Leo jioni saa 5PM Mr Kibaki amewaappointed 17 ministers wakiwemo makamu wake yaani Kalonzo aliyekuja namba tatu kwenye kura za 2007:
0. Vice - President - Kalonzo Musyoka (ODM-KENYA)
1. Internal Security Prof George Saitoti (PNU)
2. Defence Yusuf Hajji (PNU thru KANU)
3. Special Programmes Naomi Shaban (ODM-KENYA)
4. Public Service - Asman Kamama (PNU thru KANU)
5. Finance Amos Kimunya (PNU)
6. Education Prof Sam Ongeri (PNU thru KANU)
7. Foreign Affairs Moses Wetangula (PNU thru FORD-KENYA)
8. Local Government Uhuru Kenyatta (PNU thru KANU)
9. Information and Communications Samuel Poghisio (ODM-KENYA)
10. Water and Irrigation John Munyes (PNU thru FORD-KENYA)
11. Energy Kiraitu Murungi (PNU)
12. Roads and Public Works John Michuki (PNU)
13. Science and Technology Noah Wekesa (PNU)
14. Justice and Constitutional Affairs Martha Karua (PNU)
15. East Africa Cooperation Dr Wilfred Machage (PNU)
16. Transport Chirau Ali Mwakwere (PNU thru SHIRIKISHO)
____________________________________________________________
NB: Kibaki ameonyesha wazi kwamba hana nia ya kufanya mazungumzo yaliyo serious na ODM. In fact anafanya haya mazungumzo tu as a public relations gimmick ili asijelaumiwa na the so-called Donor Countries and "International Community" kwa kuwa asiyesikiliza advaisi.
1. If kulikuwepo na goodwill or softening on the side of the ODM ina maana kwamba sasa usiku wa leo watachukua a hardline position wakati wataanza mazungumzo ya roundtable kesho chini ya usimamizi wa Kufuor. Already wamekashifu hio action ya Kibaki na kuianika hadharani kama tuu mojawapo ya ishara chungu nzima za kuonyesha kwamba Kibaki ana kiburi na sio hata mtu wa kufanya dialogue naye.
2. Kuna uwezekano kwamba hii action haitamfurahisha Kufuor ambaye ataiona kama njia moja ya serikali kujaribu kusend signal kwake kwamba yeye ni mgeni huku tuu na hawatayachukulia atakayosema seriously. Tusisahau kwamba msimamo wa awali wa akina Kibaki ulikuwa eti this is an internal crisis na haliihitaji outsider mediation. Baada ya kuona international community inawasapot akina ODM ndio Kibaki walibadili msimamo na kusema wako ready for dialogue. Kwa maoni yangu walifanya hivi tu kama ukatuni ila ndani ya nyoyo zao hawana haja sana na hizi mazungumzo. Kutangazwa kwa baraza hili at the same time that Kufuor's plane ilikuwa inatua Nairobi yaani 5.pm sio ajali wala sadfa ila ni symbolic message kwa ODM kwamba liwe liwalo Kibaki hatabanduka ikulu.
3. ODM wamesema hawaitambui serikali ya Kibaki na watakapoingia bungeni wiki ijayo wataketi kwenye mkono wa kulia wa Spika yaani upande wa serikali kwajili hao ndio walioshinda eti. Wamesema watampigia kura MP (Emuhaya) Dr Marende kama spika. Anatoka Western mkoa na deputy wake watampa muislamu msomali atokaye North Eastern Province, Farah Maliim. MP (Lagdera). Hizi nafasi mbili ambazo ni muhimu sana katika njama za kesho za kumuangusha Kibaki kama vile vote of no-confidence which ukiniuliza is one of the cards ODM inayo up their sleeves. ODM na washirika wao NARC pamoja wana viti 109 na serikali na vyama vidogo vinavyowaunga mikono wana viti 101. Kwa hivyo tunaweza nashiri ODM watashinda kwa hili next week. Leo wabunge wote waliochaguliwa kwa tikiti ya chama cha ODM wamefanya closed-door meeting hapa Nairobi kupanga mada watakayowakilisha kwa roundtable mazungumzo na plani yao ya Bunge wiki ijayo. Walikataa kuwadokezea wanahabari na wananchi ni nini wanapanga kufanya.
4. Kile ambacho kinashangaza wengi ni the way ODM wanaonekana kuwa very relaxed ni kana kwamba wanampango wa siri ambao wengi hata wafuasi wao hatujui. Hawaonekani kuwa wenye stress kama vile wafuasi wao. Kutangazwa kwa baraza nusu la mawaziri kumepokelewa na riots na protest kwenye mikoa ya Rift Valley, Nyanza na Western ambako wengi wameuawa na kupoteza makao na hali ilikuwa inaanza rejea kawaida. Wananchi wanazidi kuamini sasa kwamba Kibaki hataki amani au njia za amani na waliohojiwa kwenye mji wa majani chai uitwao Kerichp walisema kwamba wameshtushwa na action hii ya Kibaki ambayo imewapea wafuasi wa PNU na msaliti Kalonzo viti vikubwa vikubwa na kubakisha "baksheesh ministries' eti for ODM in case ODM wataamua kujoin na Kibaki. Walisema kwamba sasa wanasubiri lolote lile wataambiwa na viongozi wao wa upinzani huku wakisisitiza hawaitambui serikali ya Kibaki.
5. Kwa maoni yangu the road to peace bado ipo ndefu tuu na tusubiri michafuko na hali isiyo ya kawaida hadi pale akina ODM watarizishwa au kuonyesha kurizishwa na the political situation.
6. Mkapa, Chisano na Kaunda wametembelea mahali mbali mbali kulikoathirika ili kupata picha kamili vile hali ilivyo huku. Wanasema hii itawapatia a certain objectivity endapo waalikwe kwenye table ya mazungumzo.
7. Kibaki alimtuma Uhuru Kenyatta kwa JK na maombi ya kisiri ambayo JK alipokea na kusisitiza msimamo wa Tanzania ni ule ule: no taking sides huku akihimiza suluhu ya amani itafutwe kwa mazungumzo baina ya pande zote mbili. Mda mchache baada ya kukutana na Uhuru JK alipokea ujumbe wa ODM na Raila kupitia Secretary General wa ODM Prof. Petern Anyang-Nyongo.
8. Mdogo wa Condooleza Rice amesema kwamba Marekani inataka suluhu la kudumu na sio tu la mda. Amesema endapo maongezi ya amani yatatibuka basi Kenya iwe ready for a long unstable political future ahead.
9. Viongozi wa ODM walipata sapot kutoka kwa chama kinachokeshimiwa sana cha wanasheria Law Society of Kenya (LSK) wataingia kwenye talks kesho na the constitutional/legal framework on their side. Kibaki ataingia with the political framework on his side, arguing that there is already a governing authority in the land ( yaani yeye) na instead ya kumuondoa ni kheri tu aboreshwe (thru so called Coalition government).
10. Kalonzo amefurahia sana kuteuliwa kwake kama Makamu wa Rais. Amesema eti sasa ako kwa nafasi nzuri kuwapatanisha Raila na Kibaki. Wengi wanaona kama hii ni marriage of convenience yaani kumpatia sapot Kibaki kwa njia mbili:
a) Endapo watakuwa serekali for 5 years ODM- Kenya watakuwa pamoja na PNU kwenye bunge. Na kuna uwezekano itakapoonekana wakenya hawako ready for another Kikuyu successor to Kibaki in 2012 yaani Uhuru Kenyatta basi wakikuyu watasapot Kalonzo ambaye ni mkamba na eneo lao la Eastern Province is the only other mkoa Kibaki alimshinda Raila apart from Central Province. Kwa hili tayari kina MKJJ wameshachambua kwamba kunauwezekano Kibaki na Kalonzo walikua washafanya njama kabla hata ya uchaguzi kugawa kura za Raila. Tusisahau kwamba Kivuitu na ECK walisema kuwa ni chama cha Kibaki PNU na cha Kalonzo ODMK ambazo zilimsukuma kwa pamoja atangaze results haram bila kuzipitia upya.
b) Endapo kutaitishwa kura nyingine for the presidential opponents yaani Kibaki na Raila anytime from now basi Kalonzo atamfaidi sana Kibaki. ODMK na PNU zitafanya campaign za pamoja na Kalonzo as the VP atawashinikiza wafuasi wake wampigie Kibaki kura ili a retain u VP wake. Kwa hiyo the so-called inbetween votes za Kalonzo zitamwendea Kibaki na kumpatia ushindi dhidi ya Raila. Lakini this view inasahau kwamba kuna wengi ambao waliompigia Kibaki ambao watampigia Raila au wengi walimpigia Kalonzo wataamua kumpatia raila rather than Kibaki. Vile vile wengine waliompigia Raila pia wanaweza mpigia Kibaki next time. Ila mood ilivyo sasa nchini ni kwamba Kibaki is very unpopular across the country because anaonekana kama ndiye aliyeleta shida nchini kwa kuapishwa kwake halahala usikusiku.
11. Aliyetuahidi eti this time ataappoint the so-called 'clean hands" government isiyo corrupt ndio huyu leo amemrejesha Kiraitu Murungi mmojawapo ambaye alihusishwa na sakata la AngloLeasing mpaka hata akajiuzulu. From the face of his new half cabinet, inaonekana wazi wazi kwamba Kibaki hakusoma any lesson from Kenyans rejection of his 21 ministers. Isiopkua tu wale wa KANU na ODM-K, wote wale wa PNU walikuwepo kwenye Baraza la mwaka jana. This means that Mr Kibaki is either out of touch with the feelings of the people he wishes to govern or has some of the most misleading advisors a president can ever have.
12. Kuhusu zile viti zingine 12 za nominations nimedhibitisha kwamba ODM itachukua lionshare, that is 6 na PNU 3 halafu.
Nawakilisha.
_____________________________________________________________________________________
KADHALIKA: KUNA PICHA SAFI
http://issamichuzi.blogspot.com/ZINAZOONYESHA
JK AKIKUTANA NA MJUMBE WA PNU/KIBAKI YAANI UHURU KENYATTA. PIA JK AKIPOKEA UJUMBE WA RAILA ODINGA/ODM KUTOKA KWA PROF. PETER ANYANG-NYONGO