Kenya Election 2007: Outcomes

Kenya Election 2007: Outcomes

11. Aliyetuahidi eti this time ataappoint the so-called 'clean hands" government isiyo corrupt ndio huyu leo amemrejesha Kiraitu Murungi mmojawapo ambaye alihusishwa na sakata la AngloLeasing mpaka hata akajiuzulu. From the face of his new half cabinet, inaonekana wazi wazi kwamba Kibaki hakusoma any lesson from Kenyans rejection of his 21 ministers. Isiopkua tu wale wa KANU na ODM-K, wote wale wa PNU walikuwepo kwenye Baraza la mwaka jana. This means that Mr Kibaki is either out of touch with the feelings of the people he wishes to govern or has some of the most misleading advisors a president can ever have.

Nilipokuwa mtoto darasa la 4, nilikuwa naona jamaa walioko form 4(darasa la 12) kuwa ni wasomi sana.

The same, kwa Kibaki. Kwa vile yeye uwezo wake wa kuwa clean ni mdogo sana, basi usishangae kuwa anaona jamaa hawa alioteuwa kuwa ni clean sana.
 
Mwalimu unachosema ndicho ambacho mara nyingi kimetokea. Kuzungukwa na polisi, kupigiwa saluti, na ving'ora kila aendako inamfanya mtu ajihisi "yeye ni yeye". Mwalimu alikiita hicho chote kuwa ni "sheer pomposity"!

Sababu ya Kibaki kutaka kuapishwa mapema ni dhahiri sasa kuwa it gave him command over state organs. Kitu kimoja ambacho kinaweza kutokea ni pale majenerali wa jeshi watakaposema kuwa kama jeshi linashindwa kumtambua Kibaki kama Rais na hivyo kuondoa utii wake kwake utakuwa ni mwisho wa Kibaki.

Lakini kwa kadiri vimulimuli na ving'ora vinaendelea Kibaki ana nguvu kubwa kuliko watu wanavyofikiria. Hadi hivi sasa Kibaki hahitaji recognition ya mtu mwingine yoyote kuwa ni Rais wa Kenya kwani tume imemtangaza hivyo (licha ya kauli za kigeugeu za Mwenyekiti wa Tume).

Najaribu kukaa chini na kufikiri ni jinsi gani wa Kenya wanaweza kufikia usuluhishi bila

a. Kibaki Kujiuzulu
b. Raila kuendelea kutomtambua Kibaki kama Rais?

Jibu ninaloliona ni sifuri!
 
Mwalimu unachosema ndicho ambacho mara nyingi kimetokea. Kuzungukwa na polisi, kupigiwa saluti, na ving'ora kila aendako inamfanya mtu ajihisi "yeye ni yeye". Mwalimu alikiita hicho chote kuwa ni "sheer pomposity"!

Sababu ya Kibaki kutaka kuapishwa mapema ni dhahiri sasa kuwa it gave him command over state organs. Kitu kimoja ambacho kinaweza kutokea ni pale majenerali wa jeshi watakaposema kuwa kama jeshi linashindwa kumtambua Kibaki kama Rais na hivyo kuondoa utii wake kwake utakuwa ni mwisho wa Kibaki.

Lakini kwa kadiri vimulimuli na ving'ora vinaendelea Kibaki ana nguvu kubwa kuliko watu wanavyofikiria. Hadi hivi sasa Kibaki hahitaji recognition ya mtu mwingine yoyote kuwa ni Rais wa Kenya kwani tume imemtangaza hivyo (licha ya kauli za kigeugeu za Mwenyekiti wa Tume).

Najaribu kukaa chini na kufikiri ni jinsi gani wa Kenya wanaweza kufikia usuluhishi bila

a. Kibaki Kujiuzulu
b. Raila kuendelea kutomtambua Kibaki kama Rais?

Jibu ninaloliona ni sifuri!

Mwanakijiji,

Kuunganisha kile umesema hapo juu, ni kweli kabisa Kibaki anafikiria nguvu ya kijeshi. Hebu ona jinsi alivyosaini hii statement aliiyoitoa kwa media:

MWAI KIBAKI, C.G.H., MP. President and Commander -In-Chief of the armed forces of the Republic of Kenya. Nairobi 8th January, 2008

Kulikuwa na sababu yeyote ya kuweka the commander in chief of the armed forces......?
 
Mwanakijiji,

Kuunganisha kile umesema hapo juu, ni kweli kabisa Kibaki anafikiria nguvu ya kijeshi. Hebu ona jinsi alivyosaini hii statement aliiyoitoa kwa media:



Kulikuwa na sababu yeyote ya kuweka the commander in chief of the armed forces......?

Mwafrika, wazo zima la siasa za Kenya sasa hivi hazina SABABU YE YOTE. Kibaki anachofanya ni kuendeleza kutokuwa na sababu ye yote.

Swali ni je, akiwa kama Commander-In-Chief of Armed Forces, je anayo loyality na utiifu wa hizo Armed Forces kweli? Yasije yakawa ya Dr. Obote vs Gen. Amin hapo, au Sir Tolbert vs Master Sgt. Doe.

Mmoja anadai ni mkuu wa majeshi na mwingine ndiyo kweli anaongoza majeshi!
 
Mzalendohalisi,

Inatakiwa Wakenya wamng'oe Kibaki hata kwa kutumia nguvu kwa faida ya nchi yao.

Kibaki akibaki madaraka itakuwa ni pigo kwa wapenda demokrasia Afrika, maana hata akina Karume, Mugabe na wengine wataendelea kuiba kura.

I have never known Mtanzania to be this much radical; but I think many peace loving people will ultimately be driven to have similar views in light of what is happening.

ODM wamekwishafungwa goli la mkono. Raila sasa atabakia kuwa kama yule Meya wa zamani wa Mexico City; aliyeng'ang'ania kuunda serikali mbadala bila ya mafanikio.
Mimi nadhani ni swala la muda tu sasa, mambo yataendelea kuwa shwari, na serikali ya Mh. Kibaki itazidi kuneemeka kwa miaka mitano ijayo.

Kila jambo, hata liwe baya halikosi 'silver lining' ya aina yake. Angalao kwa miaka mitano hii, haya majigambo ya ubora wao tuliyoyazoea, na ambayo tulikuwa tunayasubiri kwa hamu kutoka kwa hawa wenzetu wakenya, pengine kidogo yatakuwa yamepungua, kama wasipogundua mengine. Ni matumaini wao pia sasa watajiona kuwa hawapishana sana na sisi viumbe duni.

Sasa ngojea tuone watamfanya nini dikteta wao huyu - si walijifanya wao ni wajanja!
 
Let us be clear. Kenya is republic; nobody was born to be an indefinite ruler of Kenya. Through the balot box, Kenyans determine who runs their government for a period of five years after which his/her perfomance is assessed before renewing/terminating his/her contract. These people have said that Kibaki's contract will not be renewed; why the fuss?


Kibaki Must Go,
Or he will follow Saddam's path for the crimes commited against humanity causing
life loss for more than 1000 innocent Kenyans because of his power hunger!!!


God Bless Kenya

kenya-flagmap-64px.png

 
Mzee alisema anataka kumaliza miaka yake mingine mitano na kurudi nyumbani; hii ndiyo iliyokuwa kauli mbiu yake. Siri aliyowaficha waKenya, ni kuwa watake wasitake, hiyo miaka yake mitano ataichukua. Kwa mwendo huu, hiyo mitano itakapokwisha, si ajabu akanyakua mitano mingine, hadi hapo Muumba wake atakapomchukua kwa mapenzi yake.

Hapana, Sadam, Charles Taylor, Noriega na wengineo wa kundi hilo ni tofauti sana na Kibaki. Maslahi ya 'wakubwa' Kibaki hajayagusa na ataendelea kuyalinda. Kibaki sio tishio kwa njia yoyote ile. Si ajabu Raila ndiye anayeonekana kuwa tishio zaidi kwa maslahi haya, na ndio sababu ya wakubwa kukimbilia haraka haraka kuingilia mgogoro kabla ya mambo hayajawa mabaya zaidi. Na wengine walikimbilia haraka haraka kumtambua kuwa mshindi (kabla ya kujirekebisha kwa kufunika kombe, baada ya kuona namna ya unyang'anyi wa kijambazi ulivyotendeka)Sasa hivi wanasubiri tu mambo yapoe kabla ya kuendelea na shughuli kama kawaida.

Kumwondoa Kibaki kwa nguvu hilo wakenya wasahau; ndi maana mzee anafanya mambo kwa kujiamini, kana kwamba hakuna lolote lililoharibika.
 
Hili likibaki mi nalichukia sana.

Yaani mimi naona tumerudi nyuma katika suala demokrasia hapa Africa!!!

Kuna mambo mengi ya kujifunza kutoka kwenye huu uchaguzi mengine ya kiuchumi, kisiasa, kijamii n.k.

Mimi nizungumzie Kiuchumi.

1. Nchi jirani Uganda, DRC, Rwana na Burundi,,, zione umuhimu wa kuwa pamoja na Tanzania kwa ajili ya backup in case Kenya au Tanzania ikiwa na matatizo kwenye mambo ya huduma ya Bandari.

2. Tanzania ijue kwamba bila kuwachukua wazungu directly from Ulaya,Asia na Amerika kwa ndege zetu, haiwezi kujivunia utalii endelevu, maana kama hivi kulikwa na machafuko Kenya, ndio hivyo tena KQ haikuleta watalii maana lazima wapitie Jomo Kenyata International Airport.

3. Kukiwa na Machafuko especially Dar es Salaam, Tanzania ndio ya kuathirika kuliko hata taifa lingine lolote,,, na sisi wala tusiangalie tu mambo ya siasa, hebu tufikirie Dar es Salaam ikinyisha mvua kwa masaa 72 mfufululizo what will happen, nina imani watu zaidi ya 200,000 wanaweza kufa...na uchumi utaadhirika kwa kiasi kikubwa kwa kuwa mayai yote yako kwenye kapu moja! (Mkapa aliwahi kwenye hotuba zake za mwezi kulizungumzia hili kwa machungu) sasa mimi sijui idara za maafa,,, huwa zinasubiri yatokee au zinambinu za ku-mitigate.

na mengine mengi sana!
 
hapa nnaona iko haja ya tanzania kujiaandaa vyema hii ni nafasi nzuri iliotuonyesha jinsi gani tuna mapungufu ya kujitegemea

jengine tuwasaidie wenzetu na kumwambia huyu mpuuzi black and white kuwa tunalaani hivi vitendo vyake vya kibarazuli.

tatu tuwatishie kuwa yakitokea ya kutokea tanzania haitapokea wakimbizi kutoka kenya
 
lakini wajimini baraza la mawaziri kumi na ushee tuuu??kwa hilo angekua kashinda kwa haki ningempongeza kwa kufanya jambo la maana sio kama sie mawaziri weeengi wakati kazi zingine zafanywa na raisi mwenyewe kama leo ukiniuliza kazi ya Membe ni nin wakat raisi naye anado kazi za mambo ya nje bado nakosa jibu..lets pray for majirani zetu wawe na peace back
 
halaf kingine nachojiuliza mie huyu babu aitwaye Saitoti ni mtu mwingineeee ama ni huyu huyu nimjuaye mie ambaye yuko serikalini toka enzi zileee?it means yeye ndiye Mungu wa Kenya ama?though yasemekana Moi naye bado ana power ila huyu Saitoti now ananitisha as pia it is said jamaa ndiye anaongoza kwa kuwa na mijihela mingi account za nje
 
Mi naomba niulize kwa nini Western media na hawa mediators wanajifanya kama hawawelewi:
- Kibaki siyo president! Ni self proclaimed. Hakuapishwa kihalali na hata election commisiner sasa anakana ushindi wake. So he is MR. Kibaki not President Kibaki, kuendelea kumwita president ni kuhalalisha 'coup d'etat civilien' aliyoifanya
- Power sharing is out of question as Kibaki did NOT win the election and he does not disupute anymore that, yeye anasema kwamba ndiye aliyetangazwa mshindi! Big difference! Sasa anasema kwamba ndiye aliyeapishwa! So he is not interesting in proving hata kwamba ameshinda kihalali
- ODM has majority in parlament, so the task of forming policies etc are int heir hands, they are the ones who can make or break the country, badala ya kukimbilia ikulu kumwona kibaki, hawa manegitoator wangetumia muda wao kupanga mikakati na ODM na Odinga.
- There's no ethnic cleanisng, bali walalahoi waliochoka na wanaochoma nyumba na duka za walalahoi wenzao! The dictator is just twisting happenings and intervening with his security forces! Where there are ethnic clashes si kitu geni maana ukabila ulikuwepo miaka mingi! It was always to the advantage of KANU and now Kibaki - divide and rule!
 
lakini wajimini baraza la mawaziri kumi na ushee tuuu??kwa hilo angekua kashinda kwa haki ningempongeza kwa kufanya jambo la maana sio kama sie mawaziri weeengi wakati kazi zingine zafanywa na raisi mwenyewe kama leo ukiniuliza kazi ya Membe ni nin wakat raisi naye anado kazi za mambo ya nje bado nakosa jibu..lets pray for majirani zetu wawe na peace back

Mtaalam,

Kwanza pongezi zako zimekuwa za haraka sana kuhusu ukubwa wa Baraza, Rais amesema ameteua hao kwanza wengine ataongeza baadaye!!! kwa hiyo note hiyo!

Pili;
Rais wa Jamhuri ya Tanzania pamoja na kuwa mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri, na Of course mkuu wa nchi na mkuu wa mawaziri wote, lakini ni anafanya kazi kwa karibu zaidi za mahusiano na mataifa mengine, uchumi, usalama wa nchi (ulinzi,polisi,siasa, etc.)

Na Waziri mkuu anafanya mambo mengi ya ndani ya nchi!!! ndio maana tawala za mikoa ziko kwa waziri mkuu, ambako ndio kazi nyingi za mambo yanayohusu ndani

Kwa hiyo Rais yuko sawa tu jamaa yangu mtaalamu,,, ni mindset tu inatakuwa ku-change!!!

By the way maelezo kama haya yalishatolewa hapa before
 
K-T
IS THERE REALLY LIGHTS AT THE END OF THE TUNNEL? ARE WE FIGHTING A LOSING BATTLE? YANI HIVI HIVI MARADONA ALIFUNGA BOA LA MKONO NA WAKACHUKUA KOMBE LA DUNIA NA JUU YAKE AKAPEWA MISIFA EVEN THOUGH WE ALL SAW BAADAYE KUWA LILIKUWA LA MKONO.

HIVI VOTE OF NO CONFIDENCE INATAKIWA KURA NGAPI?
HOW IS THE SPEAKER VOTED BY A SIMPLE MAJORITY AMA?
HOW CAN THE SPEAKER HELP ODM?



 
Wabunge bado hawajala kiapo, Bunge litakutana tarehe 15, Jan. Inashangaza eeh????
 
Sioni Sababu ya kumpeleka msuluhishi wa kimataifa(kuffor) wakati Kibaka ameshatangaza baraza lake na wizara zote nyeti ameshika yeye...hata kama kutakuwa na kugawana madaraka inamaana odinga atashika nafasi ipi?ikiwa musyoka ndio tayari ameshachukua VP!!
Kweli U-dikteta hautakwisha bara afrika....
 
hivi.. Mawaziri wanachaguliwa kabla ya kuapishwa kuwa wabunge? au unakuwa Waziri kabla hujawa Mbunge rasmi?


Swali zuri sana.

Huyu jamaa kafanya harakaharaka sana ku-consolidate power hadi kushindwa kufahamu kuwa mawaziri ni lazima watokane na wabunge, na mpaka sasa hivi Kenya haina wabunge bali wabunge wateule kwa vile hawajala kiapo. Wabunge watapatikana baada ya kula kiapo; hapo ndipo wanaweza kuteuliwa kuwa mawaziri. Sasa yeye kateua kutoka kwa marafiki zake kwa paparapapara tu bila kuangalia Katiba anayodai kuilinda. Inaonyesha jinsi gani alivyo dhaifu wa fikra na mroho wa madaraka.
 
Kichuguu, ndiyo maana kwenye Katiba yetu wa kwanza kuteuliwa ni Mwanasheria Mkuu ambaye Bungeni analeta jina la Waziri Mkuu (linafunguliwa na Spika), na wabunge wanapigia kura ya kukubali au kumkataa.. na baada ya hapo Waziri Mkuu anashauriana na Rais kuunda baraza la mawaziri. Sasa sijui Katiba ya Kenya inasemaje kwa sababu hawana Waziri Mkuu na hawana Makamu wa Rais ambaye ni mgombea Mwenza kama huku kwetu..
 
Back
Top Bottom