine ya kikikuyu kabisa "Ngaahika Ndeenda-I will marry when I want", na siku hizi naambiwa ameamua kuandika kikikuyu tu, wala hata si kiswahili ambayo huko Kenya ni lugha ya Taifa!
Kwa hiyo kwa kutazama fasihi, ambayo kwayo kimsingi jamii hujidhihirisha kwa jamii nyingine, tunaona kuwa jamii ya Kenya haikuanza ukabila na Kenyatta wala Kibaki. Mizizi hiyo ilikuwapo tangu kabla ya uhuru, na kuna watu wangependa ibaki hivyo, na wamekuwa wakiitetea waziwazi. Viongozi wangeweza kutumia uzalendo kurekebisha hali hiyo tangu mapema. Kenyatta alikuwepo kwa miaka 15, ambayo mingi ya hiyo Moi alifanya kazi za urais (akiwa makamu) chini ya kivuli cha "babu", hadi mzee wa watu alipojifia kwa amani usingizini mwaka 1978. Moi ambaye hujulikana pia kama "profesa" wa siasa za Kenya akachukua nafasi hiyo kwa miaka 24, na kwa hakika amekuwa rais wa Kenya hadi leo hii, (inadaiwa "Mwai Kibaki" humaanisha pia "Moi Kabaki").
Kwa hiyo nani hakutimiza wajibu wake katika kupambana na jinamizi la ukabila huko Kenya? Jibu mnalo!
Hapana wame-withdraw na kusema kuwa wako concerned na allegations za vote fraud. Wametamka kuwa wanashirikiana na pande zote mbili kutatua mgogoro wa kisiasa uliozuka Kenya na kusababisha vifo visivyokuwa vya lazima.hujasikia Marekani imetuma salaam na kuwataka Wakenya watulie na kujenga nchi yao
hujasikia Marekani imetuma salaam na kuwataka Wakenya watulie na kujenga nchi yao
Atatumiwa vipi salam na kiapo chenyewe kakosea..Hivi kuna Rais/nchi yeyote ambayo imeishatuma salaam za pongezi kwa Kibaki???