Kazi ipo kweli kweli; kama una kiongozi anayeona 3% ni idadi ndogo basi ujue tunaelekea kubaya!VIOLENCE IN KENYA DOES NOT MEAN THE COUNTRY IS BURNING
The population directly affected by the violence is less than 3% of the Kenya population. The police are containing the affected areas where there is violence. Kenya is not burning and not at the throes of any division.
These areas and more than 33 million Kenyans are not is any way in danger or affected by the violence. Only a few hundred thousand people
It should be noted that majority of Kenya cities and areas are safe and not facing any tension for example Machakos, Narok, Nakuru, Garissa and many other cities and towns are unaffected.
Dr. Alfred N. Mutua
Public Communications Secretary &
Government Spokesperson
Source: Official Website of KE Office of Public Communications
Kazi ipo kweli kweli; kama una kiongozi anayeona 3% ni idadi ndogo basi ujue tunaelekea kubaya!
=====================
Nimeanza kuona kuwa sasa kweli Kibaki amerudi and he is there to stay. Watu wameanza kuizoea hali na kidogokidogo wanaikubali, hata hapa kwenye forum wanaonesha hivyo. Hasira zimepungua. Punde mambo mengine kama mahitaji ya kimaisha (chakula, huduma mbalimbali) yatachukua nafasi, na watu watarudi kuwatafutia watoto wao nafasi za shule, ni januari hii. Chuma kinaelekea kupoa, hakitapondeka tena. Raila na wenzie wamesahau msemo huu "strike the iron while it's still hot". Bw Odinga, chuma chapoa hicho, kallaghabaho!
Mambo haya yapo sana kwetu. Ukipata taarifa za msiba unajitupa chini na kujigalagaza huku ukiangua kilio, unachafuka kila mahali. Ajabu siku ya mazishi unaonekana na suti mpya nyeusi, tena nyote na nduguzo kama sare, hata tunashangaa mlipataje muda wa kufikiria sare kama mlikuwa na uchungu kiasi hicho. Baada ya maziko, siku hiyohiyo inafuata pilau, ndizi mbivu na vinywaji. Wale waliokuwa wanajigaragaza chini tunawaona wanacheza karata na kutaniana! Kila kitu kinasahaulika, maisha yanaendelea! Ndivyo tunavyosahau msiba, na ndiko Raila na wenzie wanakoelekea, hivi punde watasahau yote, kama mwendo ndio huu wa kusuasua. Yetu macho!
Taarifa kutoka kwa wanahabari wa BBC news wameonyesha nyumba zinavyochomwa huko vijijimi. Hizi ni nyumba za nyasi na sidhani kama hawa raia wa kawaida wana insurance, itawachukua muda kuweza kujenga hizi nyumba upya bila msaada wowote kutoka serikalini.
Hii ni tabia ambayo Robert Mugabe aliitumia kule zimbabwe kuchoma nyumba za walalahoi. Helicopter ya BBC imeonyesha unyama huu lakini wanaofanya hawakuweza kuonyeshwa. HII NI AIBU KWA AFRIKA.
Majeshi yetu yanalipwa kutokana na pesa ya walipa kodi ili yawalinde na sio kuwapiga na kuwavunja miguu na mikono. Hivi viongozi wetu wa Afrika ni lini wataweza kusahihisha matatizo kama haya ili yasiweze kutokea tena?
Silent diplomacy hadi lini ilifanikiwa? Lets break this stupid taboo na kuwaambia viongozi wenzetu hatuwezi kukubali tabia kama hizi kuendelea katika nchi za Afrika mashariki.
hivi inakuaje" rais " kibaki hadi sasa anaendelea kuwatumia mawaziri wake wale wale katika vyeo walivyokua navyo hali wengine wamekosa ubunge?? hii ikoje...maana nijuavyo inabidi achague baraza lake na kiapishwe..sanasana sasa inebidi kibaki awe anadeal na ma PEMERNENT SECRETARIES