Kenya Election 2007: Outcomes

Kenya Election 2007: Outcomes

habari sasa hivi ni mbaya naomba ifikie hatua kibaki aondoke tu. Viongozi wa Afrika simameni imara mtoe hawa wazee mkianza na Kibaki mwenye miaka 76 na kisha Mugabe mwenye miaka zaidi ya 80.

Stop this nonesense. Bob Marley alisema Afrika tu unite Where are the leaders! hapa ndio nammiss Nyerere maana angekuwa ameshatangaza kutomtambua Kibaki.
 
Jamani hii ni RECENT ktk BBC,

http://news.bbc.co.uk/2/hi/africa/7166932.stm

Thirty Kenyans including many children have been burned to death in a church, after seeking refuge from the mounting violence over last week's elections. ...Endelea from Website ya BBC,

La Kujiuliza DEMOKRASIA hii watu wanaiweza?
Kwanini Amerika anajifanya kiranja wa Demokrasia wakati haiwezi?
Watu wanaoua wengine pasi na HATIA unaogopa nini baada ya Hapo?
Kujiunga kwetu na EAC, Kenya wana-natural za magomvi kama haya?

Lkn JE harakati dhidi ya Dhulma..Tutaifidia vipi? kuna Haki wengine kufa kwajili ya FAIDA ya KIZAZA KIJACHO?

LA KUJIULIZA kwanini WANANCHI wameuwawa KANISANI? Hii sawa na kule RWANDA na BURUNDI wananchi walipouwawa KANISANI? WHAT IS THE ROLE OF CHURCH IN KENYAN POLITICS?
 
VIOLENCE IN KENYA DOES NOT MEAN THE COUNTRY IS BURNING

The population directly affected by the violence is less than 3% of the Kenya population. The police are containing the affected areas where there is violence. Kenya is not burning and not at the throes of any division.

These areas and more than 33 million Kenyans are not is any way in danger or affected by the violence. Only a few hundred thousand people

It should be noted that majority of Kenya cities and areas are safe and not facing any tension for example Machakos, Narok, Nakuru, Garissa and many other cities and towns are unaffected.

Dr. Alfred N. Mutua
Public Communications Secretary &
Government Spokesperson

Source: Official Website of KE Office of Public Communications
Kazi ipo kweli kweli; kama una kiongozi anayeona 3% ni idadi ndogo basi ujue tunaelekea kubaya!
=====================
 
leo niko mbali sana na vyombo vya habari,huko kenya nini kinaendelea? nimepata bahati ka-mtandao ka kudandia mpaka saa nne usiku.Kuna mtu ameniambia jamaa zetu(walalahoi) wanachinjana sana.
 
Kazi ipo kweli kweli; kama una kiongozi anayeona 3% ni idadi ndogo basi ujue tunaelekea kubaya!
=====================

Tell me about it John,

Kuna watu hawathamini maisha bila kujua kuwa hata akifa mtu mmoja tu unnecessarily ni makosa makubwa sana.

Wakoloni weusi hawa wanajali pesa zaidi kuliko maisha ya watu!
 
Nimeanza kuona kuwa sasa kweli Kibaki amerudi and he is there to stay. Watu wameanza kuizoea hali na kidogokidogo wanaikubali, hata hapa kwenye forum wanaonesha hivyo. Hasira zimepungua. Punde mambo mengine kama mahitaji ya kimaisha (chakula, huduma mbalimbali) yatachukua nafasi, na watu watarudi kuwatafutia watoto wao nafasi za shule, ni januari hii. Chuma kinaelekea kupoa, hakitapondeka tena. Raila na wenzie wamesahau msemo huu "strike the iron while it's still hot". Bw Odinga, chuma chapoa hicho, kallaghabaho!

Mambo haya yapo sana kwetu. Ukipata taarifa za msiba unajitupa chini na kujigalagaza huku ukiangua kilio, unachafuka kila mahali. Ajabu siku ya mazishi unaonekana na suti mpya nyeusi, tena nyote na nduguzo kama sare, hata tunashangaa mlipataje muda wa kufikiria sare kama mlikuwa na uchungu kiasi hicho. Baada ya maziko, siku hiyohiyo inafuata pilau, ndizi mbivu na vinywaji. Wale waliokuwa wanajigaragaza chini tunawaona wanacheza karata na kutaniana! Kila kitu kinasahaulika, maisha yanaendelea! Ndivyo tunavyosahau msiba, na ndiko Raila na wenzie wanakoelekea, hivi punde watasahau yote, kama mwendo ndio huu wa kusuasua. Yetu macho!
 
guys I need to speak "live" with someone from Kenya leo. mimi nitapiga simu tusikie directly from Kenya. Kama kuna mtu niandikie PM..
 
Nimeanza kuona kuwa sasa kweli Kibaki amerudi and he is there to stay. Watu wameanza kuizoea hali na kidogokidogo wanaikubali, hata hapa kwenye forum wanaonesha hivyo. Hasira zimepungua. Punde mambo mengine kama mahitaji ya kimaisha (chakula, huduma mbalimbali) yatachukua nafasi, na watu watarudi kuwatafutia watoto wao nafasi za shule, ni januari hii. Chuma kinaelekea kupoa, hakitapondeka tena. Raila na wenzie wamesahau msemo huu "strike the iron while it's still hot". Bw Odinga, chuma chapoa hicho, kallaghabaho!

Mambo haya yapo sana kwetu. Ukipata taarifa za msiba unajitupa chini na kujigalagaza huku ukiangua kilio, unachafuka kila mahali. Ajabu siku ya mazishi unaonekana na suti mpya nyeusi, tena nyote na nduguzo kama sare, hata tunashangaa mlipataje muda wa kufikiria sare kama mlikuwa na uchungu kiasi hicho. Baada ya maziko, siku hiyohiyo inafuata pilau, ndizi mbivu na vinywaji. Wale waliokuwa wanajigaragaza chini tunawaona wanacheza karata na kutaniana! Kila kitu kinasahaulika, maisha yanaendelea! Ndivyo tunavyosahau msiba, na ndiko Raila na wenzie wanakoelekea, hivi punde watasahau yote, kama mwendo ndio huu wa kusuasua. Yetu macho!

Ina maana unataka kusema kuwa hao watoto na wanawake waliochomwa moto wakiwa kanisani ni hali kutulia au kwenda kwenye another level?

Umesoma report ya red cross kuhusu maelfu ya wakikuyu wanaokimbia rift valley kwa sababu kalenjin wameingia msituni kuanza chinjachinja? Kibaki anadhani amecheza vizuri kwa kuzuia media ila in the end media ikirudi nakuonyesha yaliyotokea wakati kenya imegeuzwa kuwa north korea basi itabidi urudi kuedit hii post yako.

Kinachoendelea Kenya ni ugly, kama una ndugu mji wowote kenya isipokuwa Central Province na some parts za eastern mpigie simu akuambie what is going on!

Aibu tupu, kibaki afanye alichofanya moi kwa kukimbia nchi la sivyo taifa litaangamia. Kutuliza nairobi kwa polisi wakati the whole country inaungua ni upppuuuuuuuuuuzi na unyama unaotakiwa kulaaniwa right now.
 
Wakenya wa hapa Houston wamepata hati yao ya kuandamana leo ...
 
Taarifa kutoka kwa wanahabari wa BBC news wameonyesha nyumba zinavyochomwa huko vijijimi. Hizi ni nyumba za nyasi na sidhani kama hawa raia wa kawaida wana insurance, itawachukua muda kuweza kujenga hizi nyumba upya bila msaada wowote kutoka serikalini.

Hii ni tabia ambayo Robert Mugabe aliitumia kule zimbabwe kuchoma nyumba za walalahoi. Helicopter ya BBC imeonyesha unyama huu lakini wanaofanya hawakuweza kuonyeshwa. HII NI AIBU KWA AFRIKA.

Majeshi yetu yanalipwa kutokana na pesa ya walipa kodi ili yawalinde na sio kuwapiga na kuwavunja miguu na mikono. Hivi viongozi wetu wa Afrika ni lini wataweza kusahihisha matatizo kama haya ili yasiweze kutokea tena?

Silent diplomacy hadi lini ilifanikiwa? Lets break this stupid taboo na kuwaambia viongozi wenzetu hatuwezi kukubali tabia kama hizi kuendelea katika nchi za Afrika mashariki.
 
Chair wa AU Jonh Kofur wa Ghana anaenda Nairobi kesho- this is AU initiative!

Source: BBC
 
Taarifa kutoka kwa wanahabari wa BBC news wameonyesha nyumba zinavyochomwa huko vijijimi. Hizi ni nyumba za nyasi na sidhani kama hawa raia wa kawaida wana insurance, itawachukua muda kuweza kujenga hizi nyumba upya bila msaada wowote kutoka serikalini.

Hii ni tabia ambayo Robert Mugabe aliitumia kule zimbabwe kuchoma nyumba za walalahoi. Helicopter ya BBC imeonyesha unyama huu lakini wanaofanya hawakuweza kuonyeshwa. HII NI AIBU KWA AFRIKA.

Majeshi yetu yanalipwa kutokana na pesa ya walipa kodi ili yawalinde na sio kuwapiga na kuwavunja miguu na mikono. Hivi viongozi wetu wa Afrika ni lini wataweza kusahihisha matatizo kama haya ili yasiweze kutokea tena?

Silent diplomacy hadi lini ilifanikiwa? Lets break this stupid taboo na kuwaambia viongozi wenzetu hatuwezi kukubali tabia kama hizi kuendelea katika nchi za Afrika mashariki.

Wataweza wapi wakati wanatumia the same book.
M7 ametumia the same huko Uganda na CCM walitumia the same game huko Zanzibar kwa hiyo ni the same recyclying inaendelea over and over again!
 
hivi inakuaje" rais " kibaki hadi sasa anaendelea kuwatumia mawaziri wake wale wale katika vyeo walivyokua navyo hali wengine wamekosa ubunge?? hii ikoje...maana nijuavyo inabidi achague baraza lake na kiapishwe..sanasana sasa inebidi kibaki awe anadeal na ma PEMERNENT SECRETARIES
 
Hili suala la Kenya linaonyesha jinsi gani Mwl Julius Kambarage Nyerere (RIP) alivyokuwa visionary . Matatizo ya ukabila Nyerere alianza kudeal nayo mwaka 1961 , na wakati huo nchi nyingi zilimcheka ! Kama alivyosema Mwanakijiji hili suala la Uchaguzi linatumiwa kama catalyst tuu ila reaction ilianza siku nyingi kidogo . Wazungu wanasema you reap what you sow , sio kama nafurahia lakini hizi ndio fruits za ukabila .... Hata kwenye blog zao wanaendelea kubishana juu ya ukabila while their country is in flames , it doesn't make sense at all .

Jamani ODM na PNU ondoeni tofauti zetu minusuru Kenya , Kibaki achia madaraka uinusuru nchi yako.
 
hivi inakuaje" rais " kibaki hadi sasa anaendelea kuwatumia mawaziri wake wale wale katika vyeo walivyokua navyo hali wengine wamekosa ubunge?? hii ikoje...maana nijuavyo inabidi achague baraza lake na kiapishwe..sanasana sasa inebidi kibaki awe anadeal na ma PEMERNENT SECRETARIES

Ndio ujinga huo hawa mawaziri walipoteza kazi bunge lilipovunjwa lakini kwa sababu Kibaki bado yupo wanafikiri ni halali yao kutumia madaraka vibaya ambayo hawana. Utafikiri hizi kazi na vyeo walizaliwa navyo.
 
habari za uhakika ni kuwa kibaki alitaka kukubali matokeo baada ya kuona gap ilikuwa kubwa sana aliyoachwa na raila..kilichotokea ni kuwa makabila yote mbali ya kikuyu waliamua kumuunga mkono raila ili kuondokana na ukabila wa kibaki na genge lake la wakikuyu wa MOUNT KENYA MAFIA..hata pamoja na kibaki na wenzake kuunga mkono kalonzo abakie ili kugawa kura hawakufanikiwa...

sasa wanasema baada ya kibaki kuona mambo ni magumu ndugu zake wakikuyu wakamuambia asikubali..ndio wakamuambia awaachie kazi ya kucheza na kura...hasa kwa kutumia mtandao wa maafisa wa ECK wakikuyu walio matawini..ambao makusudi hawakupeleka matokeo ECK KWA wakati ili wajue kuna pengo la kura ngapi ...wafidie ..thats why maeneo yote yaliyotangulia kutangazwa ni yale raila aliyoongoza....wizi huu wa kura utafanya jamii ya kikuyu ambayo imetapakaa nchini kote itapigwa vita sana na hii haitakuwa vema..

mimi nafikiri nchi ya kenya lazima itoe fursa kwa makabila madogo kuongoza nchi ..sio lazima rais awe mkikuyu au luo...nafikri makabila madogo yakipata fursa ni vema kwa kuwa hayafungamani na upande wowote.....
 
Tanzania Marais wake:

Nyerere - Mzanaki - Wazanaki wangapi wamejaa serikalini?
Mwinyi - Muunguja - waunguja wangapi
Mkapa - Mmakua/mmakonde
Kikwete - Mkwere

Mawaziri Wakuu
Kawawa - Mngoni?
Sokoine - Mmasai
Warioba - Mkurya?
Salim - Mpemba
Sumaye- Muiraqw
Lowassa - Mmeru

Kwanini kwenye nafasi nyingi za juu za kisiasa hatukuwapa wale wenye advantage ya kuwa makabila makubwa (Wasukuma na Wanyamwezi) au yale makabila yaliyopata upendeleo tangu ukoloni? (Wahaya, Wachagga, na Wanyakyusa)?

Rafiki yangu mmoja alikuwa ananimbia kuwa huko Kenya ilifikia mahali kuwa baadhi ya watu hawaendi kwenye vilabu au hoteli fulani kisa mmiliki ni mtu wa kabila fulani. Pamoja na matatizo yetu Tanzania Mchagga akichoma nyama utakuta hata wanaowakejeli na kuwaona wakabila wanakuwa wa kwanza kumchangamkia ndafu na hawatachelewa kuchangamkia mtori na kuteremshia kwa mbege!

Je yawezekana ile mila na desturi ya "utani wa jadi" imetuondolea mambo mengi kiasi unaweza kumwambia mtani wako ukweli na asiumizwe na kisasi? Je Wakikuyu na Waluo, Wakamba na wengineo wanaweza kuwa na utani wa jadi?
 
Mkuu Mwanakijiji, nadhani hili la watani wa jadi nk limesaidia sana kupunguza tension kati ya makabila, na bahati yetu nyingine ni kuwa hata makabila 'makubwa' pia yapo mengi...unazungumzia wasukuma, wanyamwezi, wachagga, wahaya, wanyakyusa, wahehe, nk...so ni ngumu kwa kabila moja kuwa dominant dhidi ya mengine yote.

Suala la kuoeleana pia limechanganya sana kiasi kwamba kwa mfano mi nimejikuta nina mashemeji karibu kwenye makabila walau manne makubwa!

So ukabila kwa TZ itachukua muda kuweza kufikia walipofikia wenzetu huko Kenya!
 
Mwanakijiji,

..hivi Wamasai siyo kabila kubwa kweli?

..nadhani Marasi wetu, tukianzia na Nyerere wamekuwa fair sana ktk teuzi za kisiasa.

..huu utani wa jadi sijui umeanza lini. but it is a very interesting phenomenon.

..settler economy ilikuwa inawahamisha na kuwachanganya watu wa makabila mbalimbali Tanganyika.

..watanzania hatukuanza kuchanganyika baada ya Uhuru na JKT. tulianza kabla ya hapo.

..demographically hakuna kabila kubwa linaloweza ku-sway Uchaguzi Tanzania.

..Kenya Wakikuyu wako wengi na vilevile ndiyo walioteseka zaidi ktk kudai Uhuru.

..busara ya hali ya juu ilipaswa kutumika kupiga vita ukabila Kenya.

..wakikuyu as the biggest voting block wangeweza kuweka mkakati wa kulinda maslahi yao ya kiuchumi na kisiasa bila mwenzao kuwa RAISI wa Kenya.
 
Back
Top Bottom